ππΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Nina imani kuwa Mungu amekupa pumzi kiasi ambacho upo tayari kuendelea na majukumu yako ya leo. Hongera kwa pumzi hiyo na wajibu wangu ni kukumbusha kuitumia vyema kwa kuendeleza bidii ya kufikia mafanikio unayotamani. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza jinsi unavyoweza kugundua kama unelekea kwenye maisha ya umasikini, kipato cha kati au utajiri. Neno la leo linalenga ujifanyie tathimini kwenye yako ya baadae japo tathimini hiyo inatokana na maisha unayoishi sasa. Kumbuka, nimekuwa nikisisitiza kuwa maisha ya baadae bila kama ni maisha ya mafanikio au magumu yana uhusiano mkubwa na maisha unayoishi sasa. Kumbe katika maisha unayoyataka kwa baadae husitegemee muujiza kwa kuwa wewe ndo wa kuyaandaa.
✍πΎ Kigezo cha kwanza cha kugundua kama utakuwa au utaendelea kuwa masikini ni namna unavyotumia pesa zako. Mara nyingi katika jamii inayotuzunguka tumezoea kusikia kuwa masikini ni mtu hasiye kuwa na pesa. Je ni sahihi kuwa kuna mtu hasiye na pesa kabisa? Hapa utagundua kuwa hakuna maisha kwa mtu mwenye nguvu na akili timamu bila ya kuwa na pesa. Ili uishi unahitaji kuwa na pesa kwa kuwa upatikanaji wa mahitaji ya msingi ni lazima uwe na pesa.
✍πΎ Ikiwa unatumia pesa zako hovyo ni wazi kuwa unaandaa maisha ya umasikini wa kudumu. Na utagundua kuwa una matumizi ya hovyo endapo hauna mpango wowote wa matumizi kulingana na pato lako. Wengi wetu hatuwezi kujibu tukiulizwa: Kwa mwezi unapata pato la shilingi ngapi kwenye kila chanzo cha pesa ulichonacho na pato linatumika kwenye matumizi yapi? Kwa ujumla wengi hatuna mpango wa matumizi kwa siku au wiki achilia mbali mpango wa mwezi. Hii ni dalili mbaya katika kuandaa maisha yako ya baadae. Hakikisha kuanzia sasa uwe tayari kujibu swali hili: Je pesa zako huwa zinaenda wapi?
✍πΎ Kigezo cha pili cha kugundua maisha yako ya baadae ni kupitia matumizi ya muda. Kila aina ya mafanikio unayotamani kupata katika maisha yajayo ni lazima husisahu uhusiano wa mafanikio hayo na muda. Matumizi ya muda yana uhusiano na uzalishaji na uzalishaji una uhusiano mkubwa na pato lako. Ndiyo maana mara nyingi tumekuwa tukiambiwa muda pesa na pesa ni muda. Ikiwa haujali matumizi mazuri ya muda moja kwa moja una uzalishaji wa chini na moja kwa moja pato lako liko chini. Hivyo, ikiwa unahitaji kukuza pato lako ni lazima uanzie kwenye matumizi bora ya muda.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza jinsi kugundua hatma ya maisha yako kwa siku za baadae. Tumeona kuwa unaweza kuwa masikini ikiwa kwa sasa unatumia hovyo pesa na muda wako. Andaa maisha yako ya baadae kutoka katika maisha ya sasa kwa kuthamini pesa na muda wako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kuboresha afya ya akili yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 4,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(