MASWALI KUHUSU KIFO KULINGANA NA MAFUNDISHO YA “KARMA”: SEHEMU YA KWANZA

NENO LA LEO (MACHI 25, 2021): MASWALI KUHUSU KIFO KULINGANA NA MAFUNDISHO YA “KARMA”: SEHEMU YA KWANZA

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambapo tumepewa kibali kwa ajili ya kuendelea kuboresha maisha yetu. Leo ni siku ya nane kama taifa tukiwa kwenye maombolezo ya rafiki na mpendwa wetu, Rais na Jemederi Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli. Ikiwa ni sehemu ya maombelezo leo nitakushirikisha baadhi ya maswali ambayo kila mmoja wetu huwa anajiuliza kuhusu kifo. Kifo ni kitendawili ambacho kila mwenye uhai hakuna anayeweza kukitegua maana kila mmoja anaogopa kufa. Karibu tujifunze kwa pamoja kwa ajili ya kuboresha maisha yetu.

Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA. 

Karma ni neno la kiimani linalotumika kwenye mafundisho ya dini ya Hindu na Budha hasa katika katika bara la Asia. Neno hili linatumika kumaanisha kuwa toka siku mwanadamu anapoumbwa akaunti ya matendo yake inafunguliwa na chochote anachofanya kinaingia kwenye akaunti hiyo na na uwezekano matendo hayo kumrudia katika maisha sasa (maisha ya hapa duniani) au maisha ya baadae (maisha baada ya kifo).

Swali #1: Kifo ni nini? Tunaweza kufananisha kifo na kushona nguo au chochote unachoweza kuunda, unapounda kitu katika lugha ya ukuaji wa mwanadamu tunaweza kusema kitu hiko kinakuwa kimezaliwa na siku zake za matumizi zinahesabika toka siku kilipoanza kutumika. Hivyo, kifo hakikwepeki kwa kiumbe chochote ambacho kimezaliwa au chenye uhai. Ikiwa kuna kuzaliwa ni lazima pawepo kufa. Na ikiwa kuna kufa kuna kuzaliwa pia. Hata hivyo, katika kitendo hicho cha kuzaliwa na kufa, kinachokufa ni mwili hila roho kwa kuwa ni ya milele yenyewe haifi.

Swali #2: Kwa nini kifo? Tunaweza kusema mwanadamu ana betri tatu toka anapozaliwa: akili, kuongea na mwili. Betri hizi zinaanza kutumika na kuonesha athari zake toka mwanadamu anapoumbwa katika tumbo la mama na zitaendelea kufanya hivyo katika kipindi chote cha uhai wake. Mwisho wa matumizi ya betri hizo ni kifo. Pale ambapo athari za betri hizo inafikia ukomo ndipo tunasema mwanadamu husika amekufa. Hata hivyo, kadri betri hizi zinavyopungua uwezo wake (discharge) kadri umri wa mwanadamu unavyoongezeka, ndivyo, betri kwa ajili ya maisha ya baadae zinavyoendelea kuchaji (charging).

Swali #3: Kwa nini tunaogopa kifo? Kuna hofu ya muda wote kuhusu kifo katika ulimwengu huu kwa kuwa mara zote Ulimwengu kamwe huwa hauwezi kukosa hofu. Na ikiwa mtu anaishi katika hali ambayo hana hisia ya juu ya hofu ya kitu chochote basi mhusika anaishi kwa kutokujua asili halisi ya ulimwengu. Hali inawatokea watu wengi kwa kuwa ni kawaida watu kusinzia wakati macho yao yapo wazi, yaani mtu anaishi lakini hajui misingi halisi ya vitu vinavyomzunguka. Hivyo, ya kifo ni ya asili kwa kiumbe kilichopo katika ulimwengu huu. Hata hivyo, kulingana na “karma” wanaogopa kifo ni wale ambao hawajaitambua nafsi yao (self-actualization). Tumeona kuwa kamwe roho haifi, tunaogopa kufa kwa kuwa tunajifikiria katika mtazamo wa kimwili badala ya kujifikiria katika mtazamo wa kiroho. Unapohusianisha kifo na mtazamo wa roho, utagundua kuwa unakufa kimwili lakini roho yako inaendelea na maisha ya umilele.

Swali #4: Je watu wanahisi nini katika nyakati za kukata roho? Tumeona kuwa kulingana na mafundisho ya ”karma” toka mwanadamu anapoumbwa akaunti ya matendo yake inafunguliwa na chochote kinachoingizwa kwenye akaunti hiyo kitaendelea mbele. Katika saa ya mwisho kuelekea kwenye kifo, maisha yajayo baada ya kifo yatategemea na hali yake ya mabadiliko ya kiroho katika uchambuzi wa mizania ya maisha yake aliyoishi. Uchambuzi wa matendo yake unajikita hasa kwenye kuanzia kipindi cha kati na kuelekea kipindi cha mwisho cha maisha yake. Kwa mfano, ikiwa itatawaliwa na kuhoji maisha ya watu wa karibu yake ambao anawaacha, mada kubwa katika saa ya mwisho ya maisha yake, atafunga maisha kwa kuwaza watu hao na maisha yake yajayo yatajikita kwenye wanyama. Ndiyo maana inashauriwa ukiwa karibu na mtu anayekaribia kufa unatakiwa kumtamkia au kumwandikia maneno matakatifu kama sehemu ya kusaidia uongofu wa roho. Ushauri huu utamsaidia yule anayekata roho ikiwa anajua mafundisho haya la sivyo atajikuta akili yake inatawaliwa na vitu ambavyo anaviacha nyuma.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI 

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumeendelea na mafundisho yanayotujenga kuhusiana na maisha yetu katika kukubaliana na kifo sambamba na kujiandaa katika kuelekea kwenye ukomo wa maisha yetu. Ieleweke kuwa mafundisho haya siyo kwa ajili ya kukutia wasiwasi bali ni kwa ajili ya kukupa ufunuo wa maarifa kuhusiana na kifo, maombolezo na maisha mapya baada ya maisha haya. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Ongeza maarifa yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

 👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(