[SIKU YA AFYA YA AKILI] JE UNAFANYA NINI KUBORESHA AFYA YA AKILI YAKO?

NENO LA LEO (OKTOBA 10, 2020): [SIKU YA AFYA YA AKILI] JE UNAFANYA NINI KUBORESHA AFYA YA AKILI YAKO?

👉🏾 Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni matumaini yangu kuwa umeamka salama ukiwa na nguvu na hamasa kwa ajili ya kendeleza bidii ya mafanikio. Ni nguvu na hamasa pekee ndivyo vitakufanya uendeleze hali ya kutengeneza ushindi mdogo kwa ajili ya ukamilifu wa malengo makuu uliyojiwekea. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusiana na afya ya akili. Wengi wetu huwa tunaweka malengo kwenye kila sekta ya maisha yetu hila huwa tunasahau kipengele cha afya ya akili. Oktoba 10 ya kila ya kila mwaka Dunia huwa inaadhimisha siku maalumu kwa ajili ya afya ya akili. Tukio hili lilianza kuadhimishwa toka mwaka 1992 ikiwa na lengo la kukabiliana na magonjwa ya akili na athari zake kwa jamii.

✍🏾 Je magonjwa ya akili yanasababishwa na nini? Sehemu mbalimbali kwenye mitandao wameandika kuwa magonjwa ya akili yanasababishwa na muunganiko wa sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu ambazo zimetajwa ni: Sababu za kibaolojia (bilogical factors) kama vile ukuaji (aging) na urithishaji (hereditary); sababu binafsi (personal factors) ambazo zinajumuisha mfumo wa maisha (life style), kujithamini (self-esteem) na mfumo wa malezi; Mazingira ambayo yanajumuisha sehemu ambazo mhusika anaishi pamoja na majirani wanaomzunguka; sababu za kijamii ambazo zinajumuisha mahusiano ya mhusika dhidi ya familia yake, marafiki na makundi ya kijamii katika majukumu ya kila siku; na sababu za kiuchumi ambazo zinajumuisha uwezo wa kipato na hali maisha ya mhusika.

✍🏾 Je unatakiwa kufanya nini ili kulinda afya ya akili? Mwanafalsafa nguli Plato aliwahi kusema kuwa: “kosa kubwa ambalo wanasayansi wanafanya ni kujikita kwenye kutibu afya ya mwili bila kuweka jitihada zozote za kutibu afya ya akili; japo akili na mwili ni kitu kimoja na havitakiwi kutenganishwa”. Hivyo, ikiwa unahitaji kulinda afya ya mwili na akili unatakiwa kufanya yafuatayo:-

✍🏾 Moja, zingatia mfumo bora wa maisha. Hapa unatakiwa kuhakikisha unakula vizuri na chakula chenye virutubisho vyote, pata muda wa kutosha wa kupumzika, fanya mazoezi, epuka matumizi makubwa ya vichocheo (stimulus) vya mwili kama vile cafein, vinjwaji vya kuongeza nguvu (energy drinks), vinjwaji vyenye sukari na vyakula vyenye sukari, na hakikisha unaepuka matumizi ya dawa za kulevya, punguza au acha kabisa matumizi ya vinjwaji vyenye vilevi na uvutaji wa sigara.

✍🏾 Mbili, hakikisha unazungukwa na watu sahihi. Hapa unatakiwa kuhakikisha unaboresha mahusiano bora dhidi ya watu wanaokuzunguka kama vile wanafamilia, wafanyakazi wenzio, majirani na marafiki. Pia, unatakiwa kuhakikisha unakuwa na muda wa kujumuika na kufurahi na marafiki zako au wanafamilia. Pia, katika nyakati ambazo unapitia kwenye ugumu wa maisha kama vile kufukuzwa kazi au biashara haziendi vizuri unashauriwa husipende kukaa peke yako na badala yake hakikisha unazungukwa na watu sahihi ambao wanaweza kukusaidia kuondokana na changamoto inayokukabiri.

✍🏾 Tatu, punguza msongo wa mawazo. Binadamu wengi mara nyingi wanapitia kwenye changamoto za kimaisha ambazo zinawafanya wawe na msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ni kichocheo kikubwa cha magonjwa ya akili ambayo mwisho wake huwa ni magonjwa ya mwili. Unaweza kupunguza msongo wa mawazo kwa kuhakikisha unakuwa na muda wa kutosha wa kupumzika, tenga ratiba ya majukumu yako, pata muda wa kufanya mazoezi, hakikisha unajiamini kuwa unaweza, na pale unapokuwa na ugumu hakikisha unapata mwongozo sahihi kutoka kwa watu wanaoweza kukusaidia.

✍🏾 Nne, jenga mazingira mazuri ya kufanya kazi. Ikiwa umeajiriwa au umejiajiri na kuajiri watu wengine una wajibu wa kuhakikisha sehemu yako ya kazi inakuwa salama kwa kila mmoja anayekuzunguka. Hapa unatakiwa kutekeleza majukumu yako ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwa na muda wa kuzungumza mara kwa mara na mwajiri au waajiriwa wako. Pia, unatakiwa kutenga muda kwa ajili ya kujielimisha mara kwa mara kwenye fani yako sambamba na kupata maarifa mbalimbali kwenye kila sekta ya maisha yako. 

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza jinsi tunavyotakiwa kuweka mkazo wa kulinda afya ya akili sawa na ilivyo kwenye afya ya mwili. Tumeona mbalimbali ambazo tunatakiwa kuzitumia kwa ajili ya kulinda afya ya akili. Tumia mbinu hizi na hakika utakuwa na afya ya mwili na akili pia. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kuboresha afya ya akili yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 4,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(