NENO LA LEO (OKTOBA 22, 2020): HUU NDIYO UTATU UNAOTAFUNA BIASHARA YAKO
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku ya kipekee ambayo tumepewa kibali cha kuendelea kutoa thamani kwa wanaotuzunguka na viumbe vyote kwa ujumla. Tuendelee kutumia uhai huu kwa faida kwa kuwa wote hatujui mwisho wetu ni lini na siku hizo za mwisho zitawadia kwa njia ipi. Basi tuianze siku kwa kusema "hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani."
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza makosa matatu ambayo yanafanywa na wafanyabiashara wengi. Tafiti zinaonesha kuwa biashara nyingi (80%) zinazoanzishwa huwa zinakufa ndani ya kipindi cha miaka mitano toka kuanzishwa kwake. Pia, biashara zinazostahimili kuvuka kipindi hiko cha miaka mitano huwa zinaendeshwa kwa hasara na zimedumaa. Je wewe ni miongoni mwa wale ambao biashara yako imedumaa au ilishindwa kupenya kipindi cha miaka mitano? Haya hapa makosa yanayogharimu biashara nyingi:-
✍πΎ Kosa #1: Kutokuwa na utaratibu wa kutunza kumbukumbu. Wamiliki wengi wa biashara huwa wanakosa takwimu muhimu za mzigo unaoingia, mzigo uliotoka, faida iliyotengenezwa na gharama za uendeshaji wa kila siku. Hili ni kosa ambalo linatafuna biashara nyingi kwa kuwa mmiliki anashindwa kujua kama biashara inatengeneza faida au hasara. Hali hii inapelekea kushindwa kutofautisha mauzo ghafi pamoja na mtaji.
✍πΎ Kosa #2: Kukosekana na usimamizi mzuri wa mtaji na faida inayotengenezwa. Biashara nyingi huwa zinaendeshwa pasipokuwa na msimamizi anayewajibika moja kwa moja. Leo dukani yupo, kesho yupo baba na keshokutwa yupo mtoto. Hili siyo kosa ikiwa wote wanafuata misingi maalumu ya uendeshaji wa biashara husika. Ukweli ni kwamba biashara nyingi zinakufa kwa kuwa katika ngazi ya familia unakuta anayeielea vyema biashara husika ni mtu mmoja. Matokeo yake pindi anapoingia mtu mwingine dukani anafanya makosa yanayogharimu ukuaji wa biashara.
✍πΎ Kosa #3: Kutokuwepo mpango wa ukuaji wa biashara husika. Hili ni kosa ambalo linapelekea biashara nyingi zidumae na mwisho wake zitoweke kabisa. Kupitia mpango wa ukuaji mmiliki wa biashara anakuwa na mtazamo wa biashara yake katika vipindi tofauti kwa nyakatza baadae. Pamoja na mambo mengine mpango huu unaainisha namna ya kutafuta masoko mapya, jinsi ya kukuza mtaji na jinsi ya kuwekeza faida inayotengenezwa. Biashara nyingi hazina mpango wa aina hii na matokeo yake zinaendelea kuwa vile siku nenda rudi.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza makosa matatu ambayo yanagharimu ukuaji wa biashara katika mazingira yetu. Yapo makosa mengi hila kwa kuanzia anza kurekebisha hayo kwenye biashara yako ili uone tofauti. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(