JE NI MARA NGAPI UNAJILAZIMISHA KUTOKA KWENYE UKANDA WA FARAJA?

NENO LA LEO (OKTOBA 19, 2020): JE NI MARA NGAPI UNAJILAZIMISHA KUTOKA KWENYE UKANDA WA FARAJA?

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya katika juma jipya ambapo tunaalikwa kuendeleza yaliyo mema kwa kuwa hayo ndiyo yanayapa thamani maisha yetu. Ni asubuhi leo unakumbushwa kuendelea kupiga hatua kila siku zinazolenga kukufikisha kwenye ushindi unaotamani. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kuukimbia ukanda wa faraja (comfort zone). Kwa asili mwili wa binadamu unapenda raha kiasi ambacho hauko tayari kupokea mabadiliko ya haraka katika mazoea yaliyojengeka muda mrefu. Ni kutokana na hali hiyo watu wengi hawako tayari kuachana na mazingira waliyozoea au tabia zilizozoeleka na kuingia kwenye maisha mapya ambayo pengine hayana uhakika wa baadae.

✍🏾 Mwaka 1975 kijana Bill Gates akiwa na umri wa miaka 19 aliamua kuukimbia mfumo wa maisha uliozoeleka katika jamii. Sawa na ilivyo kwa vijana wengine Bill alilewa katika hali ambayo aliaminishwa kuwa ili ufanikiwe unatakiwa kwenda shule, usome kwa bidii, ufahulu masomo na mwisho wake upate kazi nzuri yenye malipo mazuri. Kijana Bill aliamua kubeba hatari ya kuukimbia mfumo kwa kuachana na masomo ya chuo kikuu katika Chuo cha Harvard.

✍🏾 Kijana Bill katika hali ya kushangaza akiwa hana mtaji wa rasilimali fedha ($0) akaona kuna maisha nje masomo ya chuo (ukanda wa faraja). Pamoja na kwamba kijana Bill hakuwa na mtaji wa fedha kuna vitu ambavyo alikuwa navyo katika ulimwengu wa ujasiliamali. Kubwa zaidi alikuwa na maarifa, taarifa sahihi na alijiamini kuwa anaweza. Kwa sifa hizo, kijana Bill aliungana na mwenzake Allen na kuanzisha kampuni ya Microsoft ambayo ilijikita kwenye kutengeneza "software" za kompyuta.

✍🏾 Kwa misingi ileile ya kuamini kuwa anaweza, leo hii (2020) tunapomzungumzia mzee Bill kampuni yake ina thamani ya USD trilioni moja. Tunaweza kuelezea mafanikio ya Bill Gates katika kila hali tunavyotaka, lakini pointi muhimu ya kukumbuka ni kwamba amefanikisha yote hayo kwa kuwa aliweza kuukimbia ukanda wa faraja katika muda na umri sahihi. 

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kuukimbia ukanda wa faraja katika umri na wakati sahihi. Kila mmoja wetu ana ukanda wake wa faraja ambao unamzuia kufikia mafanikio anayotamani. Jiulize ni ukanda upi wa faraja ambao umeendelea kukuzuia kufika kule unakotamani na kisha jivike bomu kwa kuukimbia ukanda huo.  Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(