👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa asubihi hii ya leo ambapo ni siku nyingine tunalianza juma la pili katika mwezi Aprili, 2020. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu na hamasa za kutosha kwa ajili ya kuendeleza bidi ya mafanikio kwenye kila sekta ya Maisha yako.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha umuhimu wa msamaha kama moja ya mbinu ya kuboresha sekta ya mahusiano yako na watu wanaokuzunguka. Katika Maisha ya kila siku ni rahisi kuwa na hasira, kukunjamana uso au kufoka au kuwa mkali baada ya kutendewa vibaya kwa namna yoyote ile na watu wanaokuzunguka. Katika hali hiyo ya hasira unaweza kujikuta umetenda tukio ambalo hukukusudia kufanya au nyakati nyingine utajutia kwa nini ulifanya hivyo.
✍🏾Binadamu ameumbwa katika asili ambayo ni vigumu kusamehe kwa roho moja au kusamehe na kusahau pale anapokuwa amehumizwa au kutendewa vibaya. Pamoja na ugumu huo wa kusamehe tunatakiwa kukumbuka kuwa hatuwezi kuwa na maisha ya furaha kama tunaishi kwa chuki, kinyongo au ugomvi dhidi ya watu wanaotukosea. Ni wazi kuwa chuki, kinyongo, ugomvi, huzuni na hisia nyinginezo zinazotokana na kuumizwa na watu wanaotuzunguka zinaharibu afya yetu pale tunaposhindwa kuruhusu zitoke ndani mwetu.
✍🏾Tumepewa mamlaka toka siku tuliyoumbwa ambayo yanatuwezesha kuchagua kuwa kati ya hisia mbili tofauti kwa nyakati tofauti. Kila unapochagua kuwa na hisia moja ni dhahiri kuwa umeamua kuachana na hisia nyingine kwa wakati huo. Hii ndiyo sheria ya asili ya uwili kinzani (the natural law of duality) ambayo mara nyingi nimekuwa nikikushirikisha kujua namna ya kuitumia kwa faida katika Maisha yako. Unaweza kuamua kuwa na hisia za furaha, amani na faraja na baadaye unaweza kuamua kuwa na hisia za hasira, ugomvi na huzuni.
✍🏾Kupitia neno la tafakari ya leo nataka kuanzia sasa uchague hisia ambazo ni sahihi katika maisha yako ili uishi kwa amani na furaha dhidi ya jamii inayokuzunguka. Hata hivyo, ni lazima tuwe tayari kutofautisha kati ya kusamehe na upole kwani tunapokuwa watu wa msamaha haimaanishi kuwa tuwaache watu watufanyie maovu kwa kadri watakavyo la hasa. Hapa ndipo unatakiwa kuwa na mipaka binafsi katika kila sekta ya maisha yako na mipaka hiyo haipaswi kuvukwa na mtu yeyote bila ridhaa yako.
✍🏾Ni kutokana na ukweli huu kila mtu ana anatakiwa kuheshimu mipaka yako kwenye masuala ya faragha, wema, upendo, ukweli, heshima, haki na mahusiano mengine kwa ujumla wake. Na endapo mtu yoyote atavuka mipaka hiyo unahitaji kusimama imara ili ili atambue kuwa haupo tayari kuona mtu yoyote anavuka mipaka hiyo.
✍🏾Hata hivyo, unatakiwa kutambua kuwa mipaka hii ni nadharia kwani inachorwa katika akili yako na haionekani kwa macho. Hivyo, unatakiwa kuwa mtu wa kwanza kuiheshimu mipaka hiyo katika Maisha yako ya kila siku na kadri unavyoheshimu mipaka hiyo ndivyo kila mmoja katika jamii inayokuzunguka ataweza kuiheshimu mipaka hiyo. Hali hii itakufanya uwe salama dhidi ya tabia mbaya za binadamu wanaokuzunguka. Mfano, mdogo ni ule usemi tuliouzoea “jiheshimu ili uheshimike”.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha umuhimu wa kusamehe katika Maisha yetu ya kila siku. Tumeona kuwa tunaposamehe ni moja ya njia ya kutuhepusha na hisia ambazo zinaathari afya yetu. Hivyo, tunaposamehe ni moja ya hatua ya kujihepusha na hisia hizo ili tuwe na furaha katika Maisha yetu. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(