NENO LA LEO (OKTOBA 21, 2020): HII NDIYO NJIA RAHISI YA KUPIMA UTAJIRI WAKO
👉🏾Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya na ya kipekee katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Kipekee kabisa natarajia umeamka ukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendelea kuwa mtu wa thamani kwa jamii na viumbe wanaokuzunguka. Basi tuianze siku kwa kusema "hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani."
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza njia rahisi ya kugundua kama wewe ni tajiri, mtu wa kipato cha kati au masikini. Mara nyingi mtaani linapotamkwa neno utajiri wengi huwa wanakimbilia kwenye tafsiri ya umiliki wa pesa.
✍🏾 Ukweli ni kwamba utajiri ni zaidi ya umiliki wa pesa kwa kuwa utajiri unapimwa kwa pesa taslimu, mali zisizohamishika, mali zinazohamishika, pesa zilizoko Benki au umiliki wa pesa kwenye masoko ya mitaji. Muunganiko wa vyote hivyo ndivyo vinaunda utajiri wa mtu.
✍🏾 Je ntawezaje kujua kuwa mimi ni tajiri? Mwanamafanikio Robert Kiyosaki huwa anasema utajiri wa mtu unapimwa na "idadi ya siku ambazo ataweza kuishi bila kufanya kazi huku akijitoaheleza kwenye mahitaji yake yote bila kuteteleka". Fikiria tukio la ghafla ambalo linakuacha kwenye mazingira ambayo hauwezi kufanya kazi. Katika mazingira hayo ambayo utakuwa haufanyi kazi ikiwa utaendelea kukidhi mahitaji yako ya msingi kwa kipindi cha muda wote utakaoishi basi wewe ni tajiri mkubwa.
✍🏾 Hata hivyo, katika jamii tuna idadi kubwa ya watu ambao ili waendelee kuishi ni lazima wafanye kazi. Huu ni ukweli husiopingika kwa kuwa ridhiki inapatikana kadri mtu anavyojibidisha kila siku. Ridhiki ya wengi ipo mikononi mwao kila siku.
✍🏾 Je nawezaje kuongeza siku za kuishi bila kufanya kazi? Ili uongeze siku ambazo unaweza kuishi pasipo kufanya kazi unalazimika kuweka mazingira ambayo pesa itakuwa inafanyia kazi hata katika kipindi ambacho umelala. Hapa unatakiwa kuweka nguvu kwenye umiliki wa mali zisizohamishika na zinazohamishika pamoja na umiliki wa pesa kwenye masoko ya mitaji.
✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza njia rahisi ya kugundua kama wewe ni tajiri, mtu wa pato la kati au masikini. Anza sasa kuongeza siku ambazo unaweza kuishi pasipo kufanya kazi. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(