👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Namshukuru Mungu kwa asubuhi hii ya leo ambapo ni deni kwangu kuhakikisha naitumia vyema kuiboresha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. Pia nashukuru Mungu kwa ajili yako wewe ambaye umeendelea kujifunza kitu kutokana na uwepo wako katika kundi hili.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo utajiri pacha unatakiwa kuutafuta zaidi ya kuangaikia kupata utajiri wa pesa na majumba. Kila mmoja linapotajwa neno utajiri tafsiri ya haraka haraka huwa ni maisha yenye kujitosheleza hasa kwenye mahitaji ya kifedha zinazotokana na uwekezaji kwenye vitega uchumi mbalimbali (vyanzo vya mapato). Ndivyo tulivyoaminishwa toka enzi za ukuaji wetu kuwa tajiri ni lazima awe na pesa, nyumba na magari.
✍🏾Sina tatizo na tafsiri hiyo hila kuanzia sasa pamoja na kuutafuta utajiri wa aina hiyo hakikisha unautafuta utajiri pacha wa ambao ni HEKIMA na BUSARA. Kwa ujumla tunapima maendeleo ya ukuaji wa mtu (personal development) kwa kuangalia HEKIMA na BUSARA aliyonayo. Unaweza kuwa na utajiri wa pesa, nyumba na magari lakini ukaonekana bado haujakomaa kutokana na kukosa utajiri pacha wa HEKIMA na BUSARA.
✍🏾Utajiri huu wa HEKIMA na BUSARA ndiyo unamwezesha mtu kufanya maamuzi mbalimbali dhidi ya pesa zake na jamii inayotuzunguka. Tukizama kwa ndani HEKIMA na BUSARA umwezesha mtu kufahamu jinsi ya kuongea mbele za watu na maneno yapi anatakiwa kuongea kulingana na hadhira inayomzunguka. Kwa kifupi HEKIMA na BUSARA umwezesha mtu kufahamu aongee maneno yapi na maneno hayo hayatamke vipi kulingana na aina yawasikilizaji waliopo mbele yake.
✍🏾Mifano ni mingi kuwa katika jamii wapo watu ambao walikimbilia kutafuta utajiri wa pesa, nyumba na magari na wakasahau utajiri pacha niliokushirikisha katika neno la tafakari ya leo na matokeo yake wakajikuta utajiri wao umegeuka kuwaangamiza. Hali hii ni kwa vile hawakujua utajiri wao utumike vipi katika kuiboresha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. Ndiyo maana jamii ina mtazamo hasi juu ya neno UTAJIRI kutokana imani zinazosababishwa na matajiri hao wasiyo na HEKIMA na BUSARA.
✍🏾Je nipataje utajiri wa HEKIMA na BUSARA katika maisha yangu? Utajiri wa HEKIMA na BUSARA unapatikana kwa kujifunza kila siku. Kila mara unatakiwa kulenga kuwa bora kwenye kila sekta ya maisha yako. Hapa ndipo unahitaji kujifunza kila mara kwa kutumia mbalimbali bila kusahau tabia ya kusoma vitabu au kuhudhuria semina mbalimbali.
✍🏾Mwisho, kupitia makala ya leo tumefunuliwa kuwa pamoja na kutafuta utajiri wa pesa, nyumba na magari bado tunatakiwa kutafuta utajiri wa HEKIMA na BUSARA. Utajiri huu ni silaha ya kukuwezesha kufanikiwa kwenye kila sekta ya maisha yako. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(