KWA NINI UNASHINDWA KUISHI KULINGANA NA NYAKATI?

NENO LA LEO (OKTOBA 13, 2020): KWA NINI UNASHINDWA KUISHI KULINGANA NA NYAKATI?

👉🏾 Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tunapata muda wa kuendeleza kutenda yaliyo mema. Wajibu tulionao ni kuhakikisha kila siku tunayo bahatika kuishi hapa Duniani inatumiwa kama ngazi ya kufanikisha maisha bora tunayotamani. Ikumbukwe kuwa maisha bora yanapatikana kwa kutoa thamani dhidi ya jamii inayotuzunguka. Basi kwa pamoja tuseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kuishi kulingana na nyakati tunazopitia. Katika neno tafakari ya jana tuliona kuwa hakuna mafanikio pasipo kuwepo uwekezaji. Katika neno la tafakari ya leo tutaona jinsi ambavyo watu wengi wanaendelea kujikandamiza kimaisha kwa kushindwa kuishi kulingana na nyakati wanazopitia. Mchakato wa mafanikio unapitia kwenye hatua mbalimbali ambapo kila hatua mhusika ni lazima atambue jinsi gani anatakiwa kuishi.
✍🏾 Katika jamii tuna idadi kubwa ya watu ambao wanaangaika kimaisha kwa kuwa wanashindwa kuishi kulingana na nyakati. Mfano, fikiria kijana ambaye anaanza maisha baada ya kuhitimu chuo. Katika hali ya kawaida kipindi cha kuanza maisha ni kipindi ambacho uwekezaji wa hali ya juu unatakiwa ili kuweka msingi wa maisha ya baadae hasa kwenye kipato. Ni katika kipindi hiki mhusika anatakiwa kujinyima kwa kadri awezavyo ili bajeti yake isizidi pato lake.
✍🏾 Hata hivyo, kwa vijana wengi hali huwa inakuwa tofauti. Katika kipindi ambacho walitakiwa kuwekeza ndipo wengi wanakula bata mjini. Ndiyo maana ni kawaida ukienda sehemu za starehe utakutana na vijana wengi kuliko wazee. Ni kawaida kuona kijana anaanza kazi leo na baada ya mwezi anachukua mkopo na kununua gari kwa ajili ya kula bata mjini. Kumbuka kijana huyo hana hata kiwanja wala shamba au kijisehemu chochote cha kumuingizia shilingi nje ya mshahara wake. Hali hii inatokea kwa kuwa vijana wengi wameshindwa kuishi kulingana na nyakati za vipindi vya ukuaji wao katika kuelekea kwenye maisha ya mafanikio.
✍🏾 Pia, kupitia neno la leo ningependa utambue kuwa katika nyakati za uwekezaji huwa zinaambatana na magumu ya maisha. Ni katika kipindi hiki chochote unachofanya hakioneshi dalili za kukuletea matunda ya haraka. Ikiwa ni mwepesi hapa ndipo wengi wanarudi nyuma na kuzama kwenye maisha ambayo hayawezi kuwasogeza mbele. Kuna kipindi cha kupanda na kipindi cha kuvuna, wengi huwa wanakimbilia kula matunda nyakati ambazo wanatakiwa kupanda na kumwagilia miche ili izalishe matunda zaidi.
✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa utachelewa sana kufanikiwa kimaisha ikiwa unashindwa kutambua uishi vipi kulingana na nyakati unazopitia. Mafanikio yanaenda kwa wale ambao wanaishi kulingana na nyakati wanazopitia. Tambua upo katika nyakati zipi na anza kuishi kulingana na matakwa ya nyakati hizo. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kuboresha afya ya akili yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 4,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
onclick='window.open(