👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Hongera kwa siku hii ya leo ambapo Waumini wa Kikristo wanasherekea Siku Kuu ya Pasaka ambayo ni maadhimisho ya Ufufuko wa Christu Yesu Mungu Mwana. Ni siku muhimu kwako kuendeleza bidii ya mafanikio katika kila sekta ya Maisha yako maana kama ni biashara siku kuu kama hizi huwa zinaambatana na matumizi makubwa ya pesa.
👉🏾Pia, kwa wale ambao leo hii ni siku ya mapumziko ni siku muhimu ya kukaa pamoja kama familia na kutafakari kwa pamoja malengo ya familia kiroho, kiuchumi, kiafya na kijamii. Ni siku ambayo pia katika mapumziko hayo unaweza kuitumia kwa ajili ya kurudisha kwenye jamii kupitia matendo mema kwa makundi maaluma kama vile kuwakumbuka Wazee, Wajane, Wafungwa na Watoto yatima.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo nitakushirikisha namba unavyotakiwa kuilinda pesa yako kwa gharam yoyote bila kujali maneno ambayo utaambiwa na jamii inayokuzunguka. Katika jamii yetu kula kila Imani kuhusiana na pes ana Imani hizo mara nyingi zimesababishwa na kukosekana kwa elimu ya pesa katika jamii. Mfano, wapo ambao wanaamini kuwa kadri unavyotumia pesa ndivyo inavyokuzoea!
✍🏾Ni juzi tu katika maongezi kwenye kundi la WhatsApp la Wahitimu wenzangu wa kidato cha nne (2005) nilijikuta katika masikitiko baada ya kuona kuwa kuna wahitimu mpaka wa digrii ya kwanza ambao bado wanaishi katika Imani za kizamani kuhusina na pesa. Hakika niliona kuwa kuna pengo kubwa la elimu ya pesa katika jamii ambalo hakuna namna nyingine ya kuliondoa zaidi ya kuendelea kutoa elimu kwa vijana.
✍🏾Tumia pesa ikuzoee!!! Watu wanaendelea kutumia pesa bila mpangilio wakitarajia kuwa kadri wanavyotumia pesa ndivyo itawazoea lakini kila wakijitahidi kufanya hivyo pesa ndivyo inazidi kuwakimbia. Umri unasogea na majukumu yanaongezeka lakini kipato hakiozeki kwa vile matumizi yanaendelea kuwa makubwa ikilinganishwa na kipato cha familia. Unaweza kutafuta mchawi ni nani ambaye anapelekea pesa zako hazikai mfukoni kumbe mchawi ni tabia zako mwenyewe ambazo zinatokana na kukosa elimu ya pesa.
✍🏾Kama ni pesa yako halali kuanzia sasa kubali kuitwa bahili au mchumi. Hakuna namna nyingine ya kuhakikisha matumizi yako yanakuwa madogo ikilinganishwa na kipato chako zaidi ya kuwa na bahili wa pesa unazopata. Moja ya kanuni ya pesa ambayo unatakiwa kuitumia kwa faida ni: matumizi hayapaswi kuzidi pato lako. Hauwezi kufanikisha hilo kama unaendelea kutafuta umaarufu kwenye jamii kwa kutumia ovyo na kugawa pesa zako. Kuanzia sasa kubali kuitwa bahili.
✍🏾Kama ni pesa yako halali kuanzia sasa kubali kuitwa mchoyo maana wanaotaka mgawane pato lako hawajui mipango uliyonayo. Tatizo ni kwamba kila mpango ulionao kwa ajili ya Maisha ya baadaye unategemea uwezo wako wa kulinda pesa unayopata katika Maisha yako ya kila siku. Ukiendelea kusambaza upendo kwa jamii inayokuzunguka kwa kusambaza pesa yako nje ya bajeti hakika mipango uliyonayo itaendelea kuwa ndoto zisizokamilika kipindi chote cha Maisha yako.
✍🏾Kama ni pesa yako halali kubali kuitwa mshamba maana zipo nyakati za kuitwa mshamba kwa ajili ya kesho iliyobora. Hata hivyo, Maisha ni kuchagua unaweza kuamua uitwe kijana wa “Town” kutokana na kutimiza Imani za jamii kuhusu pesa ambazo kwa asilimia kubwa zinahusisha matumizi makubwa ya pesa. Matokeo yake ni kuvuna kulingana na mbegu unayopanda.
✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha umuhimu wa kuilinda pesa tunayopata kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kwa gharama yoyote bila kujali maneno ya wale wanaotuzunguka. Utaitwa bahili, mchumi, mchoyo, mbinafsi, mshamba na kadharika kwa upole yapokee majina yote hayo kwa kuwa wewe ndiyo mwenye kujua ndani ya hayo yote kuna mpango gani. Pesa! Pesa! Pesa! Pesa! toka enzi za kugunduliwa kwake imekuwepo na itaendelea kutawala Maisha ya mwanadamu hivyo hauna budi zaidi ya kuendelea kujielimisha kuhusiana na Pesa. Naendelea kukumbusha kuhakikisha unapata nakala yako ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho ndani yake utajifunza kanuni 107 kuhusu pesa.
👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(