NENO LA LEO (OKTOBA 15, 2020): HIZI NDIZO SEHEMU 3 MUHIMU ZA KUJIONGEZEA MAARIFA KATIKA KARNE HII.
ππΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tens katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Ni matumaini yangu kuwa umeianza siku salama ukiwa na nguvu na hamasa za kuendelea kutoa thamani zaidi kwa jamii inayokuzunguka. Basi kila mmoja wetu na aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
✍πΎ Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza sehemu tatu ambazo unatakiwa kujiongezea maarifa katika karne hii ya 21. Kama ambavyo nimekuwa nikikusisitiza kuwa safari ya maisha yenye thamani inahusisha kujifunza na kuachana na maarifa yaliyopitwa na wakati au ambayo hayana tija (learn and unlearn process). Huu ni mchakato ambao kila mwenye kutaka kuacha alama hapa Duniani anatakiwa kuupitia katika maisha yake ya kila siku. Karibu tujifunze sehemu tatu muhimu ambazo unatakiwa kuongeza maarifa kila siku.
✍πΎ Sehemu ya kwanza: Jifunze sayansi na sanaa ya mauzo. Hii ni sehemu ambayo kila mtu mwenye kusudi la kufanikiwa katika maisha yake anatakiwa kuongeza maarifa kulingana na karne ya sasa. Ukweli katika maisha ili ufanikiwe kifedha unatakiwa kuchagua moja kati ya kuuza au kuuzwa (sell or be sold). Ili uwe na uhuru wa kifedha ni lazima uwe muuzaji mzuri. Maarifa katika tasnia ya mauzo yanabadilika kila mara kutokana na mabadiliko ya teknolojia. Ni kutokana na mabadiliko hayo unalazima kila mara kujifunza mbinu mpya za mauzo.
✍πΎ Sehemu ya pili: Jifunze kuwekeza kwenye masoko ya mitaji (capital markets). Masoko ya mitaji yanahusisha uwekezaji kwenye hisa (stocks), hatifungani za serikali (government bonds) na mifuko ya uwekezaji wa pamoja (mutual investments funds). Kama unahitaji kuwa tajiri wa kweli ni lazima ufikirie ni jinsi gani pesa inaweza kuongezeka hata katika kipindi ambacho utakuwa umelala au haufanyi kazi kwa ujumla. Kwa kifupi tunasema pesa inakufanyia kazi. Sehemu ya kufanikisha hilo ni kwenye uwekezaji kwenye masoko ya mitaji.
✍πΎ Sehemu ya tatu: Jifunze kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Hii ni sehemu nyingine ambayo itakuwezesha kutengeneza utajiri zaidi hata katika kipindi ambacho utakuwa haufanyi kazi. Ardhi inaongezeka thamani na ardhi hiyo hiyo inaweza kufanikisha kila aina uwekezaji unaofikiria. Pia, unatakiwa kufahamu kuwa ardhi haingezeki lakini sisi tunaongezeka idadi hivyo kila kipande cha ardhi unachokiona sasa kesho thamani yake itaongezeka.
✍πΎ Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza sehemu ambazo tunalazimika kuongeza maarifa katika karne ya sasa ikiwa tunahitaji kuishi maisha yenye uhuru wa kifedha. Anza sasa kuongeza maarifa katika sehemu hizo kwa ajili ya mafanikio yako. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Unaweza kujiongezea maarifa kwenye sehemu hizo tatu kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu vinavyohusiana na hizo sehemu kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
ππΎππΎππΎππΎππΎ
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
ππΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(