HAKUNA NAMNA NI LAZIMA UJITOFAUTISHE NA WENGINE

NENO LA LEO (OKTOBA 27, 2020): HAKUNA NAMNA NI LAZIMA UJITOFAUTISHE NA WENGINE.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tena tumejaliwa kuwa hai kwa ajili ya kuendeleza yaliyo bora katika maisha yetu. Kila mmoja atumie siku hii kuendelea kuchochea kuni kwa ajili ya uendelevu wa mafanikio ya ndoto yake. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kujitofautisha na kundi la watu ili upate kuwa tofauti kwenye kila sekta ya maisha yako. Watu wengi waliofanikiwa au wanaoendelea kufanikiwa ni wale ambao wanafanya vitu vya tofauti. Kundi kubwa la watu hawa linahusisha watu wenye sifa nyingi ambazo hazifanani na wanaowazunguka. Kupitia neno la tafakari ya leo nataka uanze kujitofautisha na wengine kwenye sehemu zifuatazo:- 

✍🏾 Sehemu #1: Fanya kazi nyakati ambazo wengine wamelala – Kadri wengine wanavyovuta shuka asubuhi na kuwahi kwenda kulala usiku wewe jitofautishe kwa kufanya kazi za ziada. Usiku chelewa kulala kwa kufanya kazi ambazo zina tija na asubuhi wahi kuamka kwa ajili ya maandalizi ya majukumu ya siku. Baada ya miaka kadhaa watakushangaa uliweza vipi kufikia mafanikio uliyonayo.

✍🏾 Sehemu #2: Jifunze wakati ambao wengine wanachati – Katika ulimwengu wa mafanikio unatakiwa kuwa kama nyoka katika hatua za ukuaji wake. Kadri nyoka anavyokua anaimarisha magamba yake mpaka inafikia hatua ambapo maganda hayo yanamzuia kuendelea kukua zaidi. Ili apate kukua zaidi ni lazima avue gamba na kuanzisha ukuaji upya. Katika ulimwengu wa mafanikio gamba linachukuliwa kama maarifa yanayokuzuia kusonga mbele. Ili ufanikiwe zaidi unatakiwa kuongeza maarifa kila mara.

✍🏾 Sehemu #3: Weka akiba wakati ambao wengine wanakula raha – Ni kupitia utaratibu wa kuweka akiba utaweza kuwa na uwezo kunufaika na fursa zinazojitokeza ghafla. Kadri utakavyofanikiwa kunasa fursa hizo ndivyo utaambiwa kuwa una bahati na kusahau kuwa bahati huwa inaenda kwa waliojiandaa. Pesa inaenda inakopendwa zaidi, hivyo jitofautishe na wengine kwa kuipenda pesa yako kupitia utaratibu wa kuweka akiba.

✍🏾 Sehamu #4: Ishi kana kwamba waone unavyoishi ni ndoto. Watu wengi waliofanikiwa huwa wanafanya vitu ambavyo awali vinaonekana kuwa ndoto kwenye macho ya watu wa kawaida. Ndiyo kwa wengine wataendelea kuona unafanya vitu visivyowezekana hila kwako wewe endelea kubadilisha ndoto na kuzoweka kwenye uhalisia wake.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kujitofautisha na kundi la watu wengine. Ikiwa unatamani kufika mbali hakuna namna zaidi ya kupiga hatua za ziada ikilinganishwa na kundi watu wanaokuzunguka. Anza sasa kuwa wa tofauti. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(