NENO LA LEO (APRILI 27, 2020): [UFUNUO] FAHAMU UTATU AMBAO UNAUNDA MAISHA YAKO HAPA DUNIANI

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ya siku nyingine tena ambayo tumepewa kwa ajili ya kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni zawadi muhimu katika Maisha yetu hasa tunapoendelea kutimiza malengo muhimu katika Maisha yetu. Basi wote kwa pamoja tuianze siku kwa kujisemea hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana na tumshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuliishi kusudi la maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo naendelea niakushirikisha utatu muhimu ambao unaunda Maisha yako. Mwanadamu yeyote ambaye anakusudia Maisha yake yawe na thamani hana budi kuelewa utatu huu na kuhakikisha ajiendelea kwenye kila eneo ndani huo utatu. Mwanadamu anaishi kwa ajili ya kujiendeleza katika vitu muhimu vitatu ambavyo ni: ROHO, MWILI na AKILI.

✍🏾Katika kipindi cha Maisha kila mtu mwenye kutaka kuishi Maisha yenye mafanikio ni lazima atambue kuwa sehemu hizi tatu katika Maisha yake ni muhimu na hakuna sehemu ambayo ni bora kuliko nyingine. Hivyo, mafanikio kwenye kila sehemu yanakamilishwa na mafanikio kwenye sehemu nyingine. Siyo sahihi kuendeleza roho na kusahau mwili na akili au kuendeleza akili huku ukisahau mwili na roho.

✍🏾Hapa ndipo tunaona umuhimu wa kuishi Maisha yenye uhuru wa kifedha kutokana na ukweli kwamba mtu hawezi kujiendeleza kimwili bila mahiaji muhimu ya chakula; mavazi; kinga dhidi ya mvua, jua kali au Wanyama wakali; na vitu muhimu vinavyomuwezesha kufanya kazi.

✍🏾Vivyo hivyo, mtu hawezi kujiendeleza kiakili kama hana uwezo wa kupata vitabu na muda wa kuvisoma; bila kuwa na uwezo wa kutembea nje ya mazingira aliyozoea na kujifunza kwa kuona; au uwezo wa kujifunza kutoka kwa marafiki wenye maarifa mbalimbali.

✍🏾Pia, ili kujiendeleza kiroho mhusika anatakiwa kuishi Maisha ya upendo na ni ukweli mtupu kuwa hakuna upendo katika Maisha ya dhiki kwa kuwa upendo msingi wake mkuu ni Maisha ya kutoa kwa wengine. Kwenye dhiki inayotokana na upungufu wa vitu kila mtu anatanguliza nafsi yake.

✍🏾Mwisho neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa ukamilisho wa Maisha yetu unaegemea sehemu kuu tatu ambazo ni MWILI, AKILI na ROHO. Kila sehemu ina haki ya kuendelezwa na yeyote anayefanikiwa kuendeleza sehemu zote ndiyo tunasema amefanikiwa kuishi Maisha yenye mafanikio. Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (APRILI 25, 2020): [USHAURI] KAMA UMEAJIRIWA HIKI NDICHO KITAKUTOFAUTISHA NA WAFANYAKAZI WENZAKO

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine ambayo tunaamka tukiwa wazima wa afya hivyo hatuna budi kwa pamoja kusema "hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana tumshukuru na kuitumia vyema kwa ajili ya kuliishi kusudi kuu la maisha yetu. Ni siku ambayo tunatakiwa kuendeleza bidii zinazolenga kufanikisha malengo muhimu ya maisha yetu. Pia nitumie nafasi hii kuwatakia mfungo mwema wenzetu wa Dini ya Kiislamu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha jinsi unavyoweza kujitofautisha na wafanyakazi wenzako kama umeajiriwa. Ushauri huu pia unafaa kwa mtu yeyote ambaye amejiajiri hila anataka kujitofautisha na wapinzani wake wa kibiashara.

✍🏾Kupitia neno la leo naomba utambue kuwa kitakachokutofautisha na wafanyaka wenzako ni YALE UNAYOFANYA KWENYE MUDA WA ZIADA. Ikiwa umeajiriwa na wafanyakazi wenzao ambao mnalipwa kiwango sawa cha mshahara na malupulupu ili ujitofautishe nao ni lazima ubuni vitu vya kufanya kwenye muda wa ziada.

✍🏾Vivyo hivyo kama umejiajiri kitakachokutofautisha na wapinzani wako wa kibiashara ni namna unavyotumia muda wako wa ziada. Mfano, kama imezoeleka kwa wafanyabiashara wengi kufungua biashara zao muda wa saa mbili na kufunga saa kumi na mbili wewe jitofautishe kwa kufungua saa moja asubuhi na kufunga saa moja jioni. Kwa kufanya hivyo utakuwa umejiongezea masaa mawili kwenye muda wako wa kazi jambo ambalo tayari linakutofautisha na wafanyabiashara wenzako.

✍🏾Tukirudi kwa waajiriwa, wengi huwa wanatumia muda wao wa ziada kufanya mambo yasiyo na tija kwenye kipato chao. Mfano, wafanyakazi walio wengi muda wa kufika kazini huwa ni saa moja na nusu na kuondoka ni saa tisa na nusu. Ili ujitofautishe na wenzako unatakiwa kuianza siku kwa kuamka asubuhi na mapema kama vile saa kumi na mbili. Katika muda huo wa asubuhi unaweza kuutumia kufanya mazoezi, kuomba, kusoma kitabu au kuandika makala. Pia, baada ya muda wako wa kazi badala ya kurudi nyumbani na kuangalia TV au kuzurura mitaani unatakiwa kubuni miradi ya kukuingizia kipato. Miradi hiyo utaisimamia baada ya muda wa kazi na siku za mapumziko ya kazi.

✍🏾Mwanamashahiri maarufu William Shakespeare aliwahi kuandika "those men you see at high heights, they achieved those heights when their companion were asleep". Kwa tafsiri ya kiswahili ni "wale watu wanaoonekana kuwa katika kiwango cha mafanikio, walifikia mafanikio hayo wakati wenzao walikuwa wamelala". Hivyo silaha pekee ya kukutofautisha na wenzako ni jinsi gani unatumia muda wako wa ziada.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa kama tunahitaji kujitofautisha na wenzetu kwa maana ya kufanikiwa kimaisha ni lazima tuwe tayari kufanya shughuli za ziada. Jiulize shughuli zipi za au unaweza kufanya nini ambacho kitakutoufatisha na wenzako. Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (APRILI 24, 2020): [USHUHUDA] HIVI NDIVYO NILIWEZA KUJILIPA LAKI TISA NA THEMANINI NDANI YA MIEZI MITANO

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine ambayo tumezawadiwa siku mpya katika maisha yetu. Jambo la kwanza kila mmoja wetu kwa muda wake na aseme hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana tumshukuru na kuitumia vyema kwa ajili ya kuliishi kusudi kubwa la maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la leo ambapo nitakushirikisha jinsi ambavyo niliianza tabia mpya KUJILIPA KWANZA katika safari yangu ya kuelekea kwenye UTAJIRI wa ndoto zangu. Kabla ya kukushirikisha ushuhuda huo kwanza niweke wazi kuwa watu tulio wengi tunakosa dhamira ya kutekeleza yale tunayojifunza katika maisha yetu ya kila siku. Mara nyingi tunapojifunza maarifa mapya tunakuwa na tabia mbaya ya kujiuliza maswali yanayolenga kukosoa kile tunachojifunza kwa wakati huo.

✍🏾Binafsi nilikuwa kati ya watu ambao walikuwa na tabia hiyo ya kujifunza maarifa mapya na kujihoji juu ya uhalali wa hayo ninayojifunza. Matokeo yake nilijikuta najifunza maarifa mengi kuhusu maisha lakini kati ya yote hayo niliyojifunza hakuna ambacho nilikuwa natekeleza katika maisha yangu ya kila siku. Matokeo yake ni kwamba maarifa niliyokuwa najifunza yalikuwa hayanisaidii kubadilisha chochote katika maisha yangu.

✍🏾Kwa mara ya kwanza kujifunza kuhusu KUJILIPA KWANZA ilikuwa mwaka 2015 katika kitabu cha Robert Kiyosaki cha Rich Dad Poor Dad. Kitabu hiki kilinifunulia mambo mengi kuhusu maisha yenye Uhuru wa kifedha kiasi ambacho nilijutia kwa nini sikupata kitabu hicho miaka kama minne nyuma. Hata hivyo baada ya kusoma kitabu hicho sikuweka mkakati wowote wa kutekeleza kwa vitendo yale niliyojifunza.

✍🏾Mwaka 2016 mwezi wa 6 ndipo nikakutana na makala moja ya Dkt. Amani Makirita ambaye pia ni moja wa mentors wangu ambayo ilikuwa na kichwa cha habari "Jinsi unavyoweza kuwa tajiri kwa shilingi elfu moja". Katika makala hiyo alieleza namna ambavyo unaweza KUJILIPA shilingi elfu moja kila siku na matoke ya fedha hiyo baada ya kipindi flani cha muda.

✍🏾Safari hii niliweka mkakati wa kuanza KUJILIPA KWANZA sambamba nakuwa moja wa wanafunzi wake ambapo ada ya kujiunga na kundi hili ilikuwa Tshs 50,000/ kwa mwaka. Baada ya kujiunga kwenye mafunzo yake mkakati mwingine ulikuwa ni kuhakikisha ndani ya kipindi cha mwaka mmoja niwe nimejilipa laki tano na sitini (560,000/=).

✍🏾Ili kufanikisha lengo hilo nilifungua akaunti maalum ya kuwekeza pesa hiyo kwenye mfuko wa Uwekezaji wa Umoja (Umoja fund) ambao ni moja ya mifuko ya uwekezaji wa UTT Amis. Baada ya akaunti hiyo kufunguliwa nikahakikisha kila asilimia 10 ya kila pesa iliyoingia mikononi mwangu niliiweka kwenye akaunti hiyo ya uwekezaji. Kilichonishangaza ni kwamba ndani ya miezi mitano nilijikuta nimefikisha 980,000/= wakati lengo langu lilikuwa laki tano na sitini katika kipindi cha miezi 12.

✍🏾 Toka hapo ndipo nikagundua umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo maarifa ninayojifunza. Nimeendeleza muujiza huo wa KUJILIPA KWANZA kwanza kwenye kila shilingi inayoingia mkononi mwangu hali ambayo imeniwezesha kukusanya mtaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye mashamba, viwanja na ufugaji. Hakika KUJILIPA KWANZA kuna kitu ndani yake ambacho kwa haraka haraka kabla ya kuanza kuishi kanuni hii hauwezi kukiona.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha umuhimu wa kuishi kwa vitendo maarifa tunayojifunza kila siku. Wajibu upo mkononi mwako kutekeleza haya unayojifunza ili ubadilishe maisha yako. Kwa ni mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (APRILI 19, 2020): HIVI NDIVYO ASILI (NATURE) INAVYOTUZAWADIA KULINGANA NA MATENDO YETU

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii zinazolenga kuboresha kila sekta ya Maisha. Wote kwa pamoja tuseme asanthe kwa Muumba wetu kutokana na baraka ambazo anazidi kutujalia katika Maisha yetu ya kila siku. Pia, tuendelee kuunganisha nguvu kama taifa kumuomba Mungu atuepushe na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha moja ya sheria ya asili ambayo inaendelea kuutawala ulimwengu. Sheria hii imekuwepo toka enzi za kuumbwa kwa ulimwengu na inaendelea kufanya kazi hata katika kizazi cha sasa. Sheria hii si nyingine bali ni: sheria ya kupanda na kuvuna (the natural law of sow and reap). Kwa maneno mengine sheria hii ni sawa na kusema kuwa tunaishi katika ulimwengu wa KISABABISHI (cause) na ATHARI/MATOKEO (effects). Kwa ujumla ulimwengu upo jinsi ulivyo kutokana na matendo yetu.

✍🏾Mwandishi Anthony Robins aliwahi kuandika kuwa ulimwengu jinsi ulivyo ni matokeo ya matendo yetu. Kwa lugha nyingine hatutakiwi kuuona ulimwengu katika sura ya tofauti bali tunatakiwa tufahamu kuwa sisi ndiyo tunaweza kuubadilisha ulimwengu na kuuweka katika sura tunayoitaka. Hapa ndipo kila mmoja anatakiwa kutambua kuwa matokeo anayopata yanatokana na fikra na mitazamo aliyonayo kuhusu ulimwengu.

✍🏾Ukiwa na fikra kwamba ulimwengu ni sehemu hatarishi na hisiyo rafiki kufanikisha chochote hakika utaendelea kuzunguka huku na kule bila kufanikisha chochote katika maisha. Matokeo yake utaanza kujiona mtu hasiye na bahati. Hivyo, jambo la kwanza unalotakiwa kufahamu kupitia neno la tafakari ya leo kuwa “matukio yote yanayotokea katika Maisha yetu iwe ni kwenye afya, uchumi, kiroho, kikazi, mahusiano au kijamii ni matokeo ya matendo au uwekezaji tunaoufanya kila siku”.

✍🏾Baada ya kutambua nguvu ya sheria hii ndipo kila mmoja wetu anatakiwa afahamu kuwa kila ya mafanikio anayoyataka yanaanzia ndani mwake. Ni lazima kwanza abadilishe tabia ili ziendane na mafanikio anayotamani kuyaona katika Maisha yake. Hii ni sawa na aliyekuwa Rais wa nne wa Marekani James Madison alivyowahi kunukuliwa kuwa “ni lazima uishi mabadiliko unayoyataka yatokee (be the changes you want to see)”.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa kila tunachokiona katika Maisha yetu ni matokeo ya uwekezaji wetu. Hivyo, chochote tunachotamani kufanikisha katika Maisha yetu ni lazima tujiulize tunatakiwa kuwekeza nini kwa sasa ambacho kitatupatia matokeo tunayotamani. Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (APRILI 18, 2020): HIVI NDIVYO UNAWEZA KUIFANYA KAZI HII IWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Naanza kwa kumshukuru Mungu kutokana na upendo wake ambao umeniwezesha hata asuhuhi hii ya leo nina nguvu na hamasa ya kukufikishia ujumbe wa tafakari hii ya leo. Zaidi ya yote namshukuru Mungu kutokana na uwepo katika kundi hili maana hilo ndilo kusudi na tegemeo la kazi ninayoifanya ambapo faraja yangu ni kuona kazi hii inawafikia vijana wengi. Pia, naungana na umati wa Watanzania wenzangu katika kuomba toba ili Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atunusuru na janga la ugonjwa wa mlipuko wa Covid 19.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha njia muhimu unayotakiwa kufanya kwa ajili ya kuhakikisha kazi ninayoifanya inaendelea kukufikia pamoja na kuifikia jamii ya vijana wengi zaidi. Lengo letu kubwa ambalo nimekuwa nikisisitiza ni kuona kwa pamoja tunaibadilisha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi na lengo hilo linaanzia kwenye Maisha ya kila mmoja wetu. Ili lengo hili litimizwe ni lazima fikra za vijana zibadilishwe kupitia kwa watu wanaothubutu kufikisha elimu ya mafanikio kwenye makundi mbalimbali ya jamiii kwa kutumia mbinu mbalimbali.

✍🏾Nilianza kazi hii toka mwaka 2016 ambapo nilifungua blog na fikrazakitajiri.blospot.com ambapo nilijikita kwenye kuishirikisha jamii maarifa mbalimbali kwa mfumo wa uchambuzi wa vitabu. Nilianza na hili la uchambuzi wa vitabu kwa kuwa nililenga kurahisisha usomaji wa vitabu kwa kuwa watu wengi ukiwauliza kwa nini hawajisomei vitabu watakujibu kuwa hawana muda wa kusoma kitabu ukurasa kwa ukurasa mwanzo mwisho. Pia, wengine watakuambia vitabu vingi vinavyopatikana kwa urahisi vimeandikwa kwa lugha ya kingereza ambayo siyo rafiki kwa watu wote kusoma kwa wepesi na kutafsiri wanachosoma.

✍🏾Hivyo, kutokana na sababu hizo nikaona kuna kila sababu ya kufupisha (summarize) vitabu vya mafanikio mbalimbali kwa lugha rahisi na kuishirikisha jamii kupitia mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI. Wakati naanzisha blog hiyo wafuasi (followers) kwa siku walikuwa kati ya 10 hadi 15 ambao walikuwa wametawanyika sehemu mbalimbali za Dunia. Kadri siku zilivyosogea ndivyo watembeleaji wa blog walivyozidi kuongezeka na hali hiyo ikapelekea wale wanaojiunga na mfumo wa kupokea barua pepe za uchambuzi wa vitabu kuendelea kuongezeka.

✍🏾Hali hii ilinifanya niendelee kufanya kile ambacho nilikuwa nafanya hata kama kuna nyakati nilijikuta naanza kukata tamaa hasa kutokana na utamaduni wa Watanzania wengi kutopenda kujisomea vitabu. Ili kuhakikisha kuwa kazi hii inaendelea kuwafikia wengi ndipo mwaka huu 2020 nikaona ni vyema nianzishe kundi la WhatsApp ambalo litawezesha kuendelea kukusanya vijana wengi na kuwapatia elimu inayolenga kubadilisha fikra zao. Hii ni kutokana ukweli kwamba mafanikio ya aina ya yoyote yanaanzia kwenye kubadilisha fikra za mhusika. Namshukuru Mungu kuwa kundi hili lilianzishwa likiwa na watu wasiozidi 15 lakini kuna watu zaidi ya 90. Mungu ni mwema maana kila siku naona kuwa kazi ninayoifanya ina uhitaji mkubwa kwa vijana waliowengi.

✍🏾Mafanikio yote hayo yananilazimisha kuhakikisha kila mara naendelea kuboresha kazi hii ili iendane na kasi ya ukuaji wa teknolojia. Ili kuendana na kasi hiyo ya ukuaji wa teknolojia hakuna namna zaidi ya kuendelea kuwekeza kwenye muda, nguvu, maarifa na rasilimali fedha ambavyo vyote kwa pamoja vinajikita kwenye kuiboresha kazi hii. Katika kufanikisha hilo nimekuwa kila mara najifunza kutona na usomaji wa vitabu au Makala mbalimbali kwenye mitandao sambamba na kuwa na ‘mentors’ watatu wawili wakiwa ni Watanzania na mmoja yupo nje ya nchi. Kwa mwaka natumia zaidi ya laki tano kwa ajili ya kuendelea kujifunza kutoka kwa mentors hawa lengo ni kuona natimiza lile lengo kuu la kazi hii.

✍🏾 Katika kipindi chote cha kazi hii nimejikita kwenye kutoa huduma kwa jamii kuliko kutanguliza pesa. Hivyo, kupitia Makala hii ombi langu kwako ni kuendelea kunisapoti hasa katika kununua uchambuzi wa vitabu mbalimbali ninavyokushirikisha sambamba na kushiriki kwenye semina ambazo nitakuwa naandaa. Gharama unazotakiwa kulipia kwa ajili ya kupata uchambuzi wa vitabu pamoja na kushiriki semina ni ndogo mno ikilinganishwa na kile mafunzo unayoyapata. Kupitia uchambuzi wa vitabu na semina hizo, mimi sifaidiki chochote zaidi ya kuwekeza kwenye kuiboresha kazi hii ili hatimaye iwafikie vijana wengi.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nimekushirikisha safari ambayo nimepitia na ile ambayo naendelea kuipitia hadi kuniona jinsi nilivyo kwa sasa. Tafsiri yake ni kwamba jinsi nilivyo kwa sasa siyo kitu cha bahati bali ni kitu ambacho ninakiishi kila siku. Hata hivyo, safari ya kufikia lengo kuu la kuielimisha jamii kupitia kazi zangu bado ni ndefu na ndiyo maana nimekuomba kwa njia moja au nyingine tushirikiane kwa pamoja kufikia lengo hilo. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

UJUMBE MAALUM KWA WANAFAMILIA WOTE WA FIKRA ZA KITAJIRI👇🏾👇🏾

👉🏿Poleni na majukumu ya siku ya leo wanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Ujumbe huu ni muhimu kwako kama unahitaji kuishi maisha ya ndoto yako.

✍🏾Tarehe moja mwezi huu kupitia neno la tafakari nilitoa mwelekeo wa ratiba ya mwezi huu ambapo nilisema mwishoni mwa mwezi huu kuna semina naiandaa ambayo itafundishwa kwa njia ya mtandao kupitia kundi maalum la WhatsApp.

✍🏾Baada ya kupokea mrejesho kutoka kwa baadhi yenu. Nimeandaa mada kuu ya semina hii ambayo itaenda kwa jina la JILIPE KWANZA~ NJIA YANGU YA UTAJIRI. Kupitia Semina hii utajifunza mada zifuatazo:-

✍🏾 1. JILIPE KWANZA
Ndani ya mada hii, mada ndogo zitakazofundishwa ni:-
👉🏿Nini maana ya KUJILIPA KWANZA.
👉🏿Nguvu iliyopo katika KUJILIPA KWANZA
👉🏿Kwa nini watu wanashindwa KUJILIPA KWANZA
👉🏿Hitimisho

2. SEHEMU SAHIHI YA KUWEKEZA PESA UNAYOJILIPA
Katika mada hii tutajifunza mada ndogo zifuatazo:-
👉🏿Utangulizi
👉🏿Sehemu zipi ni salama kuwekeza pesa UNAYOJILIPA. Hapa tutangalia sehemu hizi:
✍🏾Njia ya kienyeji
✍🏾Akaunti maalumu za benki
✍🏾Mifuko ya uwekezaji ya UTT
✍🏾Hisa za makampuni mengine katika Soko la hisa (DSA)
✍🏾Hatifungani/Dhamana za Serikali
👉🏿Hitimisho ambapo ntazungumzia sehemu ipi zaidi nakushauri kuwekeza pesa zako.

👉🏿 3. IFAHAMU MIFUKO YA UWEKEZAJI YA UTT
Katika mada hii tutajifunza mada ndogo zifuatazo:-
✍🏾Maana ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja wa UTT
✍🏾Aina ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja iliyopo
✍🏾Jinsi ya kufungua akaunti ya UTT
✍🏾Faida za kuwekeza kwenye mifuko ya UTT
✍🏾Mifuko ipi ambayo nakushauri uwekeze pesa yako
✍🏾Hitimisho

UTARATIBU WA KUSHIRIKI SEMINA HII
Gharama ya semina hii ni TSHS 10,000/=. Ofa! Kama humu ndani tutashiriki semina hii angalau watu 70, gharama itapungua badala ya ada hiyo sasa itakuwa TSHS. 7000/=. Pia utakapojiunga na semina hii utapewa Ofa ya Uchambuzi wa Kitabu cha Dkt. Reginald Mengi cha I Can I Must I Will.

 👉🏿👉🏿Kwa sasa unatakiwa kufanya nini? Unachotakiwa kufanya kwa sasa nikusema hapa chini neno moja NITASHIRIKI

💪🏾💪🏾💪🏾💪🏾Kwa pamoja twende na kauli mbiu ya ## I can't plan to miss this turning point##

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

 Mwalimu Augustine Mathias
Mobile: +255786 881 155/+255763 745 451/+255629 078 410
Blog: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (APRILI 17, 2020): [SIRI] FAHAMU KWA NINI BIASHARA NYINGI HUWA ZINAKUFA KATIKA KIPINDI CHA AWALI TOKA ZIANZISHWE

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama. Tumia dakika kadhaa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyokupa katika Maisha yako. Pia, muda huo wa muunganiko na Mungu hakikisha unamuomba akulinde uwe salama katika siku hii ya leo kwenye kila hatua utakayopiga.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha kwa nini biashara nyingi huwa hazidumu katika kipindi cha awali toka zinapoanzishwa. Tafiti zinaonesha kuwa tafiti zinaonesha kuwa asilimia 96 ya biashara zote huwa zinakufa kabla ya kutimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake. Kati ya hizo, takribani asilimia 80 huwa zinakufa ndani ya miaka miwili toka kuanzishwa kwake. Hata hivyo, asilimia 4 ya biashara ambazo zinaweza kumudu kuendelea baada ya miaka 10 haimaanisha kuwa zinafanya vizuri katika kutengeneza faida kwa wamiliki.

✍🏾Katika kitabu chake cha Sale Like Crazy Mwandishi kijana na bilionea Sabri Suby anatushirikisha kuwa biashara nyingi zinashindwa kukua zaidi ya miaka kumi kutokana na wamiliki wa biashara hizo kushindwa kutumia mbinu sahihi za kuiendeleza biashara husika. Mbinu namba moja ni kuhakikisha biashara inajiendesha kwa faida kwa maana uwezo wa wa biashara kuendelea kuzalisha mapato.

✍🏾Kwa maneno rahisi, ili biashara iendelee kukua toka kipindi cha kuanzishwa kwake inatakiwa iendeelee kuzalisha fedha za kutosha ambazo zitawezesha uendelevu na ukuaji wa biashara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba fedha zinazozalishwa na biashara husika ndo uhai, hewa na chakula cha biashara hiyo kuendeleza uhai wake.

✍🏾Hata hivyo siri iliyopo ni kwamba, ili biashara iweweze kuendelea kuzalisha faida ni lazima iwe na mfumo unaowezesha kuendelea kupata wateja wapya kila mara pamoja na mfumo imara wa kulinda wateja waaminifu. Ukifanikiwa kuwa na mfumo imara wa kulinda wateja na kupata wateja wapya moja kwa moja mauzo yako yataendelea kukua.

✍🏾Biashara nyingi zinakufa katika kipindi cha awali toka kuanzishwa kwake kwa kuwa waanzilishi wengi wa biashara wanakuwa hawana elimu ya misingi ya bisashara. Mfano, biashara nyingi zinaanzishwa kutokana ujuzi wa mwanzilishi wa biashara katika biashara anayoanzisha. Mfano, Mpishi anaamua kuanzisha mgahawa, Mwanasheria anaanzisha Kampuni ya huduma za kisheria au daktari anaanzisha biashara ya huduma za afya. Kubwa, ni kwamba waanzilishi wote hao hawana misingi ya kuendesha biashara husika na matokeo yake ni kwamba biashara zinakufa au zinadumaa.

✍🏾Kutokana na waanzilishi wengi kushindwa kuwa na misingi sahihi ya biashara wanajikuta biashara zinakuwa ni kazi kwa mmiliki (job) badala ya kuwa sehemu ya kuzalisha fedha kwa mmiliki wakati huo huo ikimpunguzia muda wa kufanya kazi. Mfano, biashara nyingi katika jamii yetu ni zile ambazo mmiliki hawezi kutoka kwenye biashara kila siku na hivyo anakuwa ni mtumwa wa biashara husika.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumeona kuwa biashara nyingi zinakufa kutokana na waanzilishi wengi kutoka kuwa na elimu sahihi ya msingi wa biashara. Elimu hii inahusisha namna ya kulinda pesa zinazozalishwa pamoja na namna ya kukuza idadi ya wateja kwa ajili ya bidhaa zako. Elimu hii husitegemee kuipata shuleni bali ni kupitia kusoma vitabu mbalimbali ambavyo waandishi walishakurahisishia ili uvipate kwa urahisi ni suala la wewe kujibidisha kusoma vitabu hivyo. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (APRILI 15, 2020): [COVID 19] KIPINDI MUHIMU CHA KUJIFUNZA UMUHIMU WA KUBAJETI PESA ZAKO.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na hamasa ya kutosha kukuwezesha kuendeleza pale ulipoishia jana. Ni siku muhimu ambayo tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa zawadi hii ya uhai kiasi ambacho tuna nafasi ya kuendelea kuboresha Maisha yetu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu kuishi kulingana na bajeti katika kipindi hiki ambacho shughuli za uzalishaji zinakabiliwa na giza nene la ugonjwa wa mlipuko wa CORONA. Hiki ni kipindi ambacho matukio ya baadaye kwenye sekta ya uzalishaji hayatabiriki.

✍🏾Ni kipindi ambacho taharuki na hofu inatawala Maisha ya mwanadamu kwenye mazingira yanayomzunguka. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hakuna anayejua ni sehemu ipi yenye usalama kwa kutokakuwa na maambukizi katika mazingira ya uzalishaji aliyozoea.

✍🏾Moja ya kampeni ya kupambana na ugonjwa huu ni kupunguza kutembelea sehemu ambazo siyo za lazima au kwa lugha rahisi kujitahidi kubaki nyumbani kwa kadri uwezavyo. Ni kutokana na kampeni hii mwingiliano wa watu utaendelea kupungua katika maeneo mengi ya kazi na biashara na moja ya athari yake ni kushuka kwa uzalishaji au mauzo kwenye sehemu za kazi na biashara.

✍🏾Ni kipindi ambacho baadhi ya bidhaa tulizozoea katika biashara au kazi zetu zitaadimika kutokana na kufungwa kwa mipaka ya nchi mbalimbali. Kwa kifupi, Maisha yanakumbwa na giza la kutengwa katika kisiwa ambako hakuna mwingiliano wa watu.

✍🏾Tafsiri yake ni kwamba kadri mwingiliano wa watu utakavyozidi kupungua ndivyo na pato kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja litakavyozidi kupungua na hatimaye lindi la umasikini litazidi kuongozeka. Ukweli ni kwamba mzunguko wa pesa katika jamii yoyote ni matokeo ya mwingiliano mkubwa wa watu katika eneo hilo. Ndiyo maana sehemu zenye idadi kubwa ya watu ndizo senta nzuri za biashara ya kila aina.

✍🏾Tumeona kuwa kadri taharuki ya CORONA inavyozidi kuongezeka ndivyo uchumi binafsi utavyobadirika kiasi ambacho vyanzo vya mapato ulivyokuwa navyo vitapata mtikisiko. Katika kila aina mabadiliko yanayotokea dhidi yako unatakiwa kuwa na mpango ambao utakuwezesha kujihami na hatimaye ufanikiwe kuvuka salama katika kipindi hicho kigumu.

✍🏾Moja ya mabadiliko ambayo nakushirikisha kupitia neno la tafakari ya leo ni kuhakikisha unaanza kuishi kwa bajeti tena inayozingatia vitu muhimu pekee kwa sasa. Huu siyo wakati wa kutawanya pesa kidogo ulizonazo kwenye vitu visivyo na umuhimu kwa mahitaji ya familia. Wakati huu ni wa kuhakikisha unajenga Safina ambayo itaikulinda wewe na familia yako.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha umuhimu wa kuishi kwa bajeti tena inayozingatia vitu muhimu katika mahitaji ya familia katika kipindi hiki ambacho dunia inaendelea kufunikwa na giza la ugonjwa wa CORONA. Pia, nimewahi kuandika kuwa hiki ni kipindi ambacho unatakiwa kukitumia kujifunza tabia nzuri na kuachana na tabia ambazo zilikuwa zinakufanya upoteze pesa nyingi. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

NENO LA LEO (APRILI 14, 2020): [USHAURI] JE PESA ZAKO HUWA ZINAPITILIZA NA HAUJUI ZINAKOENDA? TUMIA MBINU HII.

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umemaliza vyema siku za pasaka na sasa una uhuisho mpya kwa ajili ya kuendeleza kile unachofanya. Kumbuka nimekuwa nakusisitiza kuhakikisha kila siku unatengeneza ushindi mdogo mdogo maana ni kupitia ushindi huo ipo siku watu watashangaa mafanikio makubwa uliyonayo bila kujua kuwa wanachokiona kimeandaliwa kwa muda mrefu.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha mbinu moja ambayo unatakiwa kuitumia kwa ajili ya kujua sehemu ambazo huwa zinavujisha pesa zako. Katika jamii tunayoishi ni kawaida kusikia watu wakilalamika kuwa kila wakishika pesa zinapitiliza na hawajui zinakoelekea. Wengi ni rahisi kukumbuka kiasi cha pesa ambacho walikuwa nacho lakini hawawezi kukumbuka pesa hiyo imeshaje kwa maana namna ilivyotumika.

✍🏾Kama na wewe ni mmoja wa hao ambao huwa hawajui pesa zao zinaenda wapi, kupitia neno la tafakari ya leo nakushirikisha mbinu ambayo itakuwezesha kujua sehemu ambazo pesa yako huwa inaelekea. Mbinu hii si nyingine bali kuanzia sasa tafuta kijinotibuku kidogo na yake hakikisha unaandika kila pesa unayopata na kila aina ya matumizi unayofanya. Andika kila kiasi cha pesa kinachotumika bila kujali ni kidogo au kikubwa.

✍🏾Ndiyo namaanisha kila aina ya matumizi yanayohusisha pesa yako hakikisha yamerekodiwa kwenye kijitabu chako. Kama umekunywa chai hotelini rekodi chai hiyo umelipia shilingi ngapi. Kama umekunywa maji na soda rekodi gharama hiyo ya vinjwaji kwa kuainisha gharama ya kila aina ya kinywaji ulichotumia. Kama umenunua vocha au kujiunga kifurushi kwa mpesa au tigo pesa hakikisha unaandika kiwango ulichotumia kwenye muamala huo. Vivyo hivyo, kama kuna pesa umeitenga kama akiba au kuiwekeza hakikisha na yenyewe inarekodiwa.

✍🏾Fanya zoezi hila ndani ya mwezi wa kwanza na mwisho wa mwezi jumlisha matumizi yako ili kujua kama kiasi ulichoandika kinaleta jumla ya kiasi cha pesa ulichopata katika mwezi husika. Baada ya mwezi wa kwanza endelea na utaratibu huu kwa kipindi cha miezi kadhaa hadi pale ambapo utakuwa umejua sehemu ambako pesa yako huwa inaelekea.

✍🏾Kwa nini zoezi hili? Zoezi hili pamoja na kukusaidia kujua sehemu ambako pesa yako huwa inaelekea litakusaidia kugundua baadhi ya matumizi ya pesa ambayo siyo ya lazima. Baada ya kugundua sehemu zisizo za lazima ambazo zinavujisha pesa yako sasa unatakiwa kuandaa bajeti inayoendana na pato lako. Pia, kupitia zoezi hili utaweza kugundua sehemu zipi unaweza kuokoa pesa ambayo umekuwa ukiipoteza kwenye matumizi yasiyo ya lazima na sasa pesa hiyo unaweza kuiwekeza sehemu yenye tija.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetufunulia kuwa tumekuwa tukipata pesa na mwisho wake hatujui inakoelekea kwa vile hatuna utaratibu wa kuorodhesha matumizi ya pesa yetu. Kuanzia sasa tumeshauriwa kuhakikisha tunakuwa na kijitabu kidogo ambacho ndani yake tutaorodhesha matumizi ya pesa yote na hatimaye kujua kiasi tunachotumia ndani ya muda wa mwezi mmoja. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

Mwendelezo wa chambuzi wa Kitabu cha How to Stop Worrying and Start Living: Jinsi ya kuepuka hofu katika maisha.

Habari rafiki yangu ambaye umeendelea kuamini kazi yangu ya uchambuzi wa vitabu kupitia mtandao wa FIKRA ZA KITAJIRI. Karibu katika uchambuzi wa kitabu cha leo ambacho ni 4 kati ya vitabu 30 ambavyo nimejiwekea lengo kuvisoma katika kipindi cha mwaka huu 2020. 

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku pamoja na kujumuika na watu wenye mtazamo sawa, tafadhali fanya hivyo KWA KUBONYEZA HAPA na kujiunga na kundi letu. Nafasi ni chache hivyo fanya maamuzi ya kujiunga sasa.

Kupitia makala hii nakushirikisha sehemu iliyobakia ya uchambuzi wa kitabu How to Stop Worrying and Start Living” kutoka kwa mwandishi Dale Carnegie.

Unaweza kusoma sehemu ya kwanza ya uchambuzi wa kitabu hiki kwa kubofya kiunganisho hiki hapa chini.



SEHEMU YA TANO: KANUNI YA KIPEKEE KATIKA KUISHINDA HOFU

21. Kuishi maandiko matakatifu ni moja ya njia rahisi ya kuepukana hofu. Maisha ya wanadamu walio wengi yanatawaliwa na hofu inayotokana na gharama za mahitaji ya kila siku. Mtu mzima yoyote kila anapoamka anawaza atapata vipi hela kwa ajili ya chakula cha familia, ada za Watoto wa shule, mahitaji ya maradhi, afya, bili za maji na umeme na mengine mengi. Ni kutokana na mahitaji hayo wapo watu wengi ambao wanakata tamaa kiasi cha kutaka kujinyonga ili kuepuka ghadhabu/kalaa ya Maisha. Hata hivyo, kupitia maandiko matakatifu kila mmoja kwa Imani yake ni sehemu ambapo mtu anapata faraja, uvumilivu na tumaini la Maisha. Maisha ya mwanadamu yanazungukwa na mafumbo mbalimbali ambayo yanamfanya kila mara ahofie Maisha yake ya baadaye. Hata hivyo, kupitia misingi ya dini kila mwanadamu anaweza kuishi Maisha yenye thamani.

22. Maisha bila misingi ya Imani hayana maana. Imani imeweka misingi muhimu katika Maisha ya mwanadamu. Misingi hii inamfundisha mwanadamu namna anavyotakuwa kuishi katika mazingira yake. Ni kutokana na misingi ya Dini, Maisha ya mwenye Imani yanakamilika pale ambapo anayatoa Maisha yake kwa ajili ya watu wengine au viumbe vingine kwa ujumla wake. Hebu fikiria kama kusingekuwa na jinsi ambavyo maovu yanayoambatana na mauaji, wizi, ugomvi, fitina na mengine mengi ambavyo yangeshamiri katika ulimwengu huu. Dini imekuwepo kwa ajili ya mwanadamu kuishi Maisha yenye upendo na amani, ni kupitia dini hiyo mwanadamu kila mara anatakiwa kuishi kwa ukamilifu badala ya kuishi Maisha ya hofu. Ieleweke kuwa kinachomfanya mtu kuwa mtu wa Dini siyo tu kwenda Kanisani au Msikitini bali ni ile hali ya kuwa na Roho sambamba na kushiriki matendo mema kwenye Maisha ya kila siku. Kwa ujumla Imani ni moja nguvu za ulimwengu huu ambazo zinamwezesha mwanadamu aishi Maisha yenye amani, furaha na tumaini.

23. Kuna nguvu kubwa katika muunganiko wa mwanadamu na Mungu. Muunganiko huu unakamilika kupitia sara ambapo mwanadamu anamlilia Muumba wake dhidi ya matatizo yanayomkabili pamoja na kushukuru baraka anazojaliwa. Mwandishi anatushirikisha kuwa tatizo lililopo kwa wanadamu wengi ni kusubiria nyakati za tabu na shida ndipo wamkumbuke Muumba wao. Hakika kwa mwanadamu ambaye anaishi katika sara kila siku hana cha kuhofia katika Maisha kwa kuwa matatizo na furaha yake yote kila mara anajua kuna Mungu mwenye nguvu dhidi ya matatizo aliyonayo. Ni kupitia muunganiko huu nguvu na hamasa mpya inajitokeza kwa mtu anayeishi Maisha ya sara. Hivyo, kila mara anauhuishwa kupitia sara. Kumbe katika Maisha yetu ya kila tunatakiwa kukumbuka maandiko matakatifu yanatuambia kuwa: “Omba na utapewa; tafuta na utapata; na bisha hodi na utafunguliwa”.

SEHEMU YA SITA: JINSI YA KUEPUKANA NA HOFU YA KUKOSOLEWA

24. Watu wengi wana hofu inayotokana na kutojiamini kutokana na majukumu waliyonayo. Wengi kutokana na kiwango cha elimu au uzoefu walionao wanajikuta kwenye hali ya kudhania kuwa kazi walizonazo ni viatu ambavyo vinawapwaya. Hauwezi kuzuia watu wakubeze katika kila unachofanya hila unaweza kuhakikisha katika kila wanalobeza unawajibu kwa matokeo chanya. Kanuni kubwa unayotakiwa kuiishi ni: Mti wenye matunda ndiyo unapigwa mawe. Kadri utakavyoendelea kutoa matokeo chanya katika kazi unayoifanya ndivyo maadui wasiyokutakia mema watazidi kuongezeka. Ndivyo mwanadamu alivyo maana wivu ni moja ya tabia za asili walizonazo wanadamu. Wajibu ulionao siyo kupambana nao bali ni kuendelea kuishi misingi ya kanuni ulizojiwekea kuhusu Maisha yako na kazi unayoifanya.

25. Kanuni ya kuepuka hofu inayotokana na kukataliwa ni: kutambua kuwa hakuna mtu anayejali Maisha yako maana kila mtu yuko bize na Maisha yake. Kwa kutambua kanuni hiyo unatakiwa kuwa bize na majukumu yako ya kila siku katika Maisha na kuacha kuumizwa au kutumia muda mwingi kufikiria maneno ya watu wanaokubeza au kukukosoa. Fanya yale unayoamini ni sahihi kutoka ndani ya roho yako kwani hata ukifanya kulingana na mapenzi yao bado utakosolewa tu. Kumbuka hauwezi kuridhisha watu wote na ndiyo maana hata Yesu mwenyewe alisalitiwa na mmoja wa Mitume wake. Hivyo kwa kutambua ukweli huu kuhusu mwanadamu, hautakiwi kuishi kwa ajili ya kufurahisha wanaokuzunguka bali ishi kutimiza yale unayoamini ni sahihi na kujifanya kana kwamba hausikii maneno ya wakosoaji wasiyo na dhamira njema juu ya matendo yako. Hata hivyo, unatakiwa kutambua kuwa unaweza kujifunza kutokana na kukosolewa pale unapokosolewa kwa haki.

26. Njia nyingine ya kukabiliana na hofu ya kukosolewa ni kutenga muda wa kujifanyia tathimini dhidi ya matendo yako ya kila siku. Kila siku au kila mwisho wa wiki tenga muda kwa ajili ya kujiuliza ni makosa yapi umefanya katika kipindi cha wiki nzima ikilinganishwa na yale uliyotenda kwa usahihi. Jiulize makosa hayo yalisababishwa na nini na unaweza kufanya nini ili uhepukane na makosa hayo katika Maisha ya sasa na baadaye. Jiulize katika makosa hayo kuna uzofu upi ambao ni muhimu katika Maisha yako. Tafsiri yake ni kwamba katika yale unayokosolewa kwa haki kuna somo kubwa ambalo unatakiwa kujifunza kwa ajili ya kusonga mbele kwa mafanikio zaidi. Kumbe, kabla kusubiria maadui zetu kutukosoa tunaweza kujikosoa wenyewe kutokana na kufanya tathimini ya mara kwa mara kuhusiana na matendo tunayofanya katika majukumu ya kila siku.

27. Wakati mwingine ni muhimu kukaribisha wanaokukosoa kwa ajili ya kujifunza somo muhimu katika Maisha. Unapokuwa katika ngazi ya kufanya maamuzi ambayo yana athari kwa kundi kubwa la watu ni lazima uwe tayari kupokea wakosoaji na kupokea ushauri kutoka kwa watu wa karibu na wewe. Hakuna anayependa kukosolewa kutokana na ukweli kwamba mwanadamu anatawaliwa na hisia (feelings) kuliko mantiki (logic). Kumbe, kama unahitaji kujifunza kutoka kwa wakosoaji wako unatakiwa maamuzi yako fanyike kwa kutumia mantiki kuliko kuongozwa na hisia binafsi. Kama nguli wa sayansi Albert Einsten aliwahi kunukuliwa kuwa “wakati mwingine hayuko sahihi kwa asilimia 99” ndivyo na wewe unatakiwa kutambua pengine maamuzi unayoona ni sahihi ni kutokana na hisia zako binafsi.

SEHEMU YA SABA: NJIA 6 ZITAKAZOKUWEZESHA KUEPUKANA NA UCHOVU NA KUKUFANYA UWE NA NGUVU YA MWILI NA ROHO

28. Uchovu ni moja ya sababu zinazopelekea hofu katika Maisha. Ni kutokana na ukweli huo mwandishi kupitia sehemu anatushirikisha mbinu muhimu za kukabilianana na uchovu. Kutokana na tafiti za kitabibu, uchovu unapunguza uwezo wa mwili kukabiliana na homa ya kawaida pamoja na magonjwa mbalimbali. Pia, kulingana na tafiti za matibabu ya akili, uchovu hupunguza uwezo wa kukabiliana na hisia za hofu na wasiwasi. Hivyo, kutokana na tafiti hizo kuna kila sababu ya kufahamu namna ya kukabiliana na uchovu kama sehemu ya kukabiliana na hofu katika Maisha ya kila siku. Hivyo, kupata muda wa kupumzika ni moja ya njia ya kuepukana na wasiwasi au hofu; kanuni ni kwamba ili upunguze hofu hakikisha: unapata muda wa kupumzika mara kwa mara na pumzika kabla ya kuchoka. Tenga muda wa dakika kadhaa katika siku yako kwa ajili ya kutuliza kichwa kutoka majukumu yote ya siku. Muda wa kupumzika ni muhimu kwa ajili ya kuhuisha nguvu mpya kabla ya kuendelea na majukumu yaliyopo mbele yako. Muda unaotumia kupumzika siyo kwamba unaupoteza bali ni muda muhimu kwa ajili ya afya ya roho na mwili.  

29. Je uchovu unasababishwa na nini? Mwandishi anatushirikisha kuwa tafiti zinaonesha kuwa kuwa kazi inayohusisha ubongo/akili haiwezi kusababisha uchovu kwa mhusika. Kinachosababisha uchovu ni mtazamo au mazoea ya akili pamoja na hisia. Kwa tafsiri ya haraka ni kwamba kinachosababisha uchovu ni sababu za kisaikolojia ambazo mhusika anapambana nazo kwenye Maisha yake ya kila siku. Tafiti zinaendelea kuonesha kuwa hisia zinazopelekea uchovu ni zile hasi ambazo zinaambatana na mhusika kuwa na: chuki, kuhisi kutothaminiwa katika kazi yake, wasiwasi wa kutokamilisha kazi kwa wakati, na hofu kutofanya kazi kwa haraka. Matokeo yake ni kupelekea mhusika kupunguza uzalishaji kwenye kazi yake na hatimaye kurudi nyumbani na maumivu ya kichwa akidhani kuwa ni uchovu kumbe uchovu ameuzalisha mwenyewe bila kujua. Kumbe, njia rahisi ya kuepukana na uchovu ni kuwa na utulivu wa akili kwenye jukumu lililopo mbele yetu. Utulivu huu unapelekea neva za mwili (nerveous) kujihisi vyema na hivyo kutoa ushirikiano kwa akili katika kazi inayofanyika.

30. Hofu au wasiwasi kuhusu masuala ya familia ni moja ya chanzo kikuu cha magonjwa mengi kwa wanawake walioolewa au wenye familia kwa ujumla katika karne ya sasa. Magonjwa mengi kama vile magonjwa ya moyo, kansa ya uzazi, kansa ya ziwa, tumbo na magonjwa ya figo ni matokeo ya wasiwasi na hofu kubwa waliyonayo wanawake wengi juu masuala ya familia. Hali hii inatokana na uchovu ambao unasababishwa na majukumu ya familia kwa akina mama. Ndiyo maana ukienda kwenye mikusanyiko ya kidini wanaojazana ni akina mama ikilinganishwa na wababa kwa vile wanategemea kupitia mikusanyiko hiyo wapata suluhisho la matatizo yao. Mwandishi anatushirikisha kuwa matatizo mengi yanayowakabili akina mama huwa yanatibika pale wanapopata ushauri wa wataalamu wa magonjwa ya saikolojia. Pia, mwandishi anatushirikisha kuwa akina mama wengi wanateseka na masuala ya familia kwani kwa asili wana tabia ya kutokutoa vitu ndani. Ni kutokana na tatizo hilo, tafiti zinaonesha kuwa wapo wengi ambao wamepona matatizo yao kutokana na tiba ya maneno tu. Hivyo, ni muhimu kujenga tabia ya kutoa vitu ndani, pale unajihisi kusongwa na mambo tafuta mtu ambaye unamwamini kwa ajili ya kukupa ushauri juu ya kile ambacho kinakutatiza.

31. Kila mwanamke anaweza kupunguza hofu au wasiwasi juu ya masuala ya kifamilia kwa kutumia mbinu zifuatazo:-
ü  Kuwa na kijinotibuku ambacho unatembea nacho kila sehemu – Ndani ya kijinotibuku hicho hakikisha unaweka vitu vya muhimu ambavyo vinakufanya ujihisi tulizo la moyo. Mfano, unaweza kuweka nukuu kutoka kwenye misitari muhimu ya maandiko matakatifu, unaweza kuweka vesi za nyimbo au mashairi ambayo huwa ukiimba unajisikia faraja ndani ya nafsi yako.
ü  Husitumie muda mwingi kwenye mapungufu ya wengine – Tambua kuwa mme wako ni binadamu na ana mapungufu mengi maana kama angekuwa malaika msingeweza kuoana. Mara zote jaribu kutafuta mazuri ya watu unaoishi nao na ujikite kwenye mazuri yao kuliko maovu waliyonayo. Hii itakusaidia kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na maovu ya watu wa karibu na wewe.
ü  Jenga urafiki na majirani zako – Jivunie kuzungumza na majirani wanaokuzunguka na hakikisha unakuwa mtu wa msaada au kimbilio la mawazo. Wafanye wengi wavutie na ushauri wako ambayo unalenga kwenye suluhisho la matatizo badala ya kutoa ushauri wa kubomoa.
ü  Andaa ratiba ya siku inayofuata kabla ya kwenda kulala – Bila kuwa na mpangilio wa majukumu hakika kutokana na wingi wa majukumu ya mama, atajikuta kila siku inaisha bila kumaliza kazi zake za msingi. Hali hii itamfanya muda wote awe na uchovu hali itakayopelekea wasiwasi na hofu.
ü  Kuwa na muda wa kupumzika katika ratiba ya siku yako – Kila mara unapojisikia kupumzika hakikisha unaitendea haki nafsi yako kwa kupata muda kidogo wa kupumzika. Kwa kupumzika ni rahisi kuondo msongo wa matatizo yanayokukabiri na kujikuta kwenye uhuisho mpya wa nafsi (self rejuvenation).

32. Tumia mbinu nne zifuatazo kwa ajili ya kuepuka uchovu husiyo wa lazima katika majukumu yako ya kazi:-
  • Mbinu ya kwanza, safisha meza yako ya kazi kwa kuondoa karatasi zote ambazo hazitumiki kwa wakati husika. Hakikisha meza yako ina vitu kulingana na mpangilio wa kazi kwenye ratiba yako. Mpangilio ni sheria muhimu ya kupunguza uchovu katika kazi au biashara unayofanya. Vitu vyote vinavyojitokeza nje ya ratiba yako hakikisha unavikamilisha muda huo huo kabla ya kuendelea na yale yaliyopo kwenye ratiba. Mfano, unapofungua barua pepe yako na kukuta ujumbe unaotakiwa kujibiwa haraka hakikisha unaufanyia kazi badala ya kusema nitajibu baadaye.
  • Mbinu ya pili, tekeleza majukumu yako kwa mpangilio ya umuhimu wa kila kazi. Fanyia kazi kwanza majukumu ya muhimu kabla ya kujihusisha na yale ambayo siyo ya muhimu. Ili ufanikiwe katika mbinu hii unatakiwa kukuza uwezo wako wa kufikiri sambamba na uwezo wa kupangilia vitu kwa umuhimu wake. Hapa ndipo kuna umuhimu wa kupanga majukumu ya siku kabla ya kulala au kuamka asubuhi na mapema katika hali tulivu na kupangalia majukumu ya siku kutokana umuhimu wake.
  • Mbinu ya tatu, unapokutana na tatizo litatue kwanza na kama una ukweli kuhusiana na tatizo husika utumie kufanya maamuzi. Mara nyingi watu wanajikuta kwenye mrundikano wa matatizo yanayotakiwa kutafutiwa suluhisho kutokana na tabia ya kutofanya maamuzi kwa haraka. Ni kawaida kukuta vikao vingi vinajadiri matatizo kibao ambayo mwisho wa kikao hakuna hata moja ambalo limepatiwa suluhisho la kudumu. Hivyo, badala ya kuorodhesha matatizo mengi ni bora kushughulikia tatizo moja na baada ya kulifanyia maamuzi ndipo ugeukie tatizo jingine.
  • Mbinu ya nne, jifunze kupanga, kugatua majukumu na kusimamia. Watu wengi wanajichimbia kaburi kutokana na uchovu wa kila siku kwa kuwa wanashindwa kugatua majukumu kwa watu wengine. Zipo kazi za kawaida ambazo zingefanywa na wasaidizi wao kwa usimamizi wa karibu na hatimaye kupunguza majukumu kwenye ratiba yako. Mbinu hii pia ni muhimu kwa wafanyabiashara maana biashara nyingi zinasimamiwa na mtu mmoja hasa baba au mama jambo linalopelekea kutopata muda wa kupumzika.
33. Uchovu wakati mwingine unatokana na mtu kuboreka (bored) na kile anachofanya. Mwandishi anatushirikisha kuwa mtu anapoboreka kiwango cha mzunguko wa hewa oxyjeni mwilini huwa kinapungua na kupelekea mmengenyo wa chakula kushuka. Hali hii inamfanya mhusika ajihisi hali ya uchovu kutokana kushuka na kwa nishati ya kufanyia kazi. Tafiti zinaonesha kuwa mtu akirudi kwenye mudi ya kazi presha ya damu inaongezeka hali inayopelekea mzunguko wa hewa ya oxyjeni kuongezeka mwilini. Ni kutokana na ukweli huu wote tunashuhudia kuwa ni nadra sana kujihisi uchovu kama tunafanya kazi tunayoipenda. Unaweza kujikuta unafanya kazi zaidi ya masaa sita kwa kazi unayoipenda wakati kazi ambayo inakuboa utajikuta kila baada ya nusu saa unataka kupumzika. Kumbe somo kubwa la kujifunza ni kwamba uchovu hautokani na kazi tunazofanya bali ni matokeo ya wasiwasi/hofu, chuki na mafadhahiko. Mwisho, kuepukana na uchovu hakikisha unapenda kazi unayofanya kwa wakati husika.

34. Pia mara nyingine uchovu unasababishwa na hofu ya kukosa muda wa usingizi. Kila binadamu anataka kupata muda wa kutoshereza kwa ajili ya usingizi japo hakuna mwenye kujua kwa undani usingizi ni nini. Wengi wanakosa usingizi kutokana na hofu zinazowakabili katika Maisha hali ambayo inapelekea kulala usiku mzima bila kupata usingizi. Hali hii inapelekea kuianza siku mpya wakiwa na uchovu na matokeo yake ni kukosa ufanisi katika kazi. Hata hivyo, mwandishi anatushirikisha kuwa kinachopelekea kukosa usingizi ni ile hofu ya kutopata usingizi na tafiti zinaonesha kuwa wengi wanaosema hawapati usingizi huwa wanasinzia bila ya ufahamu wao. Kumbe, tunapolala tunatakiwa kujihisi tupo kwenye mikono ya amani na hivyo kuachia Maisha yetu kwenye mikono ya mamlaka yenye nguvu kuliko sisi. Tafsiri ya haraka haraka ni kwamba utapata usingizi pale utakapojihisi Maisha yako yapo kwenye mikono salama.

SEHEMU YA NANE: JINSI YA KUPATA KAZI YENYE FURAHA NA MAFANIKIO

35. Ukiwa bado haujapata kazi na upo chini ya umri wa miaka 18 hakikisha unafanya maamuzi mawili sahihi katika Maisha ambayo yataamua hatima ya furaha, uchumi na afya yako. Moja, amua aina ya kazi ambayo unataka kuifanya katika Maisha yako. Je unahitaji kuwa mkulima? Je unataka kuwa mfugaji? Je unataka kuwa mfanyabiashara? Je unataka kuajiriwa? Kama unataka kuajiriwa chagua fani/sekta ambayo unataka kuifanyia kazi, mfano, udaktari, sheria, misitu/wanyamapori, uhandisi, uhasibu na fani nyinginezo. Mbili, amua aina ya mtu ambaye unahitaji awe baba au mama wa Watoto wako. Maamuzi yote haya ni sawa na kucheza kamali katika Maisha hivyo ni muhimu kuhakikisha unakuwa makini maana hatima ya ndoto zote za Maisha yako itategemea na maamuzi hayo. Utaifurahia kazi kama unaipenda kutoka rohoni, ni kutokana na furaha hiyo kila mara utahitaji kuendelea na kazi. Vivyo hivyo, utaipenda ndoa kama mnapendana na kuelewana na mwenza wako.

36. Tatizo kubwa ni kwamba watu wengi kazi wanazofanya siyo kazi za ndoto zao. Wengi wanafanya kazi hizo kwa vile ndipo nafasi ya ajira ilipojitokeza hila kile walichotamani toka utotoni pengine hawakubahatika kupata ajira au ufahalu haukuwawezesha kusomea fani hiyo. Hali hii ndiyo inapelekea watu wengi hawafurahishwi na kazi wanazofanya na kwa vile hawana namna inabidi tu waendelee na kazi kwa ajili ya kupata ridhiki ya Maisha. Ana heri mtu yule anayepata kazi ya ndoto yake na tafiti zinaonesha kuwa mtu anayependa kazi anayofanya ana nafasi ya kuishi miaka mingi. Kama mzazi wajibu wako ni kuhakikisha unawaongoza wanao kuchagua kufikia kazi ya ndoto yao. Hapa ndipo wazazi wengi wanakosea kwa kulazimamisha Watoto wao kufanya kazi ambazo wao wanaona ndiyo kazi bora. Katika kuchagua kazi ya kufanya katika Maisha yako zingatia ushauri huu:-
  • Husichague kazi ambayo kila mtu anakimbilia – tafuta fani ambazo zinakimbiwa na watu wengi.
  • Chagua kazi ambayo itakuwezesha kukidhi mahitaji ya Maisha yako - Fanya maamuzi ya kuachana na kazi ambayo unatumia nguvu na akili nyingi lakini bado haiwezi kukidhi mahitaji ya muhimu ya Maisha yako.
  • Fanya utafiti wa kutosha kwenye kazi unayofikiria kuifanya kabla ya kujitosa moja kwa moja kwenye kazi hiyo. Uliza watu ambao tayari wapo kwenye kazi hiyo kwa kipindi kirefu ili kupata uzoefu walionao kwenye kazi husika. Swali muhimu, waliuze kama wangepata nafasi ya kuchagua kazi ya kufanya upya je wangekuwa tayari kuchagua kazi wanayofanya kwa sasa?
  • Epuka Imani kuwa kila mtu anaweza kufanya kazi moja katika kipindi cha Maisha yake. Ukweli ni kwamba mtu mwenye akili timamu anaweza kufanikiwa katika kazi nyingi sawa na ilivyo mtu huyo huyo anaweza kushindwa kufanikiwa katika kazi nyingi pia. Hivyo, kushindwa kufanikiwa katika kazi moja hisikufanye ukate tamaa ya kutafuta kazi nyingine ambayo unaiona kuwa bora ikilinganishwa na kazi ya sasa.
37. Tafiti zinaonesha kuwa takribani asilimia 70 ya hofu au wasiwasi wa wanadamu katika Maisha yake ya kila siku zina uhusiano na mahitaji ya pesa. Tafiti hizi zinaonesha kuwa watu waliohojiwa walikiri kama kipato chao kingeongezeka angalau kwa asilimia 10 hakika wangeweza kumaliza hofu zinazotokana na mahitaji ya pesa. Hata hivyo hali hii siyo sahihi maana ongezeko la kipato huwa linaambatana na ongezeko la matumizi. Hivyo, tatizo siyo kwamba hawana pesa ya kutosha badala yake wanakosa elimu ya namna ya kubajeti vyema pesa wanazopata. Kumbe, kinachosababisha asilimia sabini ya wasiwasi/hofu ni kutokana na watu kukosa elimu sahihi kuhusu pesa. Hizi hapa baadhi ya kanuni ambazo mwandishi anatushirikisha kuhusu namna bora ya kuondokana na hofu zinazotokana na mahitaji ya pesa:-
ü  Watu wengi wanajiuliza sehemu ambako pesa zao huwa zinaenda bila kupata majibu. Kanuni ya kwanza, hakikisha unaandika kila unachofanya na gharama yake. Ainisha kila aina ya matumizi ya siku kwenye kijinotibuku chako na hatimaye mwisho wa mwezi utagundua sehemu ambazo huwa zinapoteza pesa zako.
ü  Kanuni ya pili, andaa bajeti kulingana na mahitaji yanayoendana na pato lako. Mwandishi anatushirikisha kuwa familia mbili ambazo zinaishi kwenye nyumba mbili zinazofanana, katika eneo moja, zikiwa na idadi sawa ya wanafamilia na zote zikiwa na pato linalofanana lakini cha hajabu utakuta bajeti zinatofautiana. Unaweza kushangaa kati ya familia hizo moja pato linatosheleza na nyingine inaangaika kipesa.
ü  Kanuni ya tatu, jifunze kutumia kwa busara. Siyo kila pesa uliyonayo ni lazima itumike tu bila mpangilio bali hakikisha pesa inatumika kulingana na mpango wako wa matumizi.
ü  Kanuni ya nne, husiongeze matumizi yasiyo ya lazima kwenye pato lako. Angalia upya vitu unavyonunua kama vinaendelea kuchukua hela kutoka kwenye pato lako huna budi ya kuachana navyo. Nunua vitu vinavyosaidia kukuza pato lako.
ü  Kanuni ya tano, boresha uaminifu wako sehemu ambazo unaweza kuomba kukopeshwa. Kuna nyakati ambazo dharura zinajitokeza kama hauna uaminifu itakuwa vigumu kupata msaada. Pia hakikisha kabla kukopa jiridhishe kama kuna ulazima wa kukopa – kopa mkopo ambao utatumika kuzalisha faida.
ü  Kanuni ya sita, kata bima ya afya na bima ya kulinda mali zako dhidi ya majanga/ajali. Bima ni kwa ajili ya kukulinda katika matukio ambayo hujui yatatokea lini hivyo ni tahadhari ya kukuhepusha na upotevu wa mali zako pale majanga yanapotokea.
ü  Kanuni ya saba, badala ya kuwekeza kwenye bima ya Maisha kwa ajili ya wategemezi wako baada ya uhai wako wekeza kwenye vitega uchumi ambavyo vitawapa uhakika wa kipato kila mwezi. Mwandishi anatushirikisha kuwa uzoefu unaonesha kuwa wajane wengi baada ya kulipwa pesa za bima ya Maisha baada ya kuondokewa na waume zao pesa hizo huwa hazidumu.
ü  Kanuni ya nane, wafundishe wanao misingi ya elimu ya pesa. Mtoto anatakiwa kufundishwa kuhusu umuhimu wa kutumia fedha kwa nidhamu sambamba kuhakikisha matumizi hayazidi pato lake. Jambo jingine ambalo mtoto anatakiwa kufundishwa ni kuhusu umuhimu wa uwekezaji toka akiwa mdogo.
ü  Kanuni ya tisa, kama kuna ulazima tengeneza pesa za ziada nje ya pato lako. Kuna miradi midogo ambayo unaweza kuifanya katika muda wako wa ziada na kukuwezesha kupata pato la ziada nje ya mshahara wako. Pato hilo ndilo litatumika kujazilizia kwenye upungufu kulingana na bajeti yako.
ü  Kanuni ya kumi, kamwe husicheze kamali. Mwandishi anatushirikisha kuwa Kampuni za Kamali na “Betting” ni wezi ambao wanakubalika kisheria. Kampuni hizi zinatengeneza pesa nyingi kutokana wengi kukimbilia huko wakidhania watafanikisha Maisha yao kupitia bahati.
ü  Kanuni ya kumi na moja, kama hauwezi kuboresha zaidi pato lako ridhika na ulichonacho na siyo kuendelea kulalamika na kuishi kwa huzuni. Ifanye akili yako ikubaliane na hali ya kifedha uliyonayo na hakikisha unaishi kulingana na pato lako.

Hakika tunaweza kuishi Maisha yasiyo na hofu au wasiwasi kufuata misingi ambayo mwandishi ametushirikisha katika kitabu hiki. Utamu wa Maisha upo pale ambapo tunafanikiwa kuweka mbali hofu tulizonazo katika kila sekta ya Maisha yetu. Jiunge na mtandao wa Fikra za Kitajiri kwa  KUBONYEZA HAPA.

Karibuni kwenye fikra za kitajiri ili upate elimu isiyokuwa na mwisho.

Born to Win ~ Dream Big 

Mwalimu Augustine Mathias

Namba ya Simu: +255 763 745 451 au 
 +255 786 881 155 au  +255 629 078 410
Mwanzilishi wa Mtandao wa fikrazakitajiri.blogspot.com
Barua pepe:  fikrazatajiri@gmail.com