KUMBE NDOA ULIYOIZOEA INAWEZA VUNJIKA NA MAISHA YAKAENDELEA.

NENO LA LEO (OKTOBA 30, 2020): KUMBE NDOA ULIYOIZOEA INAWEZA VUNJIKA NA MAISHA YAKAENDELEA.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni nyingine ambayo tumeamka salama na tukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kuendeleza pale ulipoishia jana. Ikiwa ni siku ya pili tangu tumetimiza haki yetu ya msingi ya kuchagua viongozi wa kutuvusha salama katika kipindi cha miaka mitano ijayo tunaendelea kusikilizia maumivu ya kuzimwa kwa mawasiliano ya mitandao ya kijamii. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza juu ya somo muhimu ambalo limetokana na hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuzima mitandao ya kijamii. Leo hii ni siku ya tatu tangu mitandao hii izimwe na maisha mengine yameendelea. Ukweli ni kwamba kizazi cha sasa ambacho kinamiliki simu janja kimeweka ushirika au kifunga ndoa na simu hizo. Kizazi hiki kinatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko inavyokuwa kwenye majukumu mengine ya siku. 

✍🏾 Kuzimwa kwa mitandao hii ya kijamii ni ufunuo kwa wale waliofunga ndoa na simu janja kuwa wanaweza kuishi bila kufuatilia yanayojiri kwenye mitandao ya kijamii. Natambua kuwa zoezi la kuzima mitandao ya kijamii kuna ambao litakuwa limewaathiri kwa asilimia kubwa hasa kwa wale wanaotumia mitandao hii kama jukwaa la kutangaza biashara zao.

✍🏾 Ukweli unabakia kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapoteza muda mwingi kufuatilia mambo yasiyo na tija. Katika kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imezimwa unaweza kuamua kuanza maisha mapya ya kutokuendeshwa kwa rimoti na simu janja yako. 

✍🏾 Yanayojiri kwenye mitandao ya Facebook, WhatsApp au Instagram hayana tija sana ikilinganishwa na majukumu yako ya msingi ambayo umekuwa ukipiga dana dana (trade off) dhidi ya mitandao ya kijamii. Kipindi hiki ni muhimu kwako kupima ufanisi wa kutekeleza majukumu yako ya msingi ikilinganishwa na kipindi ambacho mitandao ya kijamii ilikuwa inaingilia utendaji kazi wako.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza maisha yanaweza kuendelea hata bila ya uwepo wa mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii imekuwa ni chanzo cha kupoteza muda na matokeo yake ni ufanisi mdogo katika kazi. Pia, mitandao hii imekuwa chanzo cha kuvunja mahusiano ya watu wengi, hivyo kuzimwa kwake kwa siku hizi ni fursa ya kutuonesha kuwa tunaweza kuiendesha mitandao hii badala ya mitandao hiyo kutuendesha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(