Siku ya Wanawake Duniani: Mwanamke Imara, Maadili Imara Na Uchumi Imara

NENO LA SIKU_MACHI 08/2022: Siku ya Wanawake Duniani: Mwanamke Imara, Maadili Imara Na Uchumi Imara


Hongera kwa akina mama wote ambao mnasherekea siku ya Wanawake Duniani. Hongera pia kwa akina baba wote ambao mmefanikiwa kupata mama bora na imara kutoka katika kundi la Wanawake wote wanaosherekea katika siku hii ya leo.

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

Hakika Wanawake wote mna kila sababu ya kusherekea maana kupitia ninyi Dunia imejazwa maelfu na maelfu.  

Karibu katika makala ya leo ambapo tutajifunza machache kuhusu upekee wa akina mama katika kuelekea kwenye jamii yenye Maadili imara na Uchumi imara. 

Nianze makala hii kwa kukumbushia msemo ambao umezoeleka katika jamii, "nyuma ya mwanaume aliyefanikiwa kuna Mwanamke shupavu". 

Katika makala hii nitauboresha msemo huu ili uwe na uwanda mpana katika kile ambacho nimedhamiria kukushirikisha kupitia makala hii. 

Kupitia makala hii ningependa tutazame mchango wa Wanawake katika familia na jamii kwa ujumla, hivyo msemo huu utasomeka, "Nyuma ya jamii yenye mafanikio kuna Wanawake shupavu".

Ukweli ni kwamba, Mama imara ni kiini cha Maadili bora na kila aina ya mafanikio ndani ya familia na jamii kwa ujumla. 

Mwanaume yeyote ambaye umefanikiwa kumpata mwenza bora huna budi kumshukuru Mungu, maana kupitia mwenza huyo una uhakika wa kuwa na kizazi bora pamoja na uchumi imara. 

Hata hivyo, wanaume wengi wanashindwa kunufaika na wake zao kwa kuwa wanashindwa kubeba majukumu ya kichwa cha familia. 

Mama bora anatengenezwa kupitia baba bora, kwa maana mwanaume una wajibu wa kuhakikisha mkeo anafuata misingi na kanuni za maisha ambazo wewe ni muumini wa Kanuni hizo na unaziishi katika maisha yako ya kila siku. 

Ikiwa baba ni muumini wa maadili bora ndani ya familia ni dhahiri kuona familia yenye mama mwenye maadili na watoto wenye maadili bora.   

Ieleweke kuwa baba kuitwa kichwa cha familia siyo kwa lengo la kulazimisha kila kitu ndani ya  familia bali! Baba unakuwa kichwa cha familia endapo una maono ya familia yako kimaadili na kiuchumi. 

Ikiwa baba una maono ya familia kwenye sekta uchumi ni dhahiri kuwa hata mama atakuwa na maono hayo. 

Hata hivyo, mama atakuwa na maono ya kiuchumi ya mwenza wake ikiwa baba huwa anamshirikisha na kuhakikisha kila mmoja wenu anahusika na kuchangia kwenye ukamilisho wa malengo hayo hatua kwa hatua. 

Familia nyingi zinashindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana na tabia ya kutengenisha malengo ya kifedha, yaani, baba anakuwa na malengo yake na mwenza wake ana malengo yake. 

Wakati baba anaangaika kufikiria jinsi gani atafanikisha ujenzi wa nyumba bora, mwenza wake anawaza kujenga kwao. 

Wakati baba anawaza kukusanya mtaji, mama anawaza kununua kila toleo la nguo. 

Wakati baba anawaza ada za wanafunzi, mwenza wake anawaza kusuka nywele mtindo wa elfu sabini!

Haya ndio maisha halisi ya familia  nyingi katika jamii tunayoishi. Familia zenye malengo yenye umbo 'msambamba' au kwa lugha ya wenzetu tunasema 'parallel goals'. 

Malengo msambamba katika familia ni kirusi ambacho kimeendelea kuzalisha familia nyingi katika kundi la pato la Kati au chini ya msitari wa umasikini. 

Ikiwa mnahitaji kukimbia badala ya kutambaa katika malengo ya kifedha, baba na mama mnalazimika kuwa na malengo ya pamoja ya kifedha. 

Mnahitaji kuondoa kirusi cha kutengenisha pato la kila mmoja wenu kulingana na sehemu ilikotoka, hakuna pesa ya baba au pesa ya mama badala yake iwe 'pesa ya familia'.

Je, kwa nini akina mama wengi huwa ni wasiri kwenye pato lao? Suala la jamii kuwa na akina mama wengi kuficha pato lao kwa wenza wao lipo wazi katika jamii yetu. 

Hali hii hufikia hatua ya kutegeana kwenye majukumu, unakuta mama ana akiba ya hela nyingi ambayo mme wake hajui chochote, lakini huyo huyo anaendelea kuomba hela kwa mme wake kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya malengo yake binafsi na familia. 

Rafiki! Kama familia yako ni miongoni mwa familia za aina hii, huna budi kujiuliza kwa nini mmefikia hatua hiyo. 

Ukweli ni kwamba, Wanaume wengi kutokana na tabia ya usiri wa pato lao kwa wenza wao wamepelekea  Wanawake kuona kuna haja ya kuanzisha biashara au kukusanya pesa ambazo hazitakiwi kufahamika waume zao. 

Katika jitihada hizo, Wanawake hujiondoa kwenye malengo yote ya kifedha kwa ajili ya familia na kumuangushia baba mzigo wote. 

Pia, wanaume wengine hawana maono ya kifedha, hali ambayo hupelekea kutumia hovyo hela wanazopata.

Hivyo, kwa asilimia kubwa unapoona mke wako hatoi hushirikiano kwenye malengo ya kifedha kwa ajili ya kuinua uchumi wa familia unatakiwa kujihoji ni kwa jinsi gani umechangia hali hiyo. 

Jambo la kwanza katika kufanikisha hilo, ni kuhakikisha mnakuwa na mazungumzo ya mara kwa mara yanayohusu utekelezaji wa malengo yenu ya kifedha. 

Pia, karne hii siyo ya kuishi katika nadharia ya baba ndiye mzalishaji na mmiliki wa pesa, hakikisha mkeo anakuwa sehemu ya uzalishaji na kubajeti pato la familia. 

Sifa moja ambayo akina mama wamejaliwa ni kuwa na uchungu kwenye matumizi ya hovyo hasa kwa pesa ambayo wameitolea jasho. 

Hivyo, mwanaume huna budi kutambua kuwa Mama ambaye anashirikishwa ipasavyo kwenye malengo ya kifamilia, ni chachu (catalyst) ya kufanikisha malengo hayo. 

Nihitimishe kwa kusema, kupata mke bora ni hatua ya kwanza ambayo inatakiwa kufuatiwa na kuishi kama familia moja. Familia nyingi zinajikwamisha kufanikiwa kipesa kwa kuendekeza tabia ya kila mmoja kuwa na mipango yake ya kifedha. 

Ikiwa mmeunganishwa pamoja kimwili, ipo haja ya kuwa na malengo ya pamoja kiuchumi na maendeleo ya familia kwa ujumla katika sekta zote.

NB. Unaposherekea siku ya Wanawake Duniani, ewe mama hakikisha unapata mwongozo wa maisha yenye kuacha alama kwa kujinunulia kitabu cha MAISHA YENYE THAMANI. Hata wewe baba una nafasi ya kumjenga mwenza wako katika picha ya maadili na kiuchumi kwa kadri ya maono yako. Nunua Nakala ya kitabu hiki ili kwa pamoja mjenge familia yenye misingi imara. Nitumie ujumbe kupitia WhatsApp +255 786 881 155.

WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.

onclick='window.open(