NENO LA LEO (AGOSTI 31, 2020): MAFANIKIO HUWA YANAAMBATANA NA NYAKATI ZA KUTENGWA.
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya katika uhai wa maisha yetu hapa Duniani. Ni siku ambayo tumepewa nafasi tena ya kuendelea na safari ya mafanikio ili hatimaye safari hiyo ihitimishwe kwa kishindo kikubwa cha mafanikio. Basi kwa pamoja tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii ili nipate yaliyo bora katika maisha”.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tujifunza kwa nini unatakiwa kuwa tayari kutengwa katika nyakati za safari ya kuelekea kwenye mafanikio unayotamani. Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuwa unapokuwa na ndoto ni lazima ndoto hiyo itafsiriwe kwenye malengo na malengo hayo pia yatafsiriwe kwenye matendo ya kila siku. Hivyo, kukamilisha ndoto yako ni lazima pawepo matendo ambayo umejidhatiti kuhakikisha kila siku unayatekeleza.
✍πΎ Ikumbukwe pia kuwa nilishawahi kuandika hapa kuwa ndoto ya mafanikio uliyonayo inatakiwa kuwa siri ambayo wewe pekee ndo mwenye kujua mapana na marefu yake. Hapa ndipo unaanza kutoeleweka kwenye jamii inayokuzunguka. Kuna matendo mengi ambayo kwako unafahamu kuwa yanachangia kwenye ukamilisho wa ndoto yako hila kwa wengine matendo hayo yataonekana ya hovyo.
✍πΎ Zipo nyakati ambazo utakimbiwa na marafiki kwa kudhania kuwa unakoelekea unapoteza dira. Kwa kuwa wewe ndo unaijua dira unayosafiria kuelekea kwenye mafanikio ya ndoto yako kamwe husikubali kuyumba au kurudi nyuma. Simama imara na endelea kwenye njia ambayo unaamini ni sahihi.
✍πΎ Zipo nyakati ambazo utapingwa na jamii. Katika nyakati kama hizo unatakiwa kutambua kuwa jamii haitambui misingi na kanuni unazotumia kuelekea kwenye kilele cha ndoto yako. Ni katika nyakati kama hizo ni lazima utambue kuwa kupingwa na kutengwa na jamii ni sehemu ya changamoto ambazo zinakukomaza kuelekea kwenye ile picha kubwa ya ndoto yako.
✍πΎ Zipo nyakati ambazo utaonekana kuwa tatizo kwa kuwa umeshindwa kusema ndiyo kwa kila unachoambiwa. Katika nyakati kama hizo endelea kusema hapana kwa kuwa kila unaposema ndiyo kwa kitu ambacho kipo kinyume na safari ya mafanikio yako moja kwa moja unakuwa umesema hapana kwa kitu chenye tija kwako. Hapa ndipo unatakiwa kutambua kuwa hakuna siku hata moja ambayo utawaridhisha binadamu wote.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kuendelea kuishi kwenye misingi na kanuni tunazoamini ni sahihi katika kutimiza ndoto zetu. Amua kutengwa au kumkubalia kila mtu na hatimaye majibu utayapata kulingana na maamuzi yako. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika utaona mabadiliko katika maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com