UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Nifanye Biashara Gani Ili Kukuza Pato Langu? Sehemu ya Kwanza.

NENO LA SIKU_MACHI 15/2022: UNAHITAJI KUWA TAJIRI? Nifanye Biashara Gani Ili Kukuza Pato Langu? Sehemu ya Kwanza.

Hongera rafiki yangu kwa siku hii ya leo ambayo naamini imekuwa msingi wa kupiga hatua moja kuelekea mafanikio ya ndoto za maisha yako.

Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA

Karibu katika makala ya leo ambayo ni mwendelezo wa kujifunza kuhusu mbinu ambazo zitakuwezesha kukuza pato lako na hatimaye kufikia utajiri wa ndoto zako.

Ni mafundisho ambayo yamedhamiria kubadilisha maisha ya kila mtu ambaye amedhamiria kujifunza na kuweka mafundisho katika vitendo kupitia maisha yake ya kila siku. 

Hakikisha unafuatilia makala zilizopita kwa kutembelea wavuti yetu ya FIKRA ZA KITAJIRI.


Watu wengi wana ndoto za kufanya biashara lakini wanashindwa kuchagua aina ya biashara ambayo itakuwa endelevu na kukidhi mahitaji yao. 

Kwa kukosa mwongozo sahihi wakati wa kuchagua aina biashara, wengi wamejikuta wakianzisha biashara ambazo zinakufa ndani ya muda mfupi. 

Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya biashara zinazoanzishwa huwa zinakufa ndani ya kipindi cha miaka mitano.  

Hata zile ambazo hufanikiwa kupenya kipindi hicho, nyingi huwa zinaendeshwa kwa hasara pasipo kuzalisha faida kinyume na makadirio ya wamiliki wa biashara husika. 

Tafsiri yake nini? Tafiti hizo zinatupa mwanga wa juu ya idadi kubwa ya watu ambao wanaanzisha biashara bila kufanya tafiti za kutosha au kuanzisha biashara katika eneo na nyakati zisizo sahihi. Ndiyo! Pigia msitari maneno eneo na nyakati sahihi.

Katika biashara, eneo na nyakati sahihi ni maneno yanayobeba sifa za soko la biashara unayokusudia kuanzisha. 

Kuhusu eneo sahihi, Siyo kila biashara unaweza kuifanya katika kila eneo. Wengi kutokana na kutokufanya tafiti za kutosha au kwa kuigizia biashara hujikuta wanaanzisha biashara katika maeneo ambayo siyo sahihi kwa biashara husika. 

Tafsiri yake ni kwamba biashara nyingi zinakufa kutokana na kuanzishwa katika soko ambalo siyo sahihi. 

Hivyo, kabla ya kuanzisha biashara unatakiwa kufanya tathimini ya soko. 

Jiulize ikiwa bidhaa au huduma unayotaka kuiweka sokoni kama inakidhi mahitaji ya soko husika. 

Jiulize katika soko hilo bidhaa au huduma yako inalenga kutatua changamoto ipi na kwa kundi lipi. 

Wafanyabiashara wengi huwa wanaangukia kwenye mtego huu kwa kushindwa kutambua soko wanalolenga katika eneo husika. 

Hali hii hupelekea wengi kuingia katika soko na bidhaa au huduma ambazo hazihitajiki kwa wingi kwa vile zinatatua changamoto za idadi ndogo ya watu katika jamii (soko) husika.

Kuhusu nyakati sahihi, hiki ni kigezo kingine cha kulipima soko lako. 

Je, bidhaa au huduma unayotaka kuiweka sokoni inaendana na mahitaji ya wateja kwa nyakati husika? 

Je, mbinu unazotaka kutumia kwenye uzalishaji, mauzo na usambazaji wa bidhaa au huduma husika zinaendana na matakwa ya nyakati husika? 

Teknolojia ibadilika kila siku, biashara ilifanya vizuri miaka mitano iliyopita inaweza isifanye vizuri kwa sasa. 

Mfano, kuna watu mpaka sasa wanakomaa na biashara ya kukodisha CD za filamu au kuingiza miziki kwenye simu, wakati kwa teknolojia ya wakati huu kila mtu anaweza kupata nyimbo au filamu anayotaka kutoka kwenye mtandao. 

Fikiria baadhi ya wafanyabiashara ambao hadi sasa wanakomaa na biashara ya 'internet cafe' wakati ulimwengu wa karne hii asilimia kubwa ya watu wanatembea na huduma hiyo mikononi. 

Fikiria katika karne hii mtu ambaye anaanzisha biashara ya kuuza magazeti wakati asilimia kubwa ya watu wanasomo magazeti kupitia simu janja. 

Ninachotaka hapa ujifunze ni kwamba, kabla ya kufungua biashara hakikisha mbinu za uzalishaji, mauzo na usambazaji zinaendana na matakwa ya nyakati hizi. 

Pia, unatakiwa kubadilisha mbinu za biashara yako au kubadilisha biashara kabisa kadri teknolojia inavyobadilika.

Hitimisho. Kila mtu anaweza kuanzisha biashara lakini siyo biashara zote zitakuwa endelevu. 

Unapoamua kuanzisha biashara husikurupuke kutokana na taarifa za juu kuhusu faida ya bidhaa au huduma husika katika soko. 

Unaweza kuhadithiwa mazuri ya bidhaa au huduma kwenye soko lakini pengine yote uliyohadithiwa yakashindwa kuonekana katika soko unalolilenga. 

Mara zote kabla ya kuweka bidhaa au huduma kwenye soko hakikisha una tafiti za kutosha kuhusu soko hilo.

NB. Wasiliana nami kwa ajili ya kupata mwongozo kwenye masuala ya udhibiti, bajeti na uwekezaji wa pesa zako kupitia WhatsApp +255 786 881 155.


WAHI SASA UJIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MAISHA YENYE THAMANI 

Kitabu hiki bado kinatolewa kwa bei ya OFA kwa kuchangia cha Tshs. 10,000/= tu! Utatumiwa kwa barua pepe au WhatsApp Nakala tete (soft copy) yenye fomati ya Pdf.


Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI

onclick='window.open(