UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Tumia Aina 3 Za Kipato Kukuza Utajiri Wako

NENO LA SIKU_MACHI 10/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Tumia Aina 3 Za Kipato Zitakazokuza Utajiri Wako

Habari rafiki yangu na mfuatuliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri. Hongera kwa kuwa na siku bora, siku ambayo naamini imekuwa chachu ya kukusogeza kwenye kilele cha mafanikio unayotamani.

Tumia dakika kadhaa kufanya tathimini jinsi ambavyo umetumia siku hii ukilinganisha na matamanio ya ndoto za maisha yako.

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

Karibu katika makala ya leo ambayo ni mfululizo wa mafundisho kuhusu jinsi ambavyo unaweza kutengeneza utajiri wa ndoto zako. 


Ifahamike kuwa hauwezi tajiri kama hauna chanzo chochote cha kujiingizia pesa. Hivyo, ili ukimbie katika safari ya kutengeneza utajiri wa ndoto zako huna budi kujua aina mbalimbali za vipato.

Unapojua aina mbalimbali za vipato ni rahisi kuweka malengo ya kifedha kwa siku zijazo na kuhakikisha unatumia pesa zako kwa kuzingatia malengo maalumu ya maisha yako. Watu wengi hudhania kuwa kuna njia moja ya mapato ambayo ni ujira, mishahara au kamisheni, japo zipo njia nyingine nyingi za kupata pesa kupitia njia mbadala na endelevu. 

Je, nini maana ya kipato? Kipato ni pesa ambayo mtu binafsi au kampuni inapata kwa kubadilishana na kazi, ujuzi, bidhaa, huduma au mtaji wa uliowekezwa. 

Kwa kawaida kundi kubwa la watu hupata kipato kupitia ujira au mshahara, huku wengine wakipata kipato kupitia faida inayotengenezwa kwenye biashara (kuuza bidhaa au huduma kwa gharama ya juu ikilinganishwa na gharama uliyotumika kununua au kuzalisha bidhaa au huduma husika). 

Pia, ni muhimu kuelewa kuwa aina nyingi za vipato japo siyo zote hukabiliwa na tozo au kodi mbalimbali za Serikali, maana Serikali hupata kipato chake kwa kutoza kodi. 

Je, zipo aina kuu ngapi za mapato? Kuna aina kuu tatu za kipato ambazo ni: 

Pato hai (active/earned income) - Ni aina ya kipato ambacho hupatikana kadri unavyofanya kazi. 

Ni malipo yanayotokana na matumizi ya muda, nguvu au ujuzi wako kwenye sehemu yako ya kazi. 

Hivyo, kipato chako kinatokana ujira, mshahara au kamisheni kwenye kazi unayofanya no dhahiri kuwa unaangukia katika kundi hili la kipato. 

Hii inamaanisha kuwa unabadilisha muda, nguvu, akili au ujuzi wako na kipimo cha mshahara unaolipwa. 

Ni pato ambalo hupatikana kadri unavyofanya kazi na husipofanya kazi unakosa pato hili. 

Kwa mfano, ikiwa unafanya kazi kama Afisa kwenye taasisi ya Serikali, pesa unazolipwa kila mwisho wa mwezi kama mshahara ambao umekokotolewa kama malipo ya muda na ujuzi wako katika cheo hicho. 

Mifano mingine ya mapato hai ni pamoja na: 
  • Kazi ya huduma kwa wateja
  • Ubunifu wa wavuti, 
  • Udereva (Boda boda, Bajaji n.k)
  • Ubunifu wa picha au uchoraji
  • Kufundisha 
  • Kazi za ujenzi 
  • Biashara ambayo inahitaji uwepo wako

Pato endelevu (Passive Income). Ni kundi la mapato ambayo hutokana na kukodisha mali, ushirikiano wa kibiashara ambao mwekezaji hashiriki moja kwa moja kwenye uendeshaji au pato kutokana na haki za mifumo ya biashara.


Mtiririko wa mapato katika kundi hili kwa kawaida huhitaji uwekezaji wa mapema na baada ya uwekezaji huo kipato uendelea kuingia kulingana na aina aina ya uwekezaji.


Kwa ujumla, kundi hili linajumuisha mapato ambayo hupatikana kwa mtiririko maalumu ambao chanzo chake siyo mwajiri.


Ni pato ambalo hutokana na uwekezaji katika maeneo yenye uwezo wa kuendelea kukuzalishia pesa mara baada ya kuwekeza. Katika kundi hili, mara nyingi malipo ya kodi huwa siyo ya kiwango cha juu ikilinganishwa na mapato katika kundi la kwanza.


Mfano, uwekezaji kwenye majengo ya biashara ni aina ya chanzo cha mapato ya katika kundi hili. Mifano mingine ya mapato katika kundi hili ni kama vile:- 

  • Kuwa mbia katika kampuni

  • Malipo kutokana na Hatimiliki za Kazi za Sanaa au Kitabu

  • Mitambo ya kukodisha

  • Pensheni za wastaafu ambazo hulipwa kila mwisho wa mwezi 

  • Malipo ya kwenye mitandao kupitia tovuti au blogi


Pato tulivu (Portfolio income) - Ni kundi la mapato ambayo hutokana na uwekezaji wa mtaji kama vile gawio, riba, mrahaba na faida kubwa. 

Kwa mfano, unaweza kununua hisa za Kampuni kwa bei ya chini na kuuza hisa hizo kwa faida pale zinapoongezeka thamani. Faida unayopata ni pato ambalo linaangukia kwenye kundi la mapato tulivu. 

Katika makala zilizopita nilielezea aina pato hili kama pesa inayopatikana kutokana na pesa kujizalisha yenyewe (pesa inakufanyia kazi). 

Mifano mingine ya mapato katika kundi hili ni kama vile:- 
  • Kuwa mbia katika kampuni
  • Kufungua akaunti ya akiba ili hupate riba kwa muda
  • Uwekezaji katika Dhamana za Serikali au Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja
  • Malipo kutokana na Hatimiliki za Sanaa au Kitabu
  • Kununua na kuuza rasilimali kwa faida (mashamba, viwanja, mitambo, madini, nyumba n.k)

Hitimisho. Ni muhimu kuelewa aina za mapato ili uwe kwenye nafasi nzuri ya kufanya maamuzi sahihi, kuchunguza fursa za uwekezaji na kupanga mustakabali sahihi wa pesa zako. 

Pia, unapofahamu aina mbalimbali za vipato ni rahisi kuchagua njia mbadala za kupata pesa kwa muda mrefu kutokana na uwekezaji wa mtaji. 

NB. Wasiliana nami kwa ajili ya kupata mwongozo kwenye masuala ya udhibiti, bajeti na uwekezaji wa pesa zako kupitia WhatsApp +255 786 881 155.


WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.

Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.


onclick='window.open(