[USHAURI] "KAMWE 3 MAISHANI MWAKO: NJIA YA KUDHIBITI HISIA.

NENO LA LEO (OKTOBA 6, 2020): [USHAURI] "KAMWE 3 MAISHANI MWAKO: NJIA YA KUDHIBITI HISIA.

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya ambayo tunakopeshwa tena kwa ajili ya kuendelea kutoa thamani kwa jamii inayotuzunguka. Ni siku ambayo tunaalikwa kuendelea kujitoa zaidi kwa ajili ya wengine ili kupitia kazi tunazofanya. Basi kila mmoja na aseme hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate kilicho bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐Ÿพ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza njia ya tatu ya kudhibiti hisia 3 za hasira, furaha na huzuni tunapojuimuika na jamii inayotuzunguka. Mwanadamu ameumbwa katika hali ambayo hisia huwa zina nafasi ya kutawala maisha yake. Kwa ujumla tupo jinsi tulivyo kutokana na hisia zinazotawala maisha yetu. Hapa tutaona jinsi ambavyo unatakiwa kudhibiti hisia tatu hasira, furaha na huzuni kwa kutumia neno " kamwe".

✍๐Ÿพ Kamwe husijibu endapo una HASIRA. Hasira ni hisia mbaya kwa mwanadamu ambayo inaweza kumfanya atende jambo ambalo hakuwahi kulifikiria. Katika jamii tunayoishi mara nyingi tunashuhudia ugomvi, marumbano na mauaji ambavyo ni zao la hasira. Yote hayo yanatokea kwa kuwa wengi wetu tunashindwa kuzuia hasira na kujikuta tunafanya vitendo kwa mihemko. Ikiwa una hasira ni vyema ukaondoka kwenye eneo ambalo limepelekea upandishe hasira na katika kipindi hicho jitahidi kutojibu chochote hadi pale hasira zitakapoisha.

✍๐Ÿพ Kamwe husitoe ahadi ikiwa una FURAHA iliyopitiliza. Zipo nyakati ambazo tunajikuta kwenye kilele cha hisia ya furaha. Katika hali kama hiyo wengi wetu huwa tunasahau kila kitu kuhusiana na majukumu yetu ya kila siku au uwezo tulionao. Katika hali kama hiyo unawezakujikuta unatoa ahadi ambayo hata uwezo wa kuitekeleza hauna au pengine utekekelezaji wake ni mgumu. Ili kuepuka makosa kama hayo unashauriwa kutotoa ahadi katika kipindi ambacho upo kwenye kilele cha furaha.

✍๐Ÿพ Kamwe husifanye maamuzi katika kipindi ambacho una HUZUNI. Tumeshuhudia kuona maamuzi ambayo yanafanywa na watu na mwisho wake yanaishia kuwaumiza wao wenyewe au wategemezi wao. Katika kipindi cha huzuni wengi huwa tunaona kana kwamba dunia imesimama, ni katili na hata kukosa tumaini la baadae. Kwenye nyakati kama hizo ni hatari kufanya maamuzi maana yanaweza kugharimu maisha yako kwa ujumla.

✍๐Ÿพ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kudhibiti hisia tatu za hasira, furaha na huzuni. Katika nyakati ambazo upo kwenye hisia hizo ni vyema kutofanya jambo ambalo utakuja kujitia baadae. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika maisha yako yatabadirika. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Jiendeleze katika kila sekta ya maisha yako kwa kusoma vitabu vya mafanikio. Kupata nakala ya uchambuzi wa kitabu unachopenda lipia Tshs. 4,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘๐Ÿพ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(