👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza bidii katika majukumu yako ya leo. Ni siku ambayo unatakiwa kuitumia kwa faida yako maana wapo watu wengi ambao walitamani kuwa hai lakini hawakufanikiwa. Pia, wapo ambao wapo hai lakini hawana maarifa haya bali wanachoona ni mawio na machweo ya jua bila kuwa na mpango wowote wa Maisha yao.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha tabia ambayo imekuwa ikikukwamisha kuchukua hatua muhimu katika yale unayojifunza katika Maisha yako ya kila siku. Tunaishi katika ulimwengu ambao watu wenye MACHO ya KUONA na wenye MASIKIO ya KUSIKIA wanajifunza kila siku. Kutokana na uwepo wa MACHO na MASIKIO hayo walio tayari kujifunza wanajifunza kila mara kutokana na mazingira yanayowazunguka.
✍🏾Ni kutokana na kujifunza huko kila mara wale wenye tabia ya kujifunza wanapata HAMASA ya kuchukua hatua muhimu katika Maisha yao. Mfano, kwa kutumia macho ukiwa unatembea kutoka sehemu moja hadi nyingine utaona jinsi ambavyo watu wanaweka jitihada za maendeleo katika kazi mbalimbali wanazofanya. Moyoni unajisemea hata mimi naweza kufanya hiki katika maeneo yangu (tayari umehamasika). Mfano wa pili, unaweza kuwa Youtube ukaona “clip” ya mfugaji maarufu wa kuku au mbuzi, ukajisemea hata mimi ninaweza kufuga kuku katika eneo langu ili niweze kuongeza kipato changu.
✍🏾Vivyo hivyo, katika maongezi na rafiki zako unaweza kusikia jinsi ambavyo wenzako wamefanikiwa kupiga hatua katika miradi mbalimbali ambayo ipo ndani ya uwezo wako. Moyoni moja kwa moja unajisemea hata mimi mwaka huu ni lazima nianzishe mradi kama huo kama eneo langu. Hiyo ni HAMASA ambayo imejengeka kwenye akili yako kutokana na kutumia vizuri masikio yako maana siyo wote wenye uwezo huo.
✍🏾Bila kusahau kila mara unaposoma neno la tafakari ya siku kupitia jukwaa hili kuna hamasa flani ambayo unaipata katika akili yako. Hamasa hii huwa inadumu kwa muda kadhaa katika akili yako baada ya kusoma Makala ya siku na katika kipindi hicho unajisemea hakika Mwalimu leo kanifunulia kitu ambacho nilikuwa nachukulia mzaha katika Maisha yangu ya kila siku.
✍🏾Kumbe kila siku wenye macho na masikio wanapata HAMASA kutokawa kwa jamii/mazingira yanayowazunguka. Pamoja na HAMASA hiyo hakika ni wachache wanaochukua hatua zinazolenga kuweka kuitekeleza HAMASA husika kwa vitendo. Ukweli ni kwamba watu wengi wana tabia ya kuhamasika kwa muda na baadaye wanarudi katika hali ya Maisha waliyoyazoea.
✍🏾Ndivyo ilivyo maana kwa asili mwili wa mwanadamu hautaki kujisumbua katika kuchukua hatua mpya za kimaisha. Mara nyingi HAMASA inajengeka kwenye AKILI ya mhusika na ili mzunguko wake ukamilike ni lazima MWILI wa uhusike. Hapo ndipo tatizo linapoaanzia maana mwili mara zote hautaki changamoto mpya katika Maisha. Mwili umezoea kuishi kwenye ukanda wa faraja (comfort zone) kwani katika ukanda huo hakuna usumbufu. Niliwahi kuandika kuwa “akili inataka lakini mwili ni dhaifu”, maneno haya pia tunayasoma kupitia maandiko matakatifu.
✍🏾Mwisho, somo kubwa ninalotaka ujifunze kutokana na Makala ya leo ni kutambua kuwa HAMASA bila kuchukua hatua zinazolenga kutekeleza kwa vitendo ni moja ya tabia hatarishi ambayo inaendelea kukukwamisha. Ili upige hatua kwa kasi unatakiwa kuhakikisha MWILI wako uwe tayari kuisikiliza na kuitii AKILI yako katika maarifa yote unayojifunza katika Maisha yako ya kila siku. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(