MOJA YA MAKOSA AMBAYO HUWA UNAFANYA KUHUSU FEDHA.

NENO LA LEO (OKTOBA 14, 2020): MOJA YA MAKOSA AMBAYO HUWA UNAFANYA KUHUSU FEDHA.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya katika siku za uhai wetu ambayo tunakopeshwa kwa ajili ya kuitumia vyema ili mwisho wa uhai wetu tupate kutendewa kulingana na matendo yetu. Ni katika siku hii tunakumbuka siku ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Kama taifa tunaungana pamoja kwenye kumbukizi ya Baba wa Taifa kutokana na mema aliyoyatenda enzi za uhai wake. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza moja ya makosa ambayo yanafanywa na watu wengi kwenye safari ya uhuru wa kifedha. Kila mmoja wetu anahitaji kuwa uhuru kifedha kwa kuwa fedha ni ndiyo msingi wa kufanikisha mahitaji ya msingi kwenye maisha. Kila siku tunaamka asubuhi na kuingia kwenye majukumu ya siku ambayo mwisho wake yanalenga kusaka pesa.

✍🏾 Pamoja na kwamba pesa inatafutwa na kila mtu lakini ukweli ni kwamba watu hao hao hawako tayari kuwekeza muda na pesa kwa ajili ya elimu ya pesa. Kutokuwekeza kwenye elimu ya pesa ni moja ya kosa ambalo linafanywa na watu wengi kwenye jamii na matokeo yake watu wanafanya makosa yale yale ambayo yanaishia kuwagharimu kila siku. Kukosekana kwa elimu ya pesa ni chanzo kikubwa watu wengi kuendelea kuishi kwenye dimbwi la umasikini. Wengi wameendelea kwenye mbio za panya ambazo mara nyingi uishia kwenye kingo za kuta kwa maana ni mbio ambazo hazina mshindi. 

✍🏾 Wengi wamendelea kukimbizana na fursa zenye malisho bora lakini pamoja na kufanikisha fursa hizo wanajikuta bado wanaangaika kifedha. Kwa ujumla, katika maisha muhimu siyo kiwango cha pesa unachotengeneza bali unafanya nini kutokana na pesa unayopata ndilo jambo la muhimu. Hapa ndipo umuhimu wa elimu ya pesa unapoanzia kwa maana elimu ya darasani pekee haitoshi kukukomboa kutoka kwenye umasikini. Wapo watu ambao wamesoma na wanalipwa mishahara mizuri lakini bado wanaendelea kuishi mshahara kwa mshahara.

✍🏾 Kukosekana kwa elimu ya pesa kunapelekea watu wengi kushindwa kuchukua hatua za utekelezaji kwa yale ambayo wanadhamiria kufanya. Kupitia elimu ya pesa ni Dhahiri kuwa tunafundishwa kuwa fursa ya leo haiwezi kuwa fursa ya kesho katika ulimwengu ambao mabadiliko yanatokea kila siku. Moja ya sababu zinazopelekea wengi kutoishi kwa vitendo ni kuendekeza visingizio kwa kuwa kila mara watakupatia sababu zinazoelezea kwa nini hawatekelezi yale wanayokusudia kufanya.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuhusu umuhimu wa elimu ya pesa kwenye safari ya kutengeneza maisha yenye uhuru wa kifedha. Hakikisha haufanyi makosa ya kupuuzia elimu ya pesa kadri unavyoangaika kukuza pato lako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 4,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(