👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu na hamasa ya kuendeleza pale ulipoishia jana. Hii ndiyo salamu yangu kuu ambayo kila asubuhi nitaendelea kukumbusha kwa ajili ya kukuwezesha kuianza siku yako ukiwa na hamasa ya kutosha. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ni hamasa pekee ambayo itakufanya uendelee hata kama kwa mbele unaona giza.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha mbinu ambayo unatakiwa kuitumia kwa ajili kujifunza maarifa mapya katika Maisha yako. Kama unahitaji kuboresha Maisha yako hakuna njia ya mkato zaidi ya kuweka utaratibu wa kujifunza maarifa mapya kwenye kila sekta ya Maisha yako.
✍🏾Tulipokuwa wadogo tulifundishwa misamihati kama vile: “elimu ni bahari” au “elimu haina mwisho” lakini kutokana na kukalilishwa majibu hatukuwahi kujua maana halisi ya misamihati hiyo. Ni sentesi fupi hila katika Maisha ya mafanikio zinabeba maana kubwa sana.
✍🏾Kumbe basi tunaona kuwa ili ufanikiwe kimaisha hakuna namna nyingine zaidi ya kuweka utaratibu wa kujifunza maarifa mapya kila mara. Mbinu ninayokushirikisha kupitia neno la tafakari ya leo ni: KABLA YA KUJIFUNZA ONDOA HISIA NA MTAZAMO WAKO KWENYE MADA UNAYOTAKA KUJIFUNZA (Before you learn you have to unlearn everything). Hapa ndipo kasheshe inapoanzia kiasi kwamba watu wanashindwa kujifunza wakiwa na hisia/mtazamo huru na matokeo yake hakuna jipya wanalojifunza.
✍🏾Kwa asili jamii inayotuzunguka ina watu wengi ambao wanajiona kujua kila kitu katika Maisha yao (know it all). Wengine tupo humu ndani na ndiyo maana nimesukumwa leo hii nifundishe mbinu hii kwa ajili ya kuwezesha kila mmoja aweze kujifunza maarifa mapya kwa urahisi.
✍🏾Tatizo ni kwamba pale unapojifunza ukiwa umejifunga kwenye hisia na mtazamo wako kila maarifa unayojifunza utajikuta unalazimisha yaendane na hisia/mtazamo wako. Matokeo yake ni kwamba hakuna unajichofunza kwa kuwa mwisho wa kila somo unaishia kuingia kwenye himaya ya hisia na mtazamo wako.
✍🏾Tumeona kuwa elimu haina mwisho, hila changamoto tulionayo ni elimu ya darasani tuliyosoma ilitufanya tujione kuwa tumefikia mwisho wa kujifunza baada ya kuhitimu. Elimu hii ya darasani ilitufanya tujione tumefahamu kila kitu kuhusiana na Maisha yetu hivyo hakuna haja ya kujisumbua kutafuta maarifa mapya. Matokeo yake jamii ina watu wengi ambao ni kawaida kumaliza miaka kadhaa bila kusoma hata kitabu kimoja.
✍🏾Hali hii inatufunulia kuwa katika jamii, asilimia kubwa ya watu ni wale ambao wanaona hisia na mtazamo wao ndo kila kitu katika Maisha hivyo hakuna haja ya kujifunza maarifa mapya. Ni tabia hiyo ambayo inatufanya kila tunaposhika kitabu kwa ajili ya kupata maarifa mapya tunajikuta tunasinzia kwa vile tunaona hakuna jipya katika kitabu ambacho ni zaidi ya hisia au mtazamo tulionao.
✍🏾Mwisho, kupitia makala ya leo nimekufunulia kuwa kama unataka kujifunza maarifa mapya huna budi ya kuweka hisia na mtazamo wako pembeni kuhusiana na ujuzi au maarifa unayotaka kujifunza. Hakuna namna nyingine ambayo itakuwezesha upige hatua katika Maisha zaidi ya kuwa na utaratibu wa kujifunza maarifa mapya na kuweka mikakati ya kuyatekeleza hatua kwa hatua katika Maisha yako ya kila siku. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(