UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Jifunze Kuhusu Uwekezaji Kwenye Dhamana za Serikali

NENO LA SIKU_MACHI 05/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Jifunze Kuhusu Uwekezaji Kwenye Dhamana za Serikali
Habari ya wakati huu rafiki yangu na mfuatuliaji wa masomo ya mtandao wa Fikra za Kitajiri. Naamini umekuwa na siku bora kwa kuwa umefanikisha ushindi mdogo mdogo ambao ni msingi wa kutimiza ndoto za maisha yako.

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

Karibu katika makala ya leo ambapo tutajifunza kuhusu fursa ya uwekezaji kwenye Dhamana zinazotolewa na Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Makala hizi ni mwendelezo wa masomo muhimu kuhusu udhibiti wa pesa zako na jinsi ya kuwekeza kiasi unachojilipa au kutenga kwa ajili ya uwekezaji. 


Je, uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali unamaanisha nini? Dhamana za Serikali (Hati Fungani) ni utaratibu wa Serikali kukopa pesa kutoka kwa umma kwa makubaliano maalumu ili kuendesha shughuli za maendeleo. 

Hivyo, dhamana za Serikali nchini Tanzania ni aina ya mikopo, ambapo serikali huweka dhamana kabla ya kukopa kwa wawekezaji kama ilivyo mikopo katika taasisi nyingine (ili ukopeshwe ni lazima uwe na dhamana). 

Aina za uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali. Kwa hapa Tanzania, uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali umegawanyika katika makundi mawili;
Dhamana za muda mfupi (Treasury bills au T. Bills)
Dhamana za muda mrefu (Treasury Bonds au T. Bonds)

Dhamana za muda mfupi (Treasury bills au T. Bills). Hizi ni dhamana za Serikali ambazo zinaiva ndani muda mfupi (ndani ya mwaka mmoja). 

Dhamana hizi hutolewa na Serikali kwa lengo la kupata fedha za kukidhi matakwa ya kibajeti au kukabiliana na mapungufu ya fedha kwa haraka. 

Dhamana hizi hutolewa na serikali kwa kubadilishana na fedha zilizokopwa kwa umma. 

Mwekezaji anapata riba au faida pale uwekezaji wake unapofikia kipindi cha kuiva. 

Kipindi cha kuiva kea Dhamana za muda kimegawanyika katika makundi manne ambayo ni; siku 35, siku 91, siku 182, na siku 364. 

Hati fungani za muda mfupi kwa kawaida huuzwa kwa bei chini ya Tshs. 100 na baada ya kuiva mwekezaji hulipwa Tshs. 100. 

Hivyo, faida hutengenezwa kulingana na bei ambayo mwekezaji alinunulia. 

Mfano, kupitia mnada ikiwa ulitoa ofa ya kununua dhamana moja kwa Tshs. 80, baada Dhamana kuiva utapata faida ya Tshs. 20 kwa kila Dhamana uliyonunua. 

Kiwango cha chini cha kuwekeza katika hati fungani ni shilingi Tshs. 500,000. 

Dhamana za muda mrefu (Treasury Bonds au T. Bonds). Dhamana za muda mrefu ni zile ambazo huchukua kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja kuiva. Dhamana hizi hutoa faida baada ya mwaka mmoja. 

Dhamana hizi zimegawanywa katika makundi sita kulingana na muda wake wa kuiva; yaani Dhamana za miaka 2, miaka 5, miaka 7, miaka 10, miaka 15, 20 na miaka 25. 

Faida ya Dhamana za muda mrefu hutokana na riba ambayo huwa ni kiwango maalumu kilichopangwa. 

Kiwango cha chini cha uwekezaji katika Dhamana za Serikali za muda mrefu ni Tshs. 1,000,000. 

Je, Uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali hufanyika kwa utaratibu upi? Dhamana za Serikali huwa zinauzwa kwenye masoko mawili, soko la awali (primary) na soko la upili (secondary market). 

Dhamana za katika hatua ya awali huwa zinauzwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye soko la awali kupitia Mfumo Mkuu wa Uhifadhi au kwa Kiingereza Central Depository System (CDS). 

Baada ya kuuzwa kwenye soko la awali kupitia Mfumo wa Zabuni shindani au zisizo shindani, BoT huwa inazisajili kwenye Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE). 

Katika DSE, Dhamana za Serikali huwa zinauzwa kwa mara ya pili ambapo katika hatua hii uhusisha wawekezaji wanaonunua Dhamana hizi kutoka kwa wamiliki wa awali.  

Je, katika Soko la awali Dhamana za Serikali hununuliwa kwa utaratibu upi? Katika Soko la awali Dhamana za Serikali huuzwa kwa kuendeshwa na BoT, ambayo hutumia njia ya minada kuuza Zabuni za ununuzi wa Dhamana. 

Minada hii hufaanyika kila baada ya wiki mbili kwa mfumo wa zabuni za ushindani na zisizo shindani. 

Zabuni za minada hufuata mfumo wa bei mbalimbali, yaani wazabuni (wawekezaji wenye nia ya kununua) huruhusiwa kuleta zabuni nyingi kwa kila dhamana zinazoiva na kuomba kununua kwa bei tofauti. 

Minada hii huwa inafanyika kulingana na kalenda ya mwaka ya mpango wa fedha wa serikali ambao hutangazwa na Benki Kuu ya Tanzania kila mwaka ili kuwawezesha wawekezaji kupanga mipango yao ya uwekezaji. 

Dhamana za muda mfupi hutolewa kwa mara ya kwanza kwa mtindo wa wiki mbili mbili na Dhamana za muda mrefu hutolewa kwa mtindo wa mwezi mmoja mmoja.

Je, Uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali una faida zipi? Miongoni mwa faida za uwekezaji kwenye Dhamana za Serikali ni pamoja na:-

Usalama wa mtaji, uwekezaji huu ni wa uhakika katika kulinda mtaji unaowekezwa maana Serikali haiwezi kukiuka makubaliano na wadai wake wakati wa malipo. Hivyo, uwekezaji huu hauna hatari ikilinganishwa na uwekezaji wa aina nyingine.

Uhamishikaji, Dhamana za Serikali zinaruhusu mwekezaji kuuza Dhamana zake kabla ya muda wake wa kuiva endapo atataka kufanya hivyo ikiwa ana dharura.

Kuongeza nafasi ya kukopesheka, Dhamana za Serikali zinaweza kutumika kama dhamana kwa ajili ya mikopo katika taasisi zinazokopesha.

Faida kubwa, Dhamana za Serikali zina kiwango cha faida inayoridhisha ikilinganishwa na aina nyingine za uwekezaji.

Je, Naweza vipi kushiriki kwenye mnada wa kununua Dhamana za Serikali? Ushiriki katika Minada ya Dhamana za Serikali upo wazi kwa Wakazi wote katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Wawekezaji wanaweza kuwa; mtu binafsi, taasisi, kikundi au mtoto. 

Kabla kushiriki katika minada ya Dhamana za Serikali, wawekezaji wote wanatakiwa wasajiliwe katika Mfumo wa Usajili wa Washiriki wa Benki Kuu ya Tanzania. 

Usajili huu huwa unafanywa kupitia Mawakala ambao ni benki zote ambazo zenye leseni ya kufanya biashara ya benki inayotolewa na Benki ya Tanzania pamoja na Mawakala (brokers/dealers) waliosajiliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA). 

Ili usajiliwe kushiriki minada hii unatakiwa:-
  • Vielelezo vya utambulisho;
  • Picha mbili za rangi za pasipoti za hivi karibuni; na
  • Hati ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)

Je, nitajua vipi kuna mnada wa Dhamana za Serikali? Benki Kuu ya Tanzania hutoa mwaliko kwa wawekezaji watarajiwa kuleta zabuni zao kwa mnada husika kwa njia ya Tangazo la Zabuni. 

Tangazo la Zabuni huchapishwa katika magazeti siku ya Ijumaa na kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania ukurasa kwenye (CDS Web POrtal). 

Mchakato wa zabuni unaanza mara tu baada ya Tangazo la Zabuni kuchapishwa na huendelea hadi saa 5.00 asubuhi siku ya mnada, ambayo kwa kawaida ni huwa Jumatano.

Je, mchato wa Zabuni huwa unaendeshwa kwa utaratibu upi? Baada ya kusajiliwa kushiriki mnada, unatakiwa kujaza fomu ya zabuni ya kuomba kushiriki katika mnada. 

Fomu iliyojazwa vizuri huwasilishwa kwa Mawakala. Mawakala huchukua maelezo yote na kuyaweka kwenye mfumo wa wawekezaji (CDS) na kuyawasilisha Benki Kuu ya Tanzania kwa njia ya mtandao. 

Ili kuamua bei ya zabuni kabla ya kushiriki, unashauriwa kufuatilia mwenendo wa bei za minada ya dhamana za serikali au kutumia huduma za washauri wa masuala ya kifedha au kupata mwongozo kutoka kwa mawakala hao.

Baada ya mchato wa mnada kukamilika, matokeo hutolewa kwa wastani wa saa moja baada kumalizika kwa mchakato wa kununua zabuni siku hiyo hiyo ya mnada. 

Wawekezaji walioshinda katika mnada husika hutakiwa kulipia ndani ya siku moja ya kazi baada ya mnada, yaani si zaidi ya siku ya Alhamis.

Hitimisho, Uwekezaji katika Dhamana za Serikali ni fursa nyingine ya uwekezaji nchini Tanzania. 

Taasisi za Benki na Matajiri walio wengi wanatumia fursa kuzalisha pesa zaidi tena bila ya kuwa na wasiwasi. 

NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi kuhusu gani unaweza kuwekeza pesa zako. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.

WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.

Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

onclick='window.open(