NENO LA LEO (APRILI 17, 2020): [SIRI] FAHAMU KWA NINI BIASHARA NYINGI HUWA ZINAKUFA KATIKA KIPINDI CHA AWALI TOKA ZIANZISHWE

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama. Tumia dakika kadhaa kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyokupa katika Maisha yako. Pia, muda huo wa muunganiko na Mungu hakikisha unamuomba akulinde uwe salama katika siku hii ya leo kwenye kila hatua utakayopiga.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha kwa nini biashara nyingi huwa hazidumu katika kipindi cha awali toka zinapoanzishwa. Tafiti zinaonesha kuwa tafiti zinaonesha kuwa asilimia 96 ya biashara zote huwa zinakufa kabla ya kutimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake. Kati ya hizo, takribani asilimia 80 huwa zinakufa ndani ya miaka miwili toka kuanzishwa kwake. Hata hivyo, asilimia 4 ya biashara ambazo zinaweza kumudu kuendelea baada ya miaka 10 haimaanisha kuwa zinafanya vizuri katika kutengeneza faida kwa wamiliki.

✍🏾Katika kitabu chake cha Sale Like Crazy Mwandishi kijana na bilionea Sabri Suby anatushirikisha kuwa biashara nyingi zinashindwa kukua zaidi ya miaka kumi kutokana na wamiliki wa biashara hizo kushindwa kutumia mbinu sahihi za kuiendeleza biashara husika. Mbinu namba moja ni kuhakikisha biashara inajiendesha kwa faida kwa maana uwezo wa wa biashara kuendelea kuzalisha mapato.

✍🏾Kwa maneno rahisi, ili biashara iendelee kukua toka kipindi cha kuanzishwa kwake inatakiwa iendeelee kuzalisha fedha za kutosha ambazo zitawezesha uendelevu na ukuaji wa biashara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba fedha zinazozalishwa na biashara husika ndo uhai, hewa na chakula cha biashara hiyo kuendeleza uhai wake.

✍🏾Hata hivyo siri iliyopo ni kwamba, ili biashara iweweze kuendelea kuzalisha faida ni lazima iwe na mfumo unaowezesha kuendelea kupata wateja wapya kila mara pamoja na mfumo imara wa kulinda wateja waaminifu. Ukifanikiwa kuwa na mfumo imara wa kulinda wateja na kupata wateja wapya moja kwa moja mauzo yako yataendelea kukua.

✍🏾Biashara nyingi zinakufa katika kipindi cha awali toka kuanzishwa kwake kwa kuwa waanzilishi wengi wa biashara wanakuwa hawana elimu ya misingi ya bisashara. Mfano, biashara nyingi zinaanzishwa kutokana ujuzi wa mwanzilishi wa biashara katika biashara anayoanzisha. Mfano, Mpishi anaamua kuanzisha mgahawa, Mwanasheria anaanzisha Kampuni ya huduma za kisheria au daktari anaanzisha biashara ya huduma za afya. Kubwa, ni kwamba waanzilishi wote hao hawana misingi ya kuendesha biashara husika na matokeo yake ni kwamba biashara zinakufa au zinadumaa.

✍🏾Kutokana na waanzilishi wengi kushindwa kuwa na misingi sahihi ya biashara wanajikuta biashara zinakuwa ni kazi kwa mmiliki (job) badala ya kuwa sehemu ya kuzalisha fedha kwa mmiliki wakati huo huo ikimpunguzia muda wa kufanya kazi. Mfano, biashara nyingi katika jamii yetu ni zile ambazo mmiliki hawezi kutoka kwenye biashara kila siku na hivyo anakuwa ni mtumwa wa biashara husika.

✍🏾Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumeona kuwa biashara nyingi zinakufa kutokana na waanzilishi wengi kutoka kuwa na elimu sahihi ya msingi wa biashara. Elimu hii inahusisha namna ya kulinda pesa zinazozalishwa pamoja na namna ya kukuza idadi ya wateja kwa ajili ya bidhaa zako. Elimu hii husitegemee kuipata shuleni bali ni kupitia kusoma vitabu mbalimbali ambavyo waandishi walishakurahisishia ili uvipate kwa urahisi ni suala la wewe kujibidisha kusoma vitabu hivyo. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(