FAHAMU MAKOSA 3 AMBAYO WATU WENGI WANAFANYA KUHUSU PESA.

NENO LA LEO (OKTOBA 16, 2020): FAHAMU MAKOSA 3 AMBAYO WATU WENGI WANAFANYA KUHUSU PESA.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya katika ambapo tunaendelea kupata kibali cha kuendeleza yaliyo mema katika siku ambazo tumefanikiwa kuishi hapa Duniani. Ni asubuhi ambayo tunaalikwa kuendeleza bidii katika yale tunayofanya ili kufikia ngazi za mafanikio tunayotamani. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza makosa tatu ambayo yanafanywa na watu wengi kwenye sekta ya pesa. Pesa imekuwa ni kiungo muhimu cha kufanikisha mahitaji muhimu ya maisha ya mwanadamu. Na kwa kuwa kila mwanadamu anahitaji pesa ili kufanikisha maisha yake, kila mmoja anatumia njia anazoona ni sahihi katika kukuza pato lake. Katika kama hiyo watu wengi wanajikuta wanafanya makosa mengi ambayo mara nyingi huwa yanawagharimu. Karibu tuangalie makosa matatu ambayo yanafanyika katika jamii yetu.

✍🏾 Kosa#1: Kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Kosa kubwa ambalo watu wengi wanafanya kwenye safari ya kifedha ni kutegemea chanzo kimoja cha mapato. Unapokuwa na vyanzo vingi vya mapato ni ufunguo wa kuwa huru kifedha kwa kuwa vyanzo vyote haviwezi kukumbwa na changamoto kwa wakati mmoja. Kuna aina tatu za vyanzo vya mapato lakini kati ya hizo wengi wanaangukia kwenye hii: kipato kutokana na kazi (earned income) – hii ni aina ya kipato ambacho kinapatikana pale unapokuwa kazini. Kipato chako kinatokana na kazi unayofanya na unapokuwa haufanyi kazi moja kwa moja hauna kipato. Unakula kulingana na jasho la kazi yako, hatari iliyopo ni pale ambapo ghafla unajikuta hauwezi kufanya kazi kutokana na sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kufukuzwa kazi au ulemavu wa kudumu.

✍🏾 Kosa #2: Kufanya biashara nje ya uelewa au mazingira rafiki kwako. Mafanikio ya kibiashara ni zao la kufanya kitu ambacho unapenda kwa dhati, una msukumo/shauku ya kutosha na katika mazingira ambayo una uelewa wa kutosha au rahisi kujifunza. Kabla ya kuingia kwenye biashara yoyote unatakiwa kujifanyia tathimini inayolenga kupima uelewa, uwezo, vipaji pamoja na madhaifu uliyonayo katika biashara husika. Kufanya biashara ambayo hauna shauku, haupendi au hauna uelewa wa kutosha ni njia ya kujiweka kwenye mazingira ya kutokufanikiwa katika biashara husika. Hali hiyo inatokea kutokana na uwezekano mkubwa wa kuhujumiwa na watu ambao unafanya nao kazi.

✍🏾 Kosa #3: Kuweka Imani kwa watu wasio waaminifu kwenye pesa, biashara au uwekezaji wako. Uaminifu katika maisha ya kila siku haukwepeki kutokana na ukweli kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuishi maisha ya ukamilifu bila kuhitaji mchango wa wenzake. Hata hivyo katika ulimwengu wa pesa tunawajibika kuhakikisha Imani yetu iwe kwa watu sahihi hasa wale ambao ni washirika kwenye masuala ya pesa, uwekezaji au biashara. Wengi wameumia kutokana na kuweka Imani kwa watu ambao siyo sahihi hasa katika usimamizi, utekelezaji na uendeshaji wa biashara au uwekezaji kwa ujumla wake. Uaminifu siyo kitu ambacho kinatokea haraka hasa kwa watu wapya, uaminifu unajengwa kwa muda mrefu kwa kadri unavyofanya kazi na watu kwenye biashara, uwekezaji au manunuzi/mauzo ya aina yoyote. 

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza makosa matatu ambayo yanafanywa na watu wengi kwenye sekta ya pesa. Makosa yapo mengi ambayo yanafanywa kupitia mazoea japo athari yake huwa ni kubwa kwa mhusika kufikia uhuru wa kifedha. Epuka makosa haya katika maisha yako ya kila siku ili kulinda pesa yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 4,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(