NENO LA LEO (APRILI 19, 2020): HIVI NDIVYO ASILI (NATURE) INAVYOTUZAWADIA KULINGANA NA MATENDO YETU

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii zinazolenga kuboresha kila sekta ya Maisha. Wote kwa pamoja tuseme asanthe kwa Muumba wetu kutokana na baraka ambazo anazidi kutujalia katika Maisha yetu ya kila siku. Pia, tuendelee kuunganisha nguvu kama taifa kumuomba Mungu atuepushe na janga la mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha moja ya sheria ya asili ambayo inaendelea kuutawala ulimwengu. Sheria hii imekuwepo toka enzi za kuumbwa kwa ulimwengu na inaendelea kufanya kazi hata katika kizazi cha sasa. Sheria hii si nyingine bali ni: sheria ya kupanda na kuvuna (the natural law of sow and reap). Kwa maneno mengine sheria hii ni sawa na kusema kuwa tunaishi katika ulimwengu wa KISABABISHI (cause) na ATHARI/MATOKEO (effects). Kwa ujumla ulimwengu upo jinsi ulivyo kutokana na matendo yetu.

✍🏾Mwandishi Anthony Robins aliwahi kuandika kuwa ulimwengu jinsi ulivyo ni matokeo ya matendo yetu. Kwa lugha nyingine hatutakiwi kuuona ulimwengu katika sura ya tofauti bali tunatakiwa tufahamu kuwa sisi ndiyo tunaweza kuubadilisha ulimwengu na kuuweka katika sura tunayoitaka. Hapa ndipo kila mmoja anatakiwa kutambua kuwa matokeo anayopata yanatokana na fikra na mitazamo aliyonayo kuhusu ulimwengu.

✍🏾Ukiwa na fikra kwamba ulimwengu ni sehemu hatarishi na hisiyo rafiki kufanikisha chochote hakika utaendelea kuzunguka huku na kule bila kufanikisha chochote katika maisha. Matokeo yake utaanza kujiona mtu hasiye na bahati. Hivyo, jambo la kwanza unalotakiwa kufahamu kupitia neno la tafakari ya leo kuwa “matukio yote yanayotokea katika Maisha yetu iwe ni kwenye afya, uchumi, kiroho, kikazi, mahusiano au kijamii ni matokeo ya matendo au uwekezaji tunaoufanya kila siku”.

✍🏾Baada ya kutambua nguvu ya sheria hii ndipo kila mmoja wetu anatakiwa afahamu kuwa kila ya mafanikio anayoyataka yanaanzia ndani mwake. Ni lazima kwanza abadilishe tabia ili ziendane na mafanikio anayotamani kuyaona katika Maisha yake. Hii ni sawa na aliyekuwa Rais wa nne wa Marekani James Madison alivyowahi kunukuliwa kuwa “ni lazima uishi mabadiliko unayoyataka yatokee (be the changes you want to see)”.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa kila tunachokiona katika Maisha yetu ni matokeo ya uwekezaji wetu. Hivyo, chochote tunachotamani kufanikisha katika Maisha yetu ni lazima tujiulize tunatakiwa kuwekeza nini kwa sasa ambacho kitatupatia matokeo tunayotamani. Kwa nini mpaka sasa haujajipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu cha ‘Kanuni za Pesa”?. Nakala ya uchambuzi wa kitabu hiki bado inapatikana kwa bei ya Ofa ya Tshs. 5,000/= na ndani ya nakala hiyo utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa namna ya kutengeneza, kuwekeza na kutumia pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(