NENO LA LEO (APRILI 6, 2020): [USHAURI] RAHISI NI GHARAMA

👉🏾Habari ya asubuhi Rafiki mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama na upo tayari kuendeleza bidii za kukuwezesha kufanikisha malengo ya Maisha yako. Ni siku nyingine tena ambayo tunazawadiwa kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kuubadilisha Dunia hii kuwa mahala pazuri wa kuishi.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha namna ambavyo umekuwa ukipoteza hela yako kwa kununua vitu vya gharama nafuu huku ukidhania kuwa unaokoa pesa. Watu wengi katika jamii wanatafuta mtelemko wa bei kwa ajili ya kupata wepesi kwenye manunuzi ya bidhaa. Mfano, kama kuna bidhaa A sehemu moja inauzwa kwa Tshs. 50,000/= na bidhaa hiyo hiyo sehemu nyingine inauzwa kwa Tshs. 30,000/= moja kwa moja watu wengi watakimbilia kununua sehemu yenye bei ndogo.

✍🏾Ni jambo jema kukimbilia sehemu yenye mtelemko wa bei lakini mara nyingi bidhaa unapokuta sehemu moja inauzwa gharama ya juu ikilinganishwa na sehemu nyingine kwa utofauti mkubwa wa bei jambo unalotakiwa kujiuliza ni ubora wa bidhaa inayouzwa kwa bei ya chini. Uzoefu unaonesha kuwa bidhaa moja iliyotengenezwa mfano na Mjerumani inaweza kuuzwa kwa gharama ya juu ikilinganishwa na bidhaa ya aina hiyo hiyo iliyotengenezwa na Mchina.

✍🏾Athari iliyopo ya kununua bidhaa kwa kuangalia mtelemko wa bei ni bidhaa husika kutodumu kwa muda mrefu. Utajiona kuwa umeokoa hela wakati unanunua hila bidhaa hiyo uliyonunua kwa bei pungufu muda wa matumizi (time of usage) utakuwa ni mfupi ikilinganishwa na bidhaa ambayo umeikimbia kutokana na bei yake kubwa juu. Kutokana na hali hiyo utajikuta mara kwa mara unatakiwa kununua bidhaa za aina ile ile na hivyo kupoteza pesa zako.

✍🏾Watu waliofanikiwa kitu cha kwanza wanachozingatia katika kufanya manunuzi ya aina yoyote ni kuangalia ubora wa bidhaa husika. Baada ya kujiridhisha kuwa bidhaa inau bora unatakiwa ndipo wanaomba kupunguziwa bei kama inawezekana. Hali hii inatakiwa kutumika kwenye sekta zote za uzalishaji mali. Mfano, kama unajenga hakikisha unaweka ubora kana kwamba nyumba hiyo haitaharibika ndani ya miaka 100 ijayo. Kanuni hii itakusaidia kupunguza gharama za marekebisho ya mara kwa mara hivyo kuokoa pesa yako.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo limetukumbusha kuwa katika manunuzi ya aina yoyote tunayofanya tunatakiwa kutanguliza ubora kuliko kununua kwa kufuata mtelemko wa bei. Hata hivyo, haimaanishi kuwa kila bidhaa inayouzwa kwa bei ya juu ndiyo bora zaidi, hivyo, unatakiwa kujiridhisha juu ya ubora wa bidhaa husika kabla ya kudumbukiza pesa yako. Hii ni pamoja na kujiridhisha juu ya bei za bidhaa husika kwa wauzaji wengine ili kuepuka wauzaji ambao huwa wanauza bidhaa kwa gharama ya juu.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BORN TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(