NENO LA LEO (APRILI 4, 2020): JE NI MCHWA UPI UNAOTAFUNA PESA ZAKO?

👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza jitihada kwenye majukumu yako ya kimkakati. Ni siku nyingine kwenye maisha yako ambayo ni muhimu kuitua vyema ili kuendelea kulipa thamani jina lako.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo leo nalenga ujifanyie tathimini inayolenga kufahamu vyanzo vikuu vya upotevu wa pesa yako. Watu wengi katika jamii tunayoishi wanalalamika kuwa wakishika pesa inapitiliza. Siyo tatizo pesa kupitiliza endapo inaelekea sehemu sahihi ambayo mhusika amekusudia kuitumia kulingana na mipango kazi yake. Tatizo ni pale ambapo pesa inapitiliza na kila ukijiuliza umeitumia kufanya nini haupati jibu. Neno la tafakari ya leo linatumia neno "MCHWA" kujumuishi matumizi ya ovyo yanayopelekea ipotee.

✍🏾Mkulima pindi anapolima mazao ya nafaka kama vile mahindi, mpunga, alizeti na mazao mengineyo ni lazima aweke usimamizi unaolenga kuzuia upotevu wa mazao kutoka kwa wanyama au wadudu waharibifu. Baadhi ya wanyama wanaopelekea upotevu wa mazao ni nyani, ngedele, ndege na wadudu wanaoharibu mazao. Ili mkulima huyu avune mazao ya kutosha ni lazima aweke mkakati wa kuzuia uharibifu unaotokana na wanyama au wadudu hao.

✍🏾Mfano wa pili ni kutoka kwa mfugaji. Kila mfugaji anafahamu kila aina ya "mchwa" ambao ni hatari kwa mifugo yake. Bila kufahamu michwa hiyo mfugaji ataendelea kupoteza mifugo kila mara jambo ambalo litapelekea mifugo yake isiongezeke. Mfano mfugaji wa kuku anatakiwa kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali  kama vile ugonjwa wa ndui. Vivyo hivyo kwa mfugaji wa ng'ombe au mbuzi ni lazima ailinde mifugo yake dhidi magonjwa na wanyama wakali.

✍🏾Baada ya mifano hiyo, je pesa inakabiliwa na mchwa wa aina gani? Kila mmoja anafahamu matumizi yanayopelekea pesa yake isiongezeke au kukaa kila anapopata pesa. Kupitia neno la tafakari ya leo naomba kila mmoja kwa wakati wake arodheshe vyanzo vikuu vinavyopelekea upotevu wa pesa yake. Kwenye kila chanzo ainisha umuhimu wake katika kufikia kwenye malengo makuu ya maisha yako. 

✍🏾Baada ya kukamilisha zoezi hilo hakikisha pesa yako unailinda dhidi ya michwa ambayo haina mchango chanya katika kufikia mafanikio unayotamani. Hapo sasa ndipo unatakiwa kuanza kuishi maisha mapya na kuepuka tabia zilizokuwa zinavujisha pesa yako. Kumbuka pesa inahitaji kupendwa na isipopendwa kupitia kanuni muhimu za pesa itarudi kule inakopendwa zaidi.

✍🏾Mwisho, neno la tafakari ya leo linatukumbusha kwamba kila shilingi tunayopata ina haki ya kutumiwa vyema ili kukuza kipato chetu zaidi. Ikiwa kila shilingi inayoingia mikononi mwako unaitumia yote bila kujali inaelekezwa kwenye matumizi yapi hakika kila mwaka utaendelea kuwa na pato lile lile. Hakikisha unapata nakala ya uchambuzi wa kitabu cha Rules of Money ambacho utapata kanuni 107 kuhusu pesa. 

👐🏾Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 BON TO WIN ~ DREAM BIG 

🗣🗣 Mwalimu Augustine Mathias 
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(