NENO LA LEO (APRILI 2, 2020): WATU WANAANGALIA MATOKEO

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini  yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza moto wa kubadilisha maisha yako kwa kuhakikisha kila siku unatengeneza ushindi mdogo mdogo.



JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha mtazamo wa Jamii inayotuzunguka juu ya watu wanaopata mafanikio katika maisha yao. Ili upate mafanikio ni lazima kuna kanuni ambazo unatakiwa kuziishi kwa kipindi flani cha maisha yako. Kwa ufupi ni kwamba safari ya mafanikio tunaweza kuiweka katika makundi mawili ambayo ni MCHAKATO na MATOKEO.

✍🏾Katika hatua ya MCHAKATO ndipo muhusika anahakikisha anaishi kanuni zinazomuwesesha kufikia mafanikio anayotamani. Kipindi hiki kinahusisha mabadiliko ya fikra na tabia za mhusika ili maisha yake yote yawe kwenye mwelekeo wa mafanikio anayotaka kupata katika maisha yake. Hiki ni kipindi cha kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu. Hiki ni kipindi kinachohusisha uwekezaji wa akili, muda, nguvu na rasilimali fedha. Kwa ujumla hiki ni kipindi ambacho mtu anajikana au kujitoa sadaka kwa ajili kufanikisha kile anachotamani katika maisha yake. Na katika hatua hii ndani ya jamii hakuna mwenye muda wa kufikiria matokeo ya mhusika huko mbeleni sana sana ataonekana mwenye kupoteza muda na fedha.

✍🏾Katika hatua ya MATOKEO ndipo mhusika sasa anaanza kunufaika na bidii alizoweka kwenye kipindi cha MCHAKATO. Hatua hii inakuwa wazi kwenye macho ya kila mwanajamii kwa kuwa mafanikio yanaongea yenyewe. Hapa ndipo kila mtu anaanza kukufuatilia kuhusu vyanzo vya mapato yako. Hapa ndipo vyombo vya Serikali vinaanza kufuatilia akaunti zako na pengine unaweza kuundiwa Timu za kukuchunguza umepata wapi fedha nyingi kiasi hicho. Utapewa majina mengi Mara utaiwa mhujumu uchumi, mtakatishaji pesa au freemasonry. Kwa upande wa majina ya uhujumu uchumi au utakatishaji pesa yataendelea mpaka pale vyombo vya uchunguzi vitakapojiridhisha juu ya uhalali wa vyanzo vyako vya pesa. Hila katika macho ya wanajamii wa kawaida utaendelea kuonekana freemasonry.

✍🏾Hebu fikiria juu ya mifano ifuatayo inavyoweza kubadilisha maisha yako ghafla na kila mtu akaanza kukufuatilia katika hatua ya MATOKEO. Mfano wa kwanza, ukianza kupanda miti kwa sasa na kuhakikisha kila mwaka unapanda ekari zisizopungua mbili baada ya miaka 10 utakuwa na ekari zisizopungua 20 na baada miaka ishirini ukivuna miti yako na kuuza moja kwa moja utakuwa ni milionae mpya ndani ya jamii. Kila mtu atashangaa ni wapi unapata pesa nyingi kiasi hiko.

✍🏾 Mfano wa pili, kila mwaka ukaweka lengo la kununua viwanja viwili vilivyopimwa au kununua ardhi angalau ekari moja kwenye maeneo ya kimkakati. Na katika viwanja hivyo ukaweka mkakati wa kujenga nyumba moja angalau kila baada ya miaka minne. Baada ya miaka 20 utakuwa na viwanja si chini ya 30 na ndani yake utakuwa na nyumba zisizopungua 10. Mifano ni mingi kwenye kila sekta ya uwekezaji ambayo unaiona kuwa fursa kwako. Jambo la muhimu ni kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kutengeneza ushindi mdogo mdogo kwenye fursa ulizochagua.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufunulia kuwa jamii inayotuzunguka inatazama MATOKEO kuliko inavyotazama MCHAKATO wa kufikia matokeo hayo. Wajibu wako ni kujikita kwenye miaingi ya mchakato wa kupata matokeo unayohitaji kwenye maisha yako Hakikisha unapata nakala ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho utapata kanuni 107 kuhusu pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BON TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(