[HUSISHANGAE] HIVI NDIVYO UNAWEZA KUONGEZA MUDA WAKO!

NENO LA LEO (OKTOBA 17, 2020): [HUSISHANGAE] HIVI NDIVYO UNAWEZA KUONGEZA MUDA WAKO!

๐Ÿ‘‰๐ŸพHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya na ya kipekee ambayo tunazawadiwa tena katika akaunti ya siku za maisha yetu. Ni siku ambayo tunaongozewa masaa 24 kwa ajili ya kuendelea kutoa thamani dhidi ya jamii inayotunzunguka na viumbe vyote kwa ujumla. Kumbuka wajibu wetu mkubwa katika maisha ya kila siku ni kuibadilisha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍๐Ÿพ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza namna ya kuongeza muda wetu katika kila siku tunayobahatika kuishi. Muda ni rasilimali ambayo watu wote tumepewa sawa kwa maana wote tuna masaa 24 katika siku na siku 7 kwa wiki. Pamoja na kwamba wote tumepewa rasilimali hii kwa vipimo sawa wapo watu ambao wanaona muda hautoshi na wengine wana muda wa kutosheleza kufanya yale ya muhimu katika maisha yao ya kila siku. Kiukweli ni kwamba muda haujawahi kutosha kwa watu wengi kwa kuwa mambo ni mengi kuliko muda wenyewe. Pamoja na kwamba muda ni mchache zipo mbinu ambazo unaweza kutumia ili kuhakikisha unapata muda wa kutosha kutekeleza majukumu muhimu katika siku. Karibu ujifunze mbinu hizo:-

✍๐Ÿพ Mbinu #1: Unaweza kuongeza muda kwa kuamua kupotezea au kusema hapana. Unaweza kuokoa muda wako kwa kupotezea au kusema hapana kwa baadhi ya vitu ambavyo havina tija katika maisha yako. Hapa unahitaji kuwa jasiri wa kukataa kuwa kila sio linalokuja kwenye fikra zako au mbele yako lazima lifanyiwe kazi au siyo kila anayekuja utimize haja zake. Mfano, unaweza kuachana na tabia ya mabishano, kufanya kazi za wengine ambazo sio lazima ufanye wewe, kuangalia vipindi vya TV ambavyo havina tija, kupoteza muda kwenye mitandao, epuka vikao visivyo na tija, na epuka kazi za kujitolea ambazo zimepitiliza. Tabia hizi zinapoteza muda ambao ungeutumia kwa ajili ya kuwa karibu na familia yako au kufanya mambo mengine ambayo ni muhimu.

✍๐Ÿพ Mbinu #2: Wekeza muda wako kupitia maamuzi yako ya fedha. Maamuzi ya fedha unayofanya kwa sasa yana mchango mkubwa wa kuamua hatima ya kipato chako na muda wako kwa siku zijazo. Kabla ya kufanya matumizi yoyote tambua kuwa thamani ya pesa hiyo kwa kesho ni kubwa endapo imewekezwa sehemu sahihi kuliko ikitumiwa sasa. Kutokana na msingi huu unatakiwa kufahamu kuwa kila shilingi unayoitumia kwa sasa ina athari kubwa kwenye nafasi yako ya kifedha kwa miaka ijayo. Hapa unaweza ukajitathimini kwenye matumizi yako ya fedha ambayo siyo ya lazima kama ununuzi wa vocha, magazeti, uvutaji wa sigara, ulevi au matumizi ambayo hayapo kwenye bajeti yako. MUDA UNA THAMANI ZAIDI YA PESA KUTOKANA NA UKWELI KUWA MUDA UKITUMIWA VIZURI UNATENGENEZA PESA AMBAZO ZITAENDELEA KUJITENGENEZA ZENYEWE.

✍๐Ÿพ Mbinu #3: Unaweza kuongeza mudwa wako kwa kugatua madaraka/kazi AMBAZO ZIPO JUU YA UWEZO WAKO AU SIYO ZA KIWANGO CHAKO. Fanya tathimini ya majukumu ya kazi zako za kila siku na kisha jiulize kama kuna ulazima wa kazi zote kufanywa na wewe. Chagua kazi ambazo unaona unaweza kumfundisha mtu wa chini yako azitekeleze kwa niaba yako. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeokoa muda ambao utautumia kufanya mambo mengine. Pia, sehemu nyingine ya kugatua madaraka ni kwa majukumu ambayo yapo nje ya uwezao wako. Mafanikio yanahusisha kujenga timu ya watu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano, hivyo, ili ufanikiwe ni lazima uwe tayari kuamini kuwa kazi yako inaweza kufanywa na mtu yeyote kwa viwango unavyohitaji.

✍๐Ÿพ Mbinu #4: Unaweza kuongeza muda wako kwa kuairisha baadhi ya majukumu pale inapobidi. Watu waliofanikiwa wanafahamu kama endapo kuna ulazima wa kazi husika kukamilishwa kwa sasa au kusubirishwa kwa baadae kwa kutegemea umuhimu wake kwa wakati husika. Kwa ujumla kila kazi au maamuzi unayofanya ni lazima kwanza usome alama za nyakati. Kama alama za nyakati haziruhusu kazi/maamuzi husika kufanyika kwa wakati huo hakuna haja ya kulazimisha kufanya maamuzi hayo na badala yake ni vyema ukasubiria kwa baadae.

✍๐Ÿพ Mbinu #5: Ongeza muda wako kwa kutuliza akili katika mambo yaliyo ya muhimu au yenye tija. Zipo nyakati ambazo utatakiwa kufanya kazi mara mbili zaidi ya ulivyozoea kwa ajili ya kuhakikisha unakamilisha majukumu yaliyopo mbele yako. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali zote unazielekeza kwenye jukumu husika kwa kadri zinavyotakiwa mpaka pale ambapo utaona kuwa umefanikisha kukamilisha jukumu hilo. Hapa unahitaji kuongeza muda wako kwa kuhakikisha unafanyia kazi ambayo ni ya kipaumbele kwa wakati husika na si vinginevyo. Hakikisha haurusu mwingiliano wa vitu vingine ambavyo vinaweza kukupoteza kwenye kipaumbele chako. Pia, katika zoezi la kuongeza muda ni lazima uhakikishe vipaumbele vyako vina muunganiko wa matukio kiasi kwamba kukamilika kwa kipaumbele kimoja kunapelekea kuanza kwa kipaumbele kingine. Pia, kipaumbele kimoja kisaidie kuongeza muda kwa ajili ya kipaumbele kinchofuatia.

✍๐Ÿพ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza mbinu tano ambazo tunaweza kuzitumia kuongeza muda wetu. Ni mbinu ambazo kila mmoja anaweza kuzitumia kwa kuwa ni rahisi kutumiwa katika majukumu yetu ya kila siku. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ๐Ÿ‘‡๐Ÿพ

๐Ÿ‘๐Ÿพ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI ili upate mafundisho haya kila siku, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(