JE BIASHARA YAKO IMEDUMAA? FAHAMU MCHWA UNAOITAFUNA

NENO LA LEO (AGOSTI 17, 2020): JE BIASHARA YAKO IMEDUMAA? FAHAMU MCHWA UNAOITAFUNA.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambapo tunalianza juma jipya. Ni asubuhi hii ambapo tunaalikwa kuendeleza pale tulipoishia jana kama sehemu ya kuendelea kuwa bora zaidi. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi ya kusimamia biashara yako ili iweze kukua zaidi. Katika jamii tunayoishi kwa sasa watu wengi wana biashara bila kujali ukubwa wa biashara husika. Biashara hizi zinahusisha zile ambazo ni kwa ajili ya kuuza bidhaa au kutoa huduma kwa jamii. Kama ilivyo kwa viumbe hai kwenye hatua za ukuaji ndivyo ilivyo pia kwenye biashara. Kila mmiliki wa biashara anatamani kuona biashara yake ikiongezeka kutoka hatua ya biashara ndogo kuelekea kwenye biashara yenye mtaji mkubwa.

✍🏾 Hata hivyo, uzoefu unaonesha kuwa katika kundi kubwa la wamiliki wa biashara ndani mwao ni wachache ambao wamefanikiwa kukuza biashara zao. Biashara nyingi huwa zinadumaa na nyingine kufa kabisa katika kipindi cha awali toka kuanzishwa kwake. Wote tunakubaliana kuwa biashara yoyote ni lazima ihusishe mzunguko wa pesa. Usimamizi wa pesa inayoingia na pesa inayotoka huwa ndiyo roho ya ukuaji wa biashara ya aina yoyote ile.

✍🏾 Biashara nyingi zinakufa au kudumaa kwa kuwa wamiliki hawana mfumo mzuri wa kudhibiti mzunguko wa pesa. Biashara zinazokua ni zile ambazo wamiliki wana mfumo mzuri wa kudhibiti uingiaji na utokaji wa pesa. Tunapozungumzia pesa inayoingia kwenye biashara tunamaanisha mtaji unaouingiza kwa ajili ya kununulia bidhaa ili bidhaa hizo ziuzwe kwa faida. Hivyo pesa inayoingia inahusisha pesa unayopata kutokana mauzo ya bidhaa kama faida.

✍🏾 Kwa upande wa pesa inayotoka inahusisha gharama za kulipia pango la fremu, kulipa wasaidizi wa biashara kama wapo, kulipia umeme na gharama nyinginezo ambazo zinahusiana na uendeshaji wa biashara yako. Hapa unaweza kuona kuwa kuna sehemu ya mtaji ambayo inaingia kwenye biashara haizalisha faida ya moja kwa moja. Hapa ndipo wengi huwa wanakosea baada ya kuuza huwa wanachukulia kama vile mauzo ghafi yote ni sehemu ya faida katika biashara.

✍🏾 Kwa kushindwa kutofautisha mauzo ghafi na faida wengi huwa wanatumia pesa inayotokana na mauzo bila kufahamu kuwa pesa hiyo ndani mwake kuna mtaji. Zipo biashara nyingi ambazo wamiliki wanachukua pesa kutoka kwenye mauzo ya biashara husika bila kujua kuwa pesa hiyo inahusisha mtaji. Pia tabia nyingine ni pale wamiliki wanatumia faida yote bila kutenga sehemu ya faida kwa ajili ya kukuza biashara husika.

✍🏾 Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufundisha kuwa kama ambavyo viumbe hai wanahitaji hewa ya okxyjeni na chakula kwa ajili ya kukua na kuongezeka, biashara pia uhai wake unategemea udhibiti wa pesa inayoingia na kutoka. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona tofauti katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

https://fikrazakitajiri.blogspot.com/2020/01/orodha-ya-vitabu-nilivyosoma-katika.html?m=1.

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(