NENO LA LEO (APRILI 5, 2020): [COVID_19] KIPINDI MUHIMU CHA KUBADILISHA TABIA HUSIZOZIPENDA KATIKA MAISHA YAKO

👉🏾Habari ya asubuhi mpendwa rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Mungu ni mwema kiasi ambacho ameendelea kutuweka salama na kutuzawadia siku muhimu katika maisha yetu. Hakika kila asubuhi tunatakiwa kuianza siku kwa kujisemea kauli hii: "Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana tuitumie na kumshangalia Bwana". Kauli hii inatupa hamasa ya kutumia vyema siku za maisha yetu ili hatimaye mwisho wa uhai wetu tufanikiwe kuacha alama katika uso wa Dunia.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha namna ya kutumia kipindi hiko ambacho hofu ya COVID 19 inayumbisha maisha kwa ajili kujenga tabia mpya katika maisha yako. Unapojenga tabia mpya moja kwa moja unakuwa umeachana na tabia mbaya ambazo umekuwa uzipendi lakini kila ukijaribu kuachana nazo unajikuta unashindwa.

✍🏾Dunia ya sasa tunashuhudia kila taifa likiweka mbinu zake za kupambana na CORONA. Yapo Mataifa ambayo yamezuia kutotoka nje kabisa kama sehemu ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu ambao kwa kiasi kikubwa unasambaa kwa kugusa sehemu yenye kirusi au kupitia kukohoa/kupiga chafya kwa mtu mwenye maambukizi akiwa karibu na mtu hasiye na maambukizi. Kwa hapa Tanzania moja ya jitihada zilizowekwa na Serikali ni kuzuia mikusanyiko ya watu hisiyo ya lazima sambamba na kuzingatia usafi wa mikono kila mara.

✍🏾Ndani ya jitihada zote zilizowekwa kama mbinu ya kupambana na CORONA kuna fursa nyingi za kumwezesha mhusika kubadilisha tabia. Neno la tafakari ya leo linalenga kukufunulia fursa hizo ili ufanikiwe kujenga tabia mpya katika maisha yako. Karibu ujifunze kwa undani hapa chini:-

✍🏾 Je kwa kipindi kirefu umekuwa mtu wa huruma kwa kufanikisha kila sherehe unayopewa kadi ya mchango?. Kipindi hiki cha COVID 19 kinakupatia muda wa kutathimini kiasi cha pesa ambacho umekuwa ukipoteza kutokana na michango ya kufanikisha sherehe zisizo za lazima kwako. Baada ya tathimini hiyo jenga tabia mpya ya kuhakikisha unatoa mchango wa sherehe pale ambapo unaona kuwa ni lazima ufanye hivyo kutokana na ukaribu wa yule anayekupa kadi. Weka mbinu za kukataa kadi pale ambapo unaona kuwa kadi hizo siyo za lazima wewe kushiriki.

✍🏾 Je umekuwa ukipoteza pesa zako kwa kujaribu bahati yako kupitia kubet?. Katika kipindi hiki ambacho michezo mingi imesimamishwa ni muda muhafaka kwako kuachana na tabia hiyo. Jitazame katika Ulimwengu mpya ambao unaweza kuendesha maisha yako pasipo kucheza bahati na sibu.

✍🏾 Je umekuwa unapoteza muda mwingi kwa kufuatilia michezo hasa ligi kuu mbalimbali?. CORONA imekupa nafasi ya kukaa chini na kujitafakari upya kuwa unaweza kuishi bila kufuatilia michezo hiyo unayoipenda.

✍🏾 Je umekuwa ukikosa nafasi ya kukaa pamoja na wapendwa wako kwa kuwa uko bize na kwenye sehemu za starehe au mikusanyiko ya kila aina?. CORONA inakupa nafasi ya kukaa nyumbani na wapendwa wako. Hata kama Serikali yetu haijazuia kutoka nje, wewe binafsi unatakiwa kujizuia kwenda sehemu ambazo siyo za lazima. Kumbuka wewe una nafasi kubwa ya kuilinda familia yako dhidi ya maambukizi. Hivyo, unatakiwa kupunguza kwenda sehemu ulizozoea kwenda kwa ajili ya burudani. Sasa unaweza kujijengea tabia mpya ya kuburudika ndani na wapendwa wako.

✍🏾 Je umekuwa ukitamani kupata muda wa kujisomea vitabu?. Baada ya kupunguza mizunguko hisiyo ya lazima sasa una nafasi ya kuanza kujisomea vitabu na hatimaye kufanikiwa kupata maarifa muhimu ya kuboresha maisha yako.

✍🏾 Je umekuwa kwenye kundi la marafiki ambalo unatafuta njia ya kulikwepa bila mafanikio?. CORONA inakupatia sababu nzuri ya kukimbia makundi yote yanayokwenda kinyume na mtazamo wako au kukukwamisha kuishi kanuni muhimu za maisha. Ukiulizwa mbona siku hizi hauonekani kwenye vijiwe vyetu? Jibu moja kwa moja kuwa napunguza uwezekano wa kuambukizwa na CORONA.

✍🏾  Je umekuwa na tabia ya kutokuwa mwaminifu kwa mwenza wako?. CORONA inakupa nafasi ya kumuogopa kila unayemuona mzuri maana haujui ni yupi mwenye maambukizi. Jenga tabia mpya ya kumuona mzuri pekee ni mwenza wako maana kama hadi sasa haujapata maambukizi ya CORONA ni kipimo tosha kuwa mwenza wako yuko salama.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatufunulia mwanga kuwa kipindi hiki kina fursa ndani yake za kutuwezesha kuishi tabia mpya. Ni kipindi muhimu cha kuacha tabia zote ambazo zimekuwa msalaba kipindi kirefu cha maisha yetu. CORONA ni hatua muhimu ya utakaso wa maisha yetu. Hakikisha unapata nakala ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho utapata kanuni 107 kuhusu pesa. 

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BON TO WIN ~ DREAM BIG

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(