NENO LA LEO (SEPTEMBA 23, 2020): JE NI KWA KIASI GANI UNAYATOA MAISHA YAKO KWA AJILI YA WENGINE?
๐๐พHabari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi ambayo natumaini wote tumeamka salama tukiwa na nguvu na hamasa ya kuendeleza pale tulipoishia jana. Ni muda kama huu hatuna budi ya kusema asante kwa Muumba kutokana na wingi wa rehema ambazo anazidi kutujalia katika maisha yetu ya kila siku. Basi kila mmoja na aseme hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate kilicho bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍๐พ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya wengine. Jana tuliangalia kuwa kulingana na mwanamafanikio Stephen Covey ili ufanikiwe unatakiwa kuwa mwadilifu dhidi ya misingi ya mafanikio ambayo unaiishi. Katika tafakari ya leo tutaona kuwa nyingine ambayo Stephen Covey anatushirikisha ni “utashi wa kujitoa kwa ajili ya wengine”. Hii ni nyenzo ya pili katika nyenzo 12 ambazo Covey anazitaja kama msingi wa mafanikio kwa mtu ambaye amedhamiria kufanikiwa kimaisha.
✍๐พ Mwandishi anatushirikisha kuwa maisha ya mafanikio yenye misingi halisi ya nafsi yako ni lazima yahusishe nia thabiti ya kuwasaidia wengine kupitia vipaji au kalama ambazo umejaliwa. Muda wote unahitaji kujiuliza ni kipi naweza kuchangia kwa ajili ya kuwanufaisha wengine badala ya kufikiria kunufaisha tu nafsi yako. Unahitaji kujifunza mara kwa mara kwa ajili ya kutambua wewe ni nani na umeumbwa kwa ajili ya kukamilisha kazi gani katika ulimwengu huu.
✍๐พ Katika kujitoa maisha yako kwa ajili ya wengine, muda wote unahitaji kujiuliza maswali matatu; (a) Je ulimwengu unataka nini kutoka kwangu? (b) Je mimi ni mzuri katika sekta au kazi ipi (vipaji au kalama zipi unazo)? na (c) Je nawezaje kufanya vyema kwenye kazi nizipendazo katika sehemu yangu ya kazi na hatimaye kufanikisha matakwa ya jamii inayonizunguka?.
✍๐พ Hata hivyo, kabla ya kufikiria kuwaongoza wengine unahitaji kwanza kujiongoza mwenyewe. Hii inamaanisha kwamba unahitaji kubadilisha sehemu zote za maisha yako ambazo zinaenda kinyume na uadilifu ambao ndio unabeba maadili mema. Jikomboe kwanza kabla ya kufikiria kuwakomboa wengine, huu ndio msingi wa kujitoa kwa ajili ya wenzako.
✍๐พ Kumbe, unapodhamiria kujitoa sadaka ni lazima kwanza ubebe majukumu ya maisha yako badala ya kutegemea mtu flani atahusika nayo. Hali inaondoa nafasi ya kulalamikia wengine na kutambua kuwa kabla kulaumu wengine unapaswa kujilaumu mwenyewe pale unaposhindwa kufikia malengo. Pamoja na hilo katika kuishi maisha ya kujitoa kwa ajili ya wengine ni lazima uwe tayari kulipa gharama kwa ajili ya kuwa mtu yule unayetamani kuwa (mwadilifu).
✍๐พ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa maisha ya mafanikio yanahusisha kujitoa nafsi yako kwa ajili ya wengine. Moja, kipimo cha mafanikio ya kiroho ni jinsi unavyowapenda wengine sawa na unavyoipenda nafsi yako. Hivyo, pamoja na kupambana kwa ajili ya kufanikiwa kimaisha tunakumbushwa kuwa mafanikio hayo hayana thamani kama yatajikita kwenye nafsi yako pekee. Fanyia kazi mafundisho haya ili maisha yako yawe na thamani kwako na jamii inayokuzunguka. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Neno la tafakari ya leo limeandaliwa kutoka kwenye uchambuzi wa Kitabu cha “Primary Greatness” kutoka kwa mwandishi mahiri Stephen R. Covey” Hakikisha unajifunza zaidi kuhusiana misingi 12 ya maisha ya mafanikio kwa kujipatia nakala ya uchambuzi wa kitabu kwa gharama Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
๐๐พ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(