[USHAURI] VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI KUANZISHA BIASHARA MPYA

NENO LA LEO (OKTOBA 23, 2020): [USHAURI] VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI KUANZISHA BIASHARA MPYA

👉🏾 Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambapo tunazawadiwa masaa 24 katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Wajibu tulionao ni kuendelea kutoa thamani dhidi ya jamii inayotunzunguka na viumbe vyote kwa ujumla. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza maeneo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara mpya. Linapokuja suala la kuanzisha biashara hasa kwa wajasilimali wadogo changamoto huwa ni nyingi. Kwa kutaja tu baadhi katika mazigira yetu huwa ni pamoja na: kukosekana kwa mtaji wa kuanzisha biashara husika, uhakika wa kushindana kwenye soko na uhakika wa wazo bora la biashara. Kupitia neno la tafakari ya leo nitakushirikisha sehemu za kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara yako ili uweze kukabiliana na changamoto hizi.

✍🏾 Tambua hamasa/shauku yako. Kuanzisha biashara ni sawa na kuanzisha familia kutokana na ukweli kwamba unahitaji kuwekeza muda, kufanya kazi kwa bidii pamoja na uwekezaji wa kifedha. Vyote hivi vinahitaji dhamira ya kweli kutoka ndani mwako hivyo kama hauna hamasa/shauku ya kutosha juu biashara husika itakuwa vigumu sana biashara nhiyo kukua. Kwa kifupi ni kwamba unahitaji una pendo wa hali ya juu kwenye biashara yako.

✍🏾 Tafsiri wazo lako kwenye mpango wa biashara. Mpango wako wa kibiashara unakuwa ni dira ya kukuongoza kwa ajili ya kufikia mafanikio unayohitaji. Mpango huu unapaswa kuonesha malengo ya baadae ikiwa ni pamoja na hatua utakazofuata kwa ajili ya kufikia malengo husika. Pia mpango huu kama umeandaliwa vyema unaweza kutumika kwa ajili ya kukuza mtaji kutoka kwa wafadhiri au taasisi za kifedha ikiwa ni pamoja kutumia mpango huu kwa ajili kusambaza bidhaa zako kwenye soko.

✍🏾 Fanya tafiti kuhusiana na wazo lako kama ni wazo sahihi sehemu unayotaka kuanzisha biashara. Kabla ya kuanzisha biashara hakikisha unafanya tafiti juu ya wazo lako la biashara ili uwe na taarifa sahihi zinazoendana na nyakati pamoja na sehemu husika. Taarifa hizi unaweza kuzipata kupitia semina za biashara, sehemu za masoko/biashara zinazozunguka eneo husika, maonyesho ya biashara, sehemu za viwandani au kwenye mitandao ya kijamii.

✍🏾 Tambua wapinzani wako wa karibu kwenye soko. Kwanza unahitaji kutambua kuwa washindani wako kibiashara sio maadui wako bali ni sehemu ya kujifunza mbinu zipi zimefanikiwa na zipi zimeshindwa kufanya kazi. Hii itakusaidia kuboresha mbinu zako kwa ajili ya kutoa huduma ambayo imeboreshwa ikilinganishwa na wapinzani wako. Taarifa za wapinzani wako unaweza kuzipata kupitia kwenye mitandao, semina za biashara, tafiti mbalimbali kuhusu bidhaa/huduma zinazotolewa na wapinzani wako.

✍🏾 Ainisha ni mitandao ipi ya kijamii ambayo unaweza kuitumia kutangaza biashara yako. Tambua umuhimu wa kutumia mindao ya kijamii kama vile facebook na twitter kwa ajili ya kupata taarifa sahihi kuhusu bidhaa/huduma unayokusudia kuitoa. Mitandao ya kijamii ni sehemu isiyo rasmi kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuboresha bidhaa/huduma unayokusudia kuitoa kulingana na wazo lako la biashara. Pia unaweza kutumia mitandao ya kijamii kufahamu mahitaji ya wateja katika soko linalokuzunguka.

✍🏾 Tafuta mwalimu/mshauri wako wa kibiashara. Mshauri wa biashara ni mtu muhimu kwa mtu anayeanzisha biashara kwa kuzingatia kuwa mshauri anakuwa tayari ana uzoefu wa kutosha katika sekta ya biashara. Msahauri huyu anahitaji kumpa mwanga pamoja na mwongozo mjasiliamali anayeanza safari yake ili akabiliane na mawimbi ya kibiashara. Ushauri huu utakusaidia kuepukana na makosa ya kibiashara ambayo yanaweza kupelekea upoteze mtaji wako.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza maeneo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara mpya. Biashara nyingi zinakufa kwa kuwa zinapuuza maeneo hayo wakati wa uanzishwaji wake. Kuwa wa tofauti katika biashara yako kabla ya kuianzisha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(