NENA NA NAFSI YAKO KUHUSU UTAJIRI WA NDOTO YAKO: KAULI 20 ZITAKAZOBADILISHA MTAZAMO WAKO.


   NENO LA LEO (APRILI 20, 2021): NENA NA NAFSI YAKO KUHUSU UTAJIRI WA NDOTO YAKO: KAULI 20 ZITAKAZOBADILISHA MTAZAMO WAKO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi nyingine ambayo nafasi ya kukushirikisha neno la tafakari ya leo. Matumaini yangu ni kwamba umepata pumzi ya uzima na upo tayari kuendelea na majukumu yako siku ya leo. Katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kauli 20 ambazo kila siku unatakiwa kuzinena dhidi ya nafsi yako kuhusu nguvu uliyonayo katika kuvuta utajiri unaohitaji. Tunafahamu kuwa maneno unayonena dhidi ya nafsi yako yana nafasi kubwa ya kuharibu au kujenga uwezo wako wa kujiamini katika kile unachoamini. Karibu tujifunze kwa pamoja:-

Je unahitaji kupata mafundisho ya aina hii kila siku? Jiunge kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, tafadhali BOFYA HAPA KUJIUNGA.

1. Mimi ni tajiri, mimi ni mwanaume/mwanamke tajiri, mimi ni sumaku nitavuta utajiri kwangu kutoka pande zote.

2. Mimi ni sehemu ya ulimwengu usio na mwisho na usio pungukiwa hivyo nimeunganishwa na kila kitu ninachohitaji katika kufikia utajiri wa ndoto yangu.

3. Nitawapa wengine thamani kubwa, kila mara nitakuwa mtu wa thamani kwa wengine, mimi ni mtu asiye na ukomo wa maoni na fikira za ubunifu. Natambua kuwa nitabarikiwa utajiri zaidi kadri ninavyotoa thamani kwa wengine.

4. Kuna zaidi ya kutosha kwa kila mtu. Wingi uko kila mahali ninapoangalia. Ninaona utajiri, wingi na ustawi kila mahali niendako.

5.   Nastahili kuwa tajiri. Utajiri ni haki yangu ya kuzaliwa. Utajiri ni sehemu ya maisha yangu. Ulimwengu upo tayari kunizawadia utajiri wa ndoto yangu.

SOMA: MAISHA YA UTAJIRI AU UMASIKINI: JE NI IPI HAKI YAKO YA KUZALIWA?

6.  Nimeumbwa kwa ajili ya kuishi maisha ya shibe, maisha ya kuwa na zaidi, maisha ya kujitosheleza. Hivyo, shibe ni haki yangu ya kuzaliwa. Sijaumbiwa maisha ya dhiki kwa kuwa Muumba anachukia dhiki kwa waja wake.

7. Ninawaombea watu wote maisha ya utajiri wa ndoto zao, maisha ya shibe. Ninanayo furaha kubwa kadri ninavyoona natumika kuwasaidia watu wengine kufikia utajiri wa ndoto zao. Upendo ni nyenzo kuu ambayo nitaendelea kuitumia kusaidia watu.

8. Mimi nimeumbwa na Mungu ambaye aliniweka katika Ulimwengu huu na kuinua nafsi yangu juu. Nimepewa mamlaka ya kutawala vitu vyote na kupitia kuumbwa kwa sura na mfano wake nimepewa mamlaka ya kuumba kila kitu ambacho nakiona katika fikra zangu.

9.   Kila siku, kwa kila njia, ninazidi kuwa tajiri. Najipima nakuona kuwa matendo yangu yananiwezesha kukua kiuchumi kila siku. Nitaendelea kuwa sehemu ya kukuza utajiri wangu kupitia matendo yangu.

10.  Hakuna ubaya wowote kuhusu pesa ikiwa pesa inapatikana na kutumika kwa njia halali. Mimi ndo nitaifanya pesa ionekane mbaya au nzuri kupitia matumizi ya pesa inayoingia mikononi mwangu.

11.  Matendo yangu yana thamani kwa wengine kiasi gani? Nitaendelea kutumia pesa kupima thamani ninayoitoa kwa wengine. Watu wapo tayari kulipia thamani ninayoitoa kwao kulingana na mahitaji ya soko.

12.  Pesa ni nishati safi ya kuniwezesha kumiliki na kuitawala dunia. Pesa inaundwa katika mfumo wangu wa fikra. Pesa iko akilini mwangu. Nitaendelea kutumia akili yangu kuvuta pesa ninazohitaji siku baada ya siku.

13. Ninastahili kumiliki pesa. Ninastahili kuwa na pesa nyingi. Hivyo, nipo tayari kuvutia kiasi kikubwa cha pesa kwangu kupitia thamani ninayoitoa kwa wengine.

14. Kuwa tajiri kunanipa nguvu ya kusaidia watu wengine wenye mahitaji katika Ulimwengu huu kwa ajili ya kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yao. Nitatumia sehemu ya kiasi cha pesa ninachopata kwa ajili ya kukusaidia na kuinua watu wengine.

15.  Mimi ni msimamizi mkuu wa pesa yangu. Sitakubali pesa itumike kuharibu maisha yangu. Nitasimamia maisha yangu ya kifedha kwa ajili ya utakaso wa nafsi yangu katika maisha haya na maisha yajayo.

16.  Pesa inaenda sehemu ambako inapendwa na kuthaminiwa zaidi. Nitahakikisha kila shilingi inayoingia mkononi mwangu inatumika kulingana na bajeti. Nitahakikisha natumia pesa ninayoipata kukuza uwezo wangu wa kifedha kwa kuhakikisha pesa inatumika kuzalisha pesa zaidi.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI

17.  Natambua kuwa kiwango cha pesa ninachopata kina uhusiano mkubwa na kiwango cha pesa ninachotoa kwa wengine. Kadiri ninavyotoa zaidi, ndivyo ninavyozidi kuwa tajiri. Kadiri ninavyotoa zaidi ndivyo nazidi kuunganishwa na watu ambao watanifungulia milango ya kukua zaidi kiuchumi.

18.  Watu wanaonizunguka wanabariki utajiri wangu kwa maana nimekuwa wa msaada kwao katika kila hali. Nimekuwa mtu wa kufunua fursa kwa wengine. Nimekuwa mtu wa kuendelea kuhamasisha wengine. Nimekuwa mtu wa kuonesha wengine kuwa kila jambo linawezekana.

19. Ninapumua kwa raha. Naendelea kuwa sehemu ya jamii inayolinda ubora wa hewa tunayovuta. Kila pumzi ninayovuta huongeza ufahamu wangu kuhusu wingi unaonizunguka.

20.  Nina fikra za kimilionea. Nina mawazo kimilionea. Natenda kama milionea, nahisi kama milionea, mimi ni milionea. Ninashinda vizuizi vyote ambavyo viko katika njia yangu ya mafanikio na uhuru wa kifedha.

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha kauli 20 kutoka kwenye vyanzo tofauti ambavyo vimeandika kuhusu utajiri. Hizi ni kauli chache ambazo unaweza kuzinena dhidi ya nafsi yako katika maisha yako ya kila siku. Unaweza kurekebisha au kuboresha kauli hizo ili ziendane na mazingira ya maisha yako. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganishi hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema OFA hii.

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(