NENO LA LEO (APRILI 3, 2020): MATOKEO YANAOGOPESHA

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tena ambayo tumezawadiwa na Muumba kwa ajili ya kuendeleza bidii katika safari ya kufikia kule tunakotamani kufika. Hongera sana kwa siku hii ambayo hakika una deni la kuitumia vizuri.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambalo ni mwendelezo wa neno la tafakari ya jana (Aprili 2, 2020).  Katika neno la tafakari ya Jana tuliona kuwa macho ya jamii tunayoishi yanatazama zaidi kwenye MATOKEO kuliko ilivyo kwenye MCHAKATO. Hali hii inapelekea watu wengi katika jamii kushindwa kuchukua hatua zinazolenga kuboresha maisha yao kwa kuwa wanaojifunza kwenye MCHAKATO wa kufikia mafanikio ni wachache ikilinganishwa na wale wanaojadili MATOKEO.

✍🏾Katika uhalisia wa mafanikio hatua ambayo mtu anaweza kujifunza kwa vitendo ni kwenye MCHALATO (process) ikilinganishwa na MATOKEO. Hali hii inatokana na ukweli kwamba hatua ya MATOKEO inaogopesha. Mtu ambaye amefikia hatua hiyo moja kwa moja anatafsiriwa kuwa kwenye viwango vingine kiasi ambacho hata ukaribu wa kujifunza kutoka kwake haupo.

✍🏾Ni katika hatua hii ya MATOKEO ndipo watu wanatathimini na kuona kuanza kujisemea jamaa ana bahati bila kujua kuwa bahati imetafutwa au kutengenezwa kupitia hatua ya MCHAKATO. Kumbe kama ukikutana na mtu yeyote aliyefanikiwa zaidi yako badala ya kuuliza mafanikio aliyonayo (MATOKEO) ulizia juu ya njia anazotumia (MCHAKATO) kupata matokeo husika.

✍🏾Hapa ndipo watu huwa wanakosea kwa kuwa baada ya kuambiwa kuhusu MCHAKATO unaotumika kupata MATOKEO wanajikuta kuwa walishachelewa kwa kuwa kile kinachoonekana leo kama mafanikio kilitengezwa kupitia michakato halali ya muda mrefu. Success is a process (mafanikio ni mchakato)

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kuwa badala ya kuomba mkate kwa mtengeneza mkate tunatakiwa kuomba kufundishwa mbinu zinazotumika kutengeneza mkate. Hii ni sawa na alichowahi kusema Donald Trump kupitia kitabu chake cha How to Get Rich kuwa kwa vile yeye ni Bilionea kila anakokwenda watu wanamuuliza ni jinsi gani mtu anaweza kutengeneza pesa. Hata hivyo ni wachache ambao wapo tayari kufuata hatua hizo za kutengeneza pesa kwa kuwa wengi wanaishia kujisemea sina bahati kwa vile hawajui kuwa bahati inatafutwa. Hakikisha unapata nakala ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho utapata kanuni 107 kuhusu pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BON TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(