Habari
ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya
ambapo tunaanza robo ya pili yam waka 2021. Matumiani yangu ni kwamba
unaendelea kwenye sahihi kulingana na malengo uliyoanisha katika kipindi cha mwanzo
wa mwaka. Leo ni siku 15 kati ya siku 21 za maombolezo ya kifo cha mpendwa
wetu, shujaa wa Afrika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Baada ya
mfululizo wa mafundisho kuhusu majuto kwa watu wanaokaribia kukata roho, katika
neno la tafakari ya leo nitakushirikisha mbinu ambazo unaweza kuzitumia ili kuepuka
majuto kwenye maisha yako ya kila siku.
Ukweli ni kwamba uzoefu unaonesha
kuwa maisha ya mwanadamu katika sayari hii ya dunia ni mafupi. Hakuna yeyote
kati yetu ambaye anajua ni muda kiasi gani amebakiza kwa ajili ya uhai wa hapa
duniani. Hata hivyo, watu wanaoishi maisha huru na kwa ukamilifu, maisha yasiyo
na majuto ni wachache sana katika dunia ya sasa. Kawaida majuto yanatokana na
maneno au sentensi ambazo hazijasemwa; ndoto ambazo hazijaguswa au kutekelezwa
ipasavyo; ugomvi wa kila mara ndani ya familia, ndugu, kazini, majirani au
marafiki; muda au rasilimali zilizopotea hovyo. Hata hivyo, unaweza kutumia
mbinu zifuatazo kuepuka majuto katika maisha yako ya kila siku. Karibu
tujifunze:-
MARA ZOTE ISIKILIZE ROHO YAKO. Kwa wale waumini wa dini ya Kikristo tunaamini kuwa baada ya Kristo hatukuachwa peke yetu bali kila mmoja wetu ana roho mtakatifu ambaye anamuongoza katika kutenda mema (Yohana 14: 15 – 25). Katika maisha ya kila siku watu wengi wanatenda matendo ambayo wanajutia baadae kwa kuwa wanashindwa kuisikiliza sauti ya ndani inawaambia nini kabla ya kufanya matendo husika. Husipende kufuata ushauri wa watu kabla haujatumia akili yako kuchambua ushauri husika maana ni wewe pekee unayejua hitaji la maisha yako. Hata ikiwa moyo wako unataka kitu ambacho kinaonekana kuwa hakiwezekani, jaribu kuusikilizia kwanza maana wako hauwezi kukudanganya kamwe au kukuongoza kwenye njia mbaya. Mfumo wako wa fikra na akili ni nyenzo muhimu zenye nguvu ya kukuepusha majuto ikiwa utatumia nyenzo hizo katika maamuzi yako ya kila siku. Ikiwa utatumia nyenzo hizi hata kama husipofanikiwa angalau hautajutia kuwa ulipotezwa na ushauri wa watu na utakuwa na nafasi kubwa ya kujipanga na kuanza upya.
EPUKA MAJUTO KATIKA KILA UNACHOFANYA. Maisha yetu ya kila siku kama wanadamu yanaongozwa na sheria katika ngazi mbalimbali za utawala. Kila mara jitahidi kutii sheria zilizopo katika kile unachofanya ili kujiepusha na majuto yanayotokana na uvunjifu wa sheria. Lakini pia wakati mwingine furahia maisha kana kwamba hakuna vizuizi mbele yako, ishi kwa kuisikiliza roho yako inataka nini dhidi ya sheria zinazokuzuia kufanya jambo flani. Kama unaweza safiri kwenda sehemu ambazo unatamani kufika na kufurahi uzuri wa nchi katika sehemu hizo. Tumia muda wako mara nyingi kuwaambia wapendwa wako kuwa unawapenda na pendo lako hakika walione kwa vitendo. Kama kuna kazi unafanya ambayo hauipendi, jipange na kuhakikisha unatafuta kazi nyingine ili kituo chako cha kazi kisiwe sehemu ya majuto bali sehemu ya kufurahi kutokana na jinsi unavyofanikisha ndoto zako kupitia kazi unayofanya.
RUHUSU NAFSI YAKO HALISI ICHANUE KATIKA KILA UNALOFANYA. Watu wengi wanaishi kwenye pingu za maisha au maoni ya watu wengine. Wengi katika kila wanachofanya wanaangalia mapokeo ya jamii inayowazunguka kwa maana wanataka kufurahisha kila anayewazunguka huku wakidharau mahitaji ya nafsi zao. Husiishi maisha ya kuigiza bali ishi kulingana na mahitaji halisi ya nafsi yako na katika kufanya hivyo watu sahihi watajidhihirisha katika njia zako. Kumbuka kila nafsi imeumbwa kwa makusudi ya kufanikisha jambo hapa duniani, ikiwa unaishi maisha ya wengine hakika unaidhurumu nafsi yako. Kila ukijiangalia kwenye kioo ione sura ambayo inaishi kile inacokiamini katika kila sekta ya maisha yako.
PENDA KULINGANA NA UWEZO WAKO NA MARA NYINGI UWEZAVYO. Fikiria Ulimwengu huu ungeonekana vipi ikiwa kila mtu angeonesha upendo wake wa wazi na kwa uhuru awezavyo. Hakika Ulimwengu ungekuwa sehemu ya furaha kwa mwanadamu kuishi, hata hivyo, hali haipo ndani mwetu kwa kuwa wengi watu tunaishi maisha ya unafiki. Wengi wanaishi maisha ya upendo wenye masharti; wengi wanaishi maisha ya upendo wenye woga ndani mwake; na wengi wanaisha upendo husiyo na matendo ya huruma au Faraja ndani mwake. Upendo wa dhati unaanza kwa kujipenda mwenyewe kabla ya kufanya hivyo kwa wengine. Neno upendo linapozungumzwa juu ya kupeana na kupokea matendo ya upendo, tunamaanisha pia kujipenda na kujikubali mwenyewe. Zaidi ya yote usiwe mbinafsi na upendo wako dhidi ya jamii inayokuzunguka kwa ulimwengu haujawahi kupungukiwa.
EPUKA HOFU INAYOTOKANA NA MATUKIO
AMBAYO YAKO NJE YA UWEZO WAKO KUYAZUIA. Usiruhusu
akili yako itawaliwe
na vitu vidogo vidogo ambavyo vinaweza kwenye kinyume katika maisha; ishi
kulingana na wakati uliopo kwa ajili ya wakati ujao. Acha kuitawanja akili yako
katika mambo mengi na badala yake hakikisha akili yako inajikita kwenye kazi
unayofanya. Mara zote hofu katika matukio ambayo yapo nje ya uwezo wako wa
kuyazuia inakufanya uishi maisha ya huzuni na mwisho wake hauwezi kuwa na
furaha siku zote. Una umiliki
wa akili yako, mwili, na roho, hivyo hakikisha unatumia vitu hivyo kwa ajili ya
kujiendeleza na kujijenga zaidi kuliko kujibomoa kutokana na hofu.
Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuepuka majuto kwenye maisha yako ya kila siku. Kubwa ambalo nakusisitiza ni kutambua kuwa wewe ni wa kipekee na unaweza kuishi maisha unayoyataka wewe pasipo kuingiliwa na mtu mwingine, itumie vyema nafsi yako. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Ongeza maarifa yako kupitia usomaji wa
vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha
hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs.
3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu
Augustine Mathias
Mawasiliano:
0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua
pepe: fikrazakitajiri@gmail.com