👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tena mwanzo wa juma tukiwa tunaelekea kwenye robo ya pili ya mwaka 2020. Hatuna budi kusema asanthe kwa baraka ambazo Mwenyezi Mungu anazidi kutujalia. Moja ya baraka kubwa iliyopo mikononi mwetu ni siku hii ya leo. Basi tukaitumie vyema kuendeleza jitihada za kuyafanya maisha yetu yawe na thamani.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo linatushirikisha baadhi ya kanuni muhimu ambazo unatakiwa kuzitumia kwa ajili ya kukuza utajiri wako. Hutake husitake pesa ina nguvu na itaendelea kuwa na nguvu katika kubadilisha ulimwengu tunaoishi. Ni kutokana na umuhimu huo tunatakiwa kujifunza mbinu muhimu ambazo zinatuwesha kuongeza pesa tunayomiliki. Karibu ujifunze kanuni ninazokushirikisha leo:-
✍🏾Tengeneza pesa za kutosha. Kila mara swali kubwa la kujiuliza linatakiwa kuwa: nifanye nini ili kukuza pato langu zaidi ya sasa. Hautakiwi kuridhika na chanzo kimoja cha pesa na badala yake chanzo kimoja kianzishe chanzo kingine na hatimaye uwe mifereji mingi inayotiririsha pesa kwenye mifuko na akaunti zako.
✍🏾Ilinde pesa yako. Ukiwa na pesa kuna vishawishi vingi ambavyo vinapelekea pesa ipotee mikononi mwako kwa kuwa haujui namna ya kuilinda pesa. Kuna maadui mengi wa pesa yako ambao wanaitolea macho. Mfano, ukiwa na pesa ndipo washauri wanaoongezeka, ukiwa na pesa ndipo watu wanaojiita marafiki wanakuwa wengi, ukiwa na pesa watu wanaokupenda wanakuwa ni wengi au ukiwa na pesa kesi nazo zinaoongezeka. Hivyo unatakiwa kuwa mbali na mazingira ambayo yatapelekea upoteze pesa yako kwa hasara.
✍🏾Jifunze kubajeti pesa yako. Pesa haijawahi kutosha mahitaji yaliyopo katika maisha ya kila siku. Tatizo linalopelekea kundi kubwa la watu katika jamii waendelee kuangaika kipesa ni tabia ya kutokuwa na bajeti. Watu wengi hawana vipaumbele kutokana na ukweli kwamba kila kinachopita kwenye macho wananunua. Matokeo yake ni kwamba pesa ambayo ingedumu kwa muda wa siku kadhaa inaisha ndani ya wiki moja. Baada pesa kuisha mhusika sasa ndo anatuliza akili na kuanza mipango ya kutafuta pesa nyingine tena.
✍🏾Jifunze namna ya kuifanya pesa iongezeke thamani. Pesa ambayo umeiweka kwenye akaunti ya kawaida haiongezeki thamani na sana sana inapungua thamani kutokana na makato ya gharama za huduma ya benki. Pesa inatakiwa kuvuja pesa (money should bleed money). Hivyo unatakiwa kuiwekeza pesa yako sehemu ambapo inaongezeka thamani. Pesa inatakiwa kuwekwa sehemu ambapo hata wakati umelala pawepo watu ambao wanaendelea kukufanyia kazi. Nieleweke kuwa pesa ili iwe na thamani ni lazima iwe kwenye mzunguko ambao unaifanya izalishe faida.
✍🏾Ongeza ufahamu au maarifa yako kuhusu pesa. Maarifa ni silaha muhimu ambayo itakuvusha salama kwenye safari yako ya kjufikia utajiri wa ndoto yako. Unahitaji kujifunza kwa kutumia mbinu zote ikiwa ni pamoja na kusoma vitabu, kuhudhuria semina za ujasiliamali na kuwa watu wa kukuongoza (financial coaches).
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufundisha baadhi ya kanuni muhimu kuhusiana na pesa. Hakikisha unapata nakala ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho utapata kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BON TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii:https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw