NENO LA SIKU_MACHI 12/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Anzisha Au Miliki Biashara Kama Njia Ya Kukuza Utajiri Wako
Habari rafiki kwa kuendelea kufuatilia masomo ya Mtandao wa Fikra za Kitajiri. Hongera kwa kuwa na siku bora katika maisha yako. Naamini imekuwa ni siku bora kwako kwa kuwa umeitumia kutengeneza ushindi mdogo kwa ajili ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio unayotaka.
Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA
Karibu katika makala ya leo ambapo nitakushirikisha kuhusu umuhimu wa kuanzisha au kumiliki biashara yako kama njia ya kuelekea kwenye maisha yenye uhuru wa kifedha.
Makala hizi ni mwendelezo wa makala ambazo zinakufunulia jinsi gani unaweza kutengeneza utajiri wa ndoto yako kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa. Ikiwa ni mara yako ya kwanza kusoma makala hizi, hakikisha unafuatilia makala zilizotangulia.
SOMA: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Fahamu Jinsi Ya Kukuza Pato Lako
Biashara ni njia mojawapo ya kuzalisha kipato ambayo hutumiwa na watu wengi katika jamii. Linapotajwa neno ‘biashara’ watu wengi hufikiria kuuza bidhaa au huduma za kiwango cha juu na ndio sababu wengi hukimbilia kusema hawana mtaji wa kuanzisha biashara.
Biashara ni kazi au shughuli inayohusisha ubunifu au ununuzi na uuzaji wa bidhaa au huduma kwa faida.
Hivyo, biashara inaweza kuwa kilimo, ufugaji, biashara ya duka, kusambaza bidhaa, uuzaji wa huduma, uongezaji thamani kwenye bidhaa, ufundi, usafirishaji au huduma inayotokana na matumizi ya kipaji kwa utaratibu maalumu wa malipo.
Kwa tafsiri hii, unaweza kuona kuwa: kwa asili kila mtu ni mfanyabiashara hila tunazidiana kwenye viwango na aina za biashara ambazo tunajihusisha nazo.
Kulingana na tafsiri ya biashara hapo juu, unaweza kuona kuwa biashara inahusisha pande mbili kubalishana thamani kwa faida.
Ili biashara ikamilike ni lazima pawepo mtu anayotoa na anayepokea bidhaa au huduma kwa kubadilishana na kitu kingine.
Hivyo, biashara inahusisha ubunifu wa kuzalisha au kununua bidhaa au huduma kwa kuzibalisha na kitu cha thamani chenye faida ikilinganishwa na gharama zilizotumika kubuni, kuzalisha bidhaa au kutoa huduma husika.
Hapa ndipo tunapata neno ‘Mjasiriamali (Entrepreneur)’, ambalo hutumika kujumuisha watu ambao hubuni na kuanzisha biashara mpya na wapo tayari kubeba hatari katika kuanzisha biashara hiyo kwa ajili ya kufurahia manufaa yatokanayo na biashara husika.
Nani anaweza kuwa Mjasiriamali? Kila mtu anaweza kuwa mjasiriamali kwa kubuni na kuanzisha biashara kwa ajili ya kujiongezea kipato. Ikiwa unahitaji kukuza utajiri wako hakuna namna nyingine zaidi ya kuhakikisha unabuni na kuanzisha au kununua bidhaa au kutoa huduma kwa faida.
Matajiri wengi ambao unawafahamu hapa Tanzania au Duniani kote, wengi wamepata utajiri huo kupitia ubunifu na uzalishaji wa bidhaa au huduma kulingana na mahitaji katika soko.
Pia, ukifuatilia zaidi matajiri wengi utagundua kuwa wengi wametengeneza utajiri wao, kwa maana, walianzia hatua za chini kabisa mpaka kufikia viwango vya kujulikana na kuliteka soko.
Hitimisho. Je, umewahi kutamani kuanzisha au kumiliki biashara yako? Kama jibu ni ndiyo, fahamu kuwa unaweza kuwa tajiri wa kesho ikiwa umedhamiria kufuata misingi ya kutengeneza utajiri.
Tukutane katika makala ijayo ambapo nitaendelea kukufunulia maarifa muhimu kuhusu biashara kama msingi imara wa kukuza pato lako.
NB. Wasiliana nami kwa ajili ya kupata mwongozo kwenye masuala ya udhibiti, bajeti na uwekezaji wa pesa zako kupitia WhatsApp +255 786 881 155.
WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI
Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.
onclick='window.open(