Habari
ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tumepata
kibali cha kuamka salama. Matumaini yangu ni kwamba tayari unaendelea na
majukumu yako ya siku ya leo katika kuhakikisha siku yako inakubwa bora. Tunaendelea
na masomo yanayolenga kutufungua akili katika safari ya kujijua sisi ni nani na
tumeumbwa kwa ajili ya kukamilisha nini hapa duniani. Hilo ndilo jukumu kubwa
ambalo kila siku tunao wajibu wa kuangaika nalo kwa maana tumeumbwa kuendeleza
mema ya nchi kupitia akili na kazi ya mikono yetu.
Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA.
Katika
mafundisho yaliyopita tuliona kuwa “Karma” ni neno la kiimani
linalotumika kwenye mafundisho ya dini ya Hindu na Budha hasa katika katika
bara la Asia. Neno hili linatumika kumaanisha kuwa toka siku mwanadamu
anapoumbwa akaunti ya matendo yake inafunguliwa na chochote anachofanya
kinaingia kwenye akaunti hiyo na uwezekano wa matendo hayo kumrudia katika
maisha ya sasa (maisha ya hapa duniani) au maisha ya baadae (maisha baada ya
kifo). Kwa ujumla, “Karma” ni sawa na matendo yako katika kila siku ya
maisha yako. Karibu tujifunze sheria 12 za mafundisho ya Karma na umuhimu wake
katika kuliishi kusudi la maisha yetu:-
Sheria
#1: Sheria Mama ya Asili ya Kisababisho na Athari (Cause and Effect).
Hii ni sheria ya asili yenye nguvu katika kuamua mafanikio ya kila aina katika maisha yetu ya kila siku. Kubwa ni kwamba tunachojifunza kupitia sheria hii ni kila matokeo tunayopata ni zao la matendo yetu kwenye maisha ya kila siku. Tunavuna kulingana na kile tunachopanda. Ikiwa unahitaji kupata furaha, amani, upendo, na urafiki, ni lazima mtu AWE mwenye furaha, amani, upendo, na rafiki wa kweli. Hivyo, chochote ambacho mtu atapanda kwenye Ulimwengu kama mbegu ni lazima kimrudie kama matunda kulingana na mbegu alizopanda.
Sheria #2: Uumbaji. Chochote tunachohitaji kufanikisha katika maisha ni lazima tuwe tayari kushiriki kwa maana hakuna muujiza utakaofanikisha matokeo pasipo uhusika wetu. Sisi ni wamoja na Ulimwengu ndani na nje, chochote kinachotuzunguka katika Ulimwengu huu ni kwa ajili ya kutuimarisha ndani. Hakikisha unazungukwa na yale ambayo unahitaji yatokee katika maisha yako ili kufanikisha uumbaji wake.
Sheria #3: Unyenyekevu. Chochote unachohitaji kubadilisha katika maisha yako ni lazima kwanza ukubaliane nacho. Ikiwa ni tabia ambayo unahitaji kuibadilisha ni lazima kwanza ukubali madhaifu ya kuwa na tabia hiyo. Ikiwa ni mtu unamuona kuwa adui kwa mafanikio unayohitaji ni lazima uwe tayari kukubaliana kuachana naye kwa ajili ya kufikia kiwango cha juu cha mafanikio. Zaidi ya yote ili ufanikiwe ni lazima uwe tayari kujinyenyekea na kujiona mdogo kuliko wengine.
Sheria #4: Ukuaji. Popote uendapo, hapo ulipo; mara zote ikiwa unahitaji kukua kiroho ni sisi ambao tunapaswa kubadilika na wala sio watu, mahali au vitu vilivyopo sehemu husika. Kitu pekee ambacho tumepewa katika kubadilika ni mamlaka juu ya nafsi zetu. Tunapobadilisha nafsi yetu kulingana na mazingira na imani zilizopo ndani ya mioyo yetu, maisha yetu yanafuatia kubadilika pia ili kuendena na mazingira mapya. Hivyo, husipambane kubadilisha watu au mazingira na badala yake pambana kufanya yanayokuhusu na mwishowe utaeleweka.
Sheria #5: Wajibu. Ikiwa kuna kitu kibaya katika maisha yako, tambua kuwa hayo ni matokeo ya nje ambayo ni mwitikio wa kutoka ndani mwako. Hivyo, jambo lolote baya linaloonekana kwenye limeanzia ndani mwako (mfumo wako wa fikra). Tunaakisi yale yanayotuzunguka na yanayotuzunguka yanaakisi kutoka kwetu – huo ndiyo ukweli kuhusu Ulimwengu. Anza kubadilika mwenyewe kwa ajili ya kubadilisha Ulimwengu unaokuzunguka. Hivyo, lazima mtu atambue wajibu wake katika kufikia kile ambacho nahitaji katika maisha yake.
Sheria #6: Uunganisho (connection). Vitu vidogo au vinavyoonekana kuwa vya maana sana lazima vifanyike kwa sababu kila kitu katika Ulimwengu kimeunganishwa. Kila ni muhimu kwa ajili ya hatua inayofuata, na kadhalika na kadhalika. Mtu lazima afanye kazi ya awali ili kukamilisha kazi iliyopo mbele yake. Hivyo, kila hatua ni muhimu katika ukamilisho wa matokeo unayotaka kulingana na kazi husika. Pia, ni lazima kutambua kuwa kuna muunganiko kati ya yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Kila unalofanya sasa lina mchango chanya au hasi katika maisha yako ya baadae.
Sheria #7: Kujikita kwenye jambo moja. Mtu hawezi kufikiria vitu viwili kwa wakati mmoja. Ikiwa mtazamo wetu uko kwenye Maadili ya Kiroho, haiwezekani kwetu kwa wakati huo huo kuwa na mawazo ya chini kama uchoyo au hasira. Hauwezi kuwa wa moto na wakati huo huo ukawa wa uvuguvugu. Kumbe, kupitia sheria hii tunatakiwa kutuliza akili yetu kwenye jambo moja linalofanyika kwa wakati husika. Epuka kuwa na fikra zilizogawanyika.
Sheria #8: Utoaji na Ukarimu. Ikiwa mtu anaamini kitu kuwa ni kweli, basi wakati mwingine katika maisha yake atahitajika kudhihirisha ukweli huo. Hapa ndipo mazoea yanachukua mkondo wake kwa maana yapo ambayo SIYO kweli lakini kulingana na mazoea tumeaminishwa kuwa ni KWELI.
Sheria #9: Hapa na Sasa (Here & Now). Mtu hawezi kuwa “hapa” na “sasa” ikiwa anaangalia nyuma yaliyopita au ana wasiwasi juu ya siku zijazo. Mawazo ya zamani, mitindo ya zamani, tabia za zamani, na ndoto za zamani na hofu kwa maisha yajayo hutuzuia kuwa wapya kulingana na maisha ya wakati uliopo. Tunaishi katika yaliyopita wakati hatuna nafasi ya kuyabadilisha ya kurekebisha.
Sheria #10: Badilisha. Historia inajirudia ikiwa hatujajifunza masomo ambayo yanatakiwa kubadilishwa katika njia ya sasa. Kuna mengi ambayo tunatakiwa kujifunza kutokana na matukio ya historia ili kuepusha matukio hayo katika maisha ya sasa na wakati ujao.
Sheria #11: Uvumilivu na Thawabu. Zawadi zote zinahitaji taabu ya awali. Tuzo za thamani ya kudumu zinahitaji uvumilivy na bidii ya muda wote. Furaha ya kweli hutokana na kufanya kile ambacho mtu anapaswa kufanya kwa kutambua kuwa tuzo itakuja kwa wakati wake.
Sheria #12: Umuhimu & Ushawishi. Mtu anapata kutoka kwenye kitu
chochote kulingana
na thamani anayoweka katika kitu hiko. Thamani ya
kweli ya kitu ni matokeo ya moja kwa moja ya nguvu na dhamira ambayo mhusika amweka katika kitu hiko. Kila mchango binafsi ni mchango wa wote na mchango wenye upendo
huleta fura
ya maisha na kuhamasisha wengine.
Mwisho, kupitia neno la
tafakari ya leo nimekushirikisha sheria 12 za mafundisho ya Karma. Si sheria
mpya katika maisha yetu ya kila siku kwa maana ni vitu ambavyo tunavielewa. Wajibu
wetu ni kuanza kuishi sheria hizi kwa kuhusisha muunganiko wa mwili na roho na
matendo yenye mwendelezo katika maisha ya kila siku. Kumbuka,
mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu
hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi
katika Maisha yako.
PS: Ongeza maarifa yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu
Augustine Mathias
Mawasiliano:
0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua
pepe: fikrazakitajiri@gmail.com