NENO LA SIKU_MACHI 03/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Muujiza Wa Riba Jumuishi!
Habari rafiki yangu na hongera kwa kuendelea kujifunza kupitia maarifa yanayotolewa na mtandao wa Fikra za Kitajiri. Naamini umekuwa na siku bora kiasi ambacho umefanikisha mambo ya msingi yaliyoainishwa katika ratiba yako ya leo.
Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA
Karibu katika makala ya leo ambapo tutajifunza jinsi gani unaweza kutumia 'muujiza wa riba jumlishi' kukuza utajiri wako.
Kama ni mara ya kwanza kusoma makala hizi, nashauri upitie makala zilizopita maana kuna madini ya thamani ambayo yatabadilisha maisha yako ikiwa hata hivyo utaamini kuwa inawezekana kisha ukachukua hatua stahiki.
Nitaanza kwa kuelezea maana ya neno 'riba' katika mtazamo wa uwekezaji.
Riba ni ongezeko la thamani ya pato lililowekezwa (Kianzio au 'Principal') ambalo hulipwa kulingana na aina ya uwekezaji kama vile katika uwekezaji wa masoko ya mitaji kama dhamana za Serikali, Uwekezaji wa Pamoja, Hatifungani au Hisa.
Kulingana na aina ya uwekezaji, riba inaweza kulipwa mara kadhaa kwa mwaka (kila mwezi, robo mwaka au nusu mwaka) au mara moja kwa mwaka.
Je, Riba Jumuishi (Compounding interest) ni nini? Riba jumuishi au limbikizi kadri utakavyopenda kuibatiza ni pale pato la riba unalopata kupitia uwekezaji linawekezwa tena hivyo kukuletea riba zaidi.
Hii ndiyo maana halisi ya msemo, "Pesa hutengeneza pesa, na pesa inayotengenezwa huendelea kutengeneza pesa zaidi na zaidi".
Riba jumuishi huharakisha ukuaji wa akiba na uwekezaji wako kwa wakati kutokana na kila shilingi inayoongezeka kama riba hutumika kuzalisha shilingi zaidi.
Ikiwa unahitaji pesa ikufanyie kazi kwa maana pesa ijizalishe yenyewe, basi riba jumlishi itatenda muujiza huo katika maisha yako.
Muhimu! Katika uwekezaji naendelea kukumbusha kuwa hakuna pesa ya bure au pesa ya haraka.
Ikiwa unahitaji muujiza wa pesa jumlishi ni lazima kwanza uwe na malengo ya muda mfupi, kati au mrefu.
Faida zaidi ya riba jumlishi utaipata ikiwa una malengo ya kuanzia muda wa kati (miaka mitano) na muda mrefu (miaka kumi na kuendelea).
Pia, kadri unavyowekeza kiasi kikubwa ndivyo pesa yako itazalisha pato kubwa zaidi.
Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa mwenye mtaji kidogo hatonufaika na riba jumlishi, hapa nasisitiza umuhimu wa kuwa na malengo hai ya uwekezaji. Unataka kufanikisha nini kupitia uwekezaji wako?
Jambo la msingi: Ili riba jumlishi ikutendee muujiza unatakiwa kuwekeza kiwango fulani cha pesa kwa wakati mmoja kulingana na uwezo wako au mpango wako wa uwekezaji.
Wekeza pesa hiyo katika akaunti ambayo umejiridhisha kwenye usalama wake na kisha chagua pesa inayozalishwa kama riba iendelee kujimbilikiza (reinvest).
Pia, bado unaweza kuendelea kutumia akaunti hiyo kuwekeza pesa kila mara kulingana na utaratibu wako wa kujilipa kwanza (hii itategemea na sehemu ambako umefungua akaunti yako ya uwekezaji au aina ya uwekezaji).
Kadri riba inavyolipwa ndivyo kiwango ulichowekeza kinaongezeka zaidi.
Je, muujiza wa riba jumlishi unatokea wapi? Unapowekeza pesa kwa mara ya kwanza (Kianzio), baada ya muda wa malipo ya riba (I) kiasi kilichowekezwa huongezeka kwa asilimia fulani (riba) ya kiasi kilichowekezwa (K + I).
Malipo ya riba yanayofuatia hukokotolewa kwa kiwango kilichoongezeka awali kwenye kianzio na riba mpya ya wakati huo [(K+I)+I] na mtiririko huo huendelea hivyo mpaka mwisho wa malengo ya uwekezaji wako.
Hivyo, kila mara mchanganyiko wa Kianzio (K) na Riba (I) hutokea wakati wa malipo ya riba mpya kwenye akaunti yako ya uwekezaji, hali ambayo hupelekea pesa kuendelea kujizalisha yenyewe.
Nifanye nini kunufaika na muujiza wa riba jumlishi? Ni rahisi: Ainisha mkakati wa uwekezaji wa pesa unazojilipa au ainisha kiwango cha kuwekeza mara moja (inashauriwa iwe pesa nyingi kiasi).
Pesa hiyo iondoe kwenye mahesabu yako nje ya mpango wa uwekezaji uliokusudia.
Kisha chagua sehemu salama ya kuwekeza pesa zako (kujua sehemu ipi ambayo nakushauri uwekezaji pesa zako, jiunge na program ya pesornal coaching ambapo nitakupa mwongozo wa hatua kwa hatua pamoja na usimamizi kwa kipindi maalumu).
Baada ya kuchagua sehemu ya kuwekeza pesa zako, fungua akaunti kwa kuzingatia taratibu za sehemu uliyochagua. Kisha wekeza pesa zako kwa kuzingatia mpango wako wa uwekezaji.
Acha wataalamu wa fedha (kulingana taratibu za akaunti uliyochagua) wakutendee muujiza wakati huo endelea na shughuli nyingine za kujiingizia kipato zaidi. "Hivyo ndivyo utajiri unavyojengwa."
Mpaka hapo umenielewa kuhusu muujiza wa riba jumlishi? Utanielewa tu! Hebu tupitie mfano huu kwa njia mbili tofauti za ulipaji wa riba kwa kiwango kilichowekezwa.
Njia ya kwanza; John amewekeza jumla ya kiasi cha milioni tano katika akaunti maalumu, akaunti ya uwekezaji ambayo amechagua inatoa riba ya asilimia kumi (10%) kwa mwaka. Je, baada ya miaka mitano John atakuwa na shilingi ngapi kwenye akaunti yake ya uwekezaji?
A = P (1 + I)^n
Ambapo; "A" ni kiwango thamani ya pesa baada ya miaka mitano, "P" ni Kianzio ambacho John amewekeza, "I" ni kiwango cha riba katika desimali (badili asilimia ya riba kwenda desimali), na "n" ni muda ambao John amepanga kuwekeza.
A = 5,000,000 *(1+0.1)^5 = 8,052,550
Njia ya pili, Chukulia John amewekeza kiasi hicho hicho kwenye akaunti maalumu ambayo malipo ya riba hulipwa mara mbili kwa mwaka kiwango cha riba ya asilimia kumi (10%). John atakuwa na shilingi ngapi baada ya miaka mitano kwenye akaunti yake ya uwekezaji?
A = P (1 + r/n)^n*t
Ambapo; "A" ni kiwango thamani ya pesa baada ya miaka mitano, "P" ni Kianzio ambacho John amewekeza, "r" ni kiwango cha riba katika desimali (badili asilimia ya riba kwenda desimali), "n" ni idadi ya malipo ya riba kwa mwaka na "t" ni muda ambao John amepanga kuwekeza.
A = 5,000,000 *(1 + 0.1/2)^2*5 = 8,144,473.134
Hitimisho, kupitia mfano hapo juu kwa njia mbili tofauti unaweza kuona jinsi riba jumlishi inavyotenda muujiza katika ulimwengu wa uwekezaji.
Kama umedhamiria kujilipa kwanza, nakushauri utumie makala hii kufanya maamuzi sahihi katika kuwekeza pesa utakazokuwa unajilipa.
Anza sasa na baada ya mwaka mmoja utanikumbuka kwa kubadilisha maisha yako.
Kumbuka, unaweza kuzaliwa masikini na hakuna dhambi katika hilo, hila kama wewe una nguvu na akili timamu ukifa masikini ni dhambi. Fanya maamuzi haraka!
NB. Husisite kuwasiliana nami ikiwa unahitaji mwongozo zaidi juu ya jinsi gani unaweza kujiunga na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.
WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.
onclick='window.open(