NENO LA LEO (OKTOBA 20, 2020): SIRI 6 AMBAZO MATAJIRI HAWATAKUAMBIA.
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo tumejaliwa kuwa na pumzi ya bure katika siku za uhai wetu. Ni siku ambayo naendelea kukumbusha kuwa kila siku ambayo unabahatika kuishi ni msingi wa kujenga mlima wa mafanikio katika maisha yako. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza siri sita ambazo matajiri wengi wanazitumia kukuza utajiri wao. Mara ukipata nafasi ya kuongea na tajiri yeyote wengi huwa hawataki kuweka wazi jinsi walivyofanikiwa kuwa na tajiri au jinsi gani wanafanikisha kukuza utajiri wao. Wapo ambao watakukatisha tamaa kuwa kutengeneza utajiri siyo jambo jepesi na ni watu wachache ambao wamebalikiwa kuwa na kariba ya namna hiyo. Pia wapo ambao kwa haraka haraka watakuambia ni rahisi kuwa tajiri bila kukuambia kwa undani unatakiwa kufanya nini ili uwe tajiri. Karibu tujifunze siri 6 ambazo zinatumiwa na matajiri wengi:-
✍πΎ Siri #1: Mshahara pekee hauwezi kukufanya uwe tajiri. Wafanyakazi wengi ambao wanategemea mshahara pekee maisha yao ni kuishi mwezi kwa mwezi (mshahara kwa mshahara). Maana yake ni kwamba kiwango wanacholipwa kupitia mshahara ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kawaida katika maisha. Niliwahi kuandika kuwa wanaopanga viwango vya mshahara huwa wanaweka kiwango ambacho kitamfanya mhusika aendelee kufanya kazi ili apate mshahara. Kama umeajiriwa anza sasa kutafuta kipato cha ziada nje ya mshahara.
✍πΎ Siri #2: Mfumo wa bei ni miongoni mwa wezi wanaoiba utajiri wako. Ni wazi kwamba thamani ya pesa ya leo haiwezi kuwa sawa na kesho kulingana na mabadiliko ya mfumuko wa bei yanayotokea. Ili pesa iendelee kuwa na thamani dhidi ya mfumuko wa bei inatakiwa kuwekezwa sehemu ambapo inaongezeka thamani. Anza kuwekeza sasa.
✍πΎ Siri #3: Nunua vitu vinavyoongezeka thamani (assets) na epuka kununua vikorokoro (liabilities). Hii ni siri kubwa ambayo inatenganisha watu tajiri na watu masikini. Masikini mara nyingi wanajikita kununua vitu ambavyo thamani yake inapungua kwa kipindi cha muda wakidhania kuwa ni rasilimali (assets). Vitu hivyo vinaendelea kuwagharimu kila siku kutokana na gharama za matunzo au uendeshaji. Kinyume chake ni sahihi kwa watu tajiri kwenye kununua.
✍πΎ Siri #4: Epuka kuwa na matumizi yanayozidi pato lako. Masikini mara nyingi wanajiingiza kwenye mikopo kutokana na kuwa na bajeti kubwa inayozidi pato wanaloingiza. Matokeo yake madeni yanaendelea kuwatafuna siku hadi siku. Ikiwa unahitaji kuwa tajiri ni lazima uhakikishe unatumia pungufu kuliko pato lako.
✍πΎ Siri #5: Mara zote jilipe kwanza! Huu ni muujiza mwingine katika ulimwengu wa kutengeneza utajiri. Siri hii inakutaka kuhakikisha kila shilingi inayoingia mikononi mwako utenge asilimia flani (10 - 15) kwa ajili ya kuwekezwa sehemu ambapo inaongezeka thamani.
✍πΎ Siri #6: Muujiza wa ongezeko la riba katika kipindi cha muda maalumu. Ikiwa umewekeza pesa yako sehemu ambayo kila mwaka inaongezeka kwa asilimia flani, baada ya mwaka wa kwanza pesa iliyowekezwa itaongengezeka kwa asilimia inayotolewa na taasisi husika kama ongezeko la riba. Katika mwaka wa pili pesa yako itaongezeka kuanzia kwenye thamani yake ya mwisho wa mwaka wa kwanza. Hali hiyo itaendelea mpaka mwisho wa kipindi cha uwekezaji.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza siri 6 ambazo zitakuza utajiri wako. Anza sasa kwa kuwa kesho huwa haina mwisho. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(