👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi hii ya leo ambapo naandika neno la tafakari ya leo nikiwa na furaha tele kutokana na kuzawadiwa siku hii muhimu katika Maisha yangu. Ni kutokana na furaha hiyo najiona kuwa nina kila sababu ya kuendelea kuingarisha Dunia hii kwa kuhakikisha kazi hii inawafikia vijana wengi ambao hakika kati ya vijana 100 watakaofikiwa na ujumbe huu naamini asilimilia 25 kati yao watabadilika kimaisha. Hongera rafiki kwa siku hii muhimu katika Maisha yako.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha baadhi ya kauli ambazo unatakiwa kujisemea kila siku asubuhi na hakika siku yako itakuwa yenye kujawa na furaha na hamasa. Ni wazi kwamba kwenye Maisha tunapokosa furaha na hamasa hatuwezi kufanikisha chochote tunachofanya.
✍🏾Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa furaha na hamasa kwa pamoja ni kichochoe (catalyst) cha kukuwezesha kupiga hatua kwenye kila unachofanya katika siku husika. Hii ni nikutokana na ukweli kwamba hamasa inakuwezesha uwe na nguvu, jitihada na bidii katika kazi. Vivyo hivyo, furaha inakuwezesha kuwa na fikra chanya kwenye kazi yako na mazingira yanayokuzunguka. Kupitia neno la tafakari ya leo kila siku hakikisha unajisemea sentensi hizi:-
✍🏾 Moja, Kwa siku ya leo nitakuwa na furaha. Kauli hii itakuwezesha kuifanya akili yako muda ifikirie matendo yenye furaha kuliko matendo ya hisia hasi. Itakuwezesha uwe fikra zako kuchambua mawazo chanya kwenye kila tukio lililopo mbele yako. Katika tukio hasi wewe utatafuta upande wa pili wa tukio hilo ambao ni upande chanya. Ni kupitia kauli hii utaendelea kutambua kuwa furaha halisi inatokana ndani mwako na siyo kutegemea watu wanaokuzunguka kukupatia furaha unayohitaji.
✍🏾 Mbili, Kwa siku ya leo nitajitahidi kwenda sawa na hali halisi ya Ulimwengu na siyo kulazimisha matakwa yangu. Moja sababu ambayo inapelekea watu kupoteza furaha na hamasa katika Maisha yao ya kila siku ni tabia ya kulazimisha kubadilisha ulimwengu uendane na matakwa/matamanio yao. Ukweli ni kwamba ni rahisi kujibadilisha mwenyewe kuliko kubadilisha mfumo wa ulimwengu. Tafsiri yake ni kwamba kila siku unatakiwa kutekeleza yale yaliyopo ndani ya uwezo wako na mengi kuachia asili (nature) ifanye kazi yake.
✍🏾 Tatu, Siku ya leo nitaulinda mwili wangu. Kauli hii itakuwezesha kuulinda mwili wako dhidi ya mazingira hatarishi unayoweza kukutana nayo katika siku yako. Ni kupitia kauli hii utahakikisha unafanya mazoezi ya kujenga mwili, utakula vyakula na kunywa vinywaji vyenye tija katika mwili wako na utaulinda mwili wako dhidi ya uchafu. Kwa ujumla kauli hii itakuwezesha kuupenda mwili wako kwa kuwa ndilo hekalu la roho yako.
✍🏾 Nne, Siku ya leo nitahakikisha naboresha akili yangu. Kauli hii itakuwezesha kuhakikisha kila siku unapata chakula cha ubongo ambacho si kingine bali ni maarifa mapya. Kila siku unatakiwa kuwa na ratiba ya kujisomea maarifa muhimu ambayo yakuwezesha kupiga hatua katika kila sekta ya Maisha yako. Hivyo, jisemee kuwa siku ya leo nitasoma kitu ambacho kitanifanya niwe na utulivu wa akili kwa ajili ya kupata maarifa mapya.
✍🏾 Tano, Siku ya leo nitaboresha roho yangu kutokana na matendo yangu. Kauli hii inakuwezesha kutenda matendo ambayo yanalenga kuiboresha roho yako katika mazingira yanayokuzunguka. Hapa ndipo unatakiwa kutenda matendo mema kwa jamii inayokuzunguka sambamba na kuwa mtu wa msaada kwa kadri uwezavyo.
✍🏾 Sita, Siku ya leo nitakuwa mtu mwenye kukubalika. Kauli hii inakuondolea hofu ya kukataliwa ambayo inatesa watu wengi. Hivyo, kupitia kauli hii unatakiwa kuandaa mazingira ya kukubalika kuanzia kwenye mavazi unayovaa kwenye siku husika, namna unavyoongea na wengine au jinsi unavyowakosoa wengine.
✍🏾 Saba, Siku ya leo nitajitahidi kuishi kana kwamba leo ndiyo siku yangu ya mwisho. Kauli hii itakuwezesha kuishi kana kwamba hauna deni la kuacha kukamilishwa siku inayofuata. Ni kutokana na kauli hii utaweza kuepuka ugonjwa wa kusogeza au kuhairisha mambo kwa ajili ya kutimizwa baadae.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa kila siku tunatakiwa kuwa na furaha na hamasa ambavyo kwa pamoja vinatupa msukumo wa kutekeleza majukumu yetu ya kila siku. Furaha na hamasa tunaiweza kuipata kutokana na kauli tunazoanza nazo kila siku asubuhi. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(