👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza pale ulipoishia jana. Muhimu ni kwamba hautakiwa kuacha kutengeneza ushindi mdogo mdogo kila siku kwa maana mjumuisho wa ushindi huo ndiyo mafanikio unayotamani katika Maisha yako. Kumbuka mafanikio ni mchakato ambao unatakiwa kuuishi kila siku.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha njia ya rahisi ya kusoma Makala zinazoshirikishwa ndani ya kundi hili kupitia neno la tafakari ya siku kama tulivyozoea. Nafahamu kuwa mwanzoni mtu anapojiunga na kundi anakuwa na ratibu ya kufuatilia masomo kila siku na kadri siku zinavyoenda anajikuta amesoma masomo yasiyozidi matatu (3) kati ya masomo yanayoshirikishwa katika kipindi cha wiki moja.
✍🏾Hii ni sawa na kwenye usomaji wa vitabu vya mafanikio, wengi huwa wanakuwa na hamasa ya kusoma kitabu ambapo mtu anaweza kusoma kurasa kama kumi za mwanzo na baada ya hapo hakuna mwendelezo unaolenga kukisoma kitabu chote. Kumbe tatizo kubwa lililopo ni kukosa nidhamu binafsi ambayo ingempa msukumo wa kuwa na ratiba ya kujisomea maarifa muhimu kwenye ratiba yake ya kila siku.
✍🏾Kawaida Makala ninazoshirikisha kupitia neno la tafakari ya siku huwa zinawekwa hapa kwenye kati ya muda wa saa moja na robo hadi saa moja na dakika ishirini kwenye siku za katikati ya wiki. Kwa siku za mwisho wa wiki Makala hizi huwa zinawekwa kati ya saa moja na nusu hadi saa mbili. Nakupa muda ambao huwa Makala hizi zinawekwa ili upate urahisi wa kutenga ratiba yako ya kuhakikisha unaianza siku kwa kusoma Makala hizi.
✍🏾Ushauri ni kwamba kila siku kabla ya kufikia saa tatu hakikisha uwe umesoma Makala ya siku husika na kutoa mrejesho kwa ufupi sana juu ya kile ulichojifunza. Pia, inatakiwa kila mara unapoona Makala imeingia kwenye kundi baada ya kufungua data kwenye simu yako uhakikishe unasoma Makala hiyo kwa muda huo huo, husiseme nitasoma baadaye maana ukifanya hivyo baadaye hautapata muda wa kusoma.
✍🏾Nasema hivi kwa kuwa kila siku naona wanaotoa mrejesho ni wachache sana ikilinganishwa na idadi yetu ndani ya kundi. Kadri unavyotoa mrejesho ndivyo natambua kama mada ya siku husika imeeleweka kwa wale waliosoma. Uzuri ni kwamba kupitia mfumo ninaotumia ninaweza kuona Makala niliyoweka imesomwa na watu wapi na wapi hawajasoma.
✍🏾Ukweli ni kwamba natumia nguvu, akili, muda na rasilimali nyingi kuhakikisha natekeleza ahadi yangu ya kukuletea masomo kila siku. Wajibu ulionao ni kusoma masomo haya na kuchambua pointi muhimu za kufanyia kazi katika Maisha yako ya kila siku. Hakika ili ufanikiwe kufanya hivyo ni lazima uwe na nidhamu binafsi ambayo inakusukuma kutekeleza ratiba yako ya kujifunza kila siku.
✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo nimekushirikisha umuhimu wa kusukumwa na nidhamu binafsi ambayo itakuwezesha kutenga muda katika siku yako kwa ajili ya kujisomea Makala zinazoshirikishwa kila siku kwenye kundi hili. Pia, kupitia neno hili tumekumbushwa umuhimu wa kutoa mrejesho juu ya kile tulichojifunza ili iwe rahisi kwa Mwalimu kujua kama masomo yanaeleweka na kutekelezwa na walengwa. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(