TABIA 10 AMBAZO HUTOJUTIA KUZIISHI MAISHANI MWAKO

NENO LA LEO (APRILI 2, 2021): [BURIANI JPM] TABIA 10 AMBAZO HUTOJUTIA KUZIISHI MAISHANI MWAKO

Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku ya Ijumaa kwa wale ambao ni wahumini wa dini ya Kikristo ikiwa ni kumbukizi cha ya kuadhimisha kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo. Matumani yangu ni kwamba wote tumeamka salama na tupo tayari kuendelea na majukumu yetu ya siku ya leo. Pia, kama taifa bado tupo kwenye maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu, shujaa wa Afrika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ikiwa ni siku ya 16 kati ya siku 21 za maombolezo.

 Kama bado hujajiunga na kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI kwa ajili ya kupata neno la tafakari kila siku, tafadhali JIUNGE SASA. 

Katika neno la tafakari ya leo nitakushirikisha tabia 10 ambazo hakika hutojutia kuziishi katika kipindi cha maisha yako yote. Katika mafundisho ya majuto kwa watu anaokaribia kukata roho tuliona kuwa majuto mengi katika saa ya kupambania dakika ya mwisho wa uhai yanatokana na vitu ambavyo wengi walishindwa kuviishi katika kipindi cha uhai wao. Ni tabia za kawaida ambazo tunashindwa kuziishi kila siku na pale mwisho wa uhai unapokaribia tunajikuta kwenye majuto ya rohoni. Ikiwa hakuna anayejua saa wala siku ni muhimu kuanzia sasa uanze kuishi tabia zifuatazo kila siku:-

MAJUTO KWA WANAOKARIBIA KUKATA ROHO – SEHEMU YA MWISHO 

ONESHA UPENDO WAKO KWA KILA UMPENDAYE. Ni kawaida watu wengi kukosa muda wa kuwa karibu na wapendwa wao kutokana na majukumu ya kila siku. Mbaya zaidi karne ya sasa kutokana na mapinduzi ya teknolojia ya habari, watu wengi wanajikuta hata ule muda wanaokuwa na wapendwa wao muda mwingi wanajikita kwenye kuperuzi mitandao. Matakeo yake watu hawana muda wa kuonesha upendo kwa wapendwa wao. Kuanzia sasa jenfa tabia ya kuonesha upendo kwa wapendwa wako.

Tumia neno NAKUPENDA/NAWAPENDA kila mara kwa kadri uwezavyo kwa wapendwa wako. Pia, hakikisha unakuwa na ratiba katika siku ya karibu na familia au wapendwa wako ujumla. Katika muda huo hakikisha unapata muda wa kuongea na kufurahi na kila mmoja. Kadri utakavyo imarisha tabia hii ndivyo utashangaa unaanza kupendwa na kila mtu ambaye unaonesha upendo wako kwake. Toa upendo kikamilifu, pokea upendo kikamilifu; husiogope, maana upendo unavuta baraka nyingi katika maisha.

ISHI KWA KUONGOZWA NA MALENGO. Tumeona kuwa watu wengi katika kipindi cha kukata roho wanajutia kutokutimiza ndoto muhimu katika maisha yao. Hali hii inatokana na kutokujali muda kwa maana wengi wanaishi kana kwamba uhai utaendelea kuwepo. Bahati mbaya ni kwamba kifo huwa kinatuvamia katika nyakati ambazo hatukutarajia. Ili kuepuka majuto ya aina hii unashauriwa kuishi kwa malengo kwenye kila sekta ya maisha yako. Ishi ukiuona mwisho wa safari yako katika picha ya akili yako. Weka mikakati ya muda mfupi na muda mrefu na kuhakikisha unaiishi kila siku.

TUMIA TEKNOLOJIA KUONESHA UPENDO WAKO. Ni kawaida katika majukumu yetu ya kila siku kuwa mbali na wapendwa wetu. Hata hivyo, kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano tunaweza kuunganishwa na familia zetu kila mara tunapohitaji. Tunaweza kutumia mawasiliano ya “video call” au mawasiliano ya kawaida kuongea na kila mmoja ambaye tunahitaji kuonesha upendo wetu. Pia, tunaweza kunufaika na ukuaji wa teknolojia ya habari kupitia kupiga picha na wapendwa wetu. Shirikishana picha ambazo zitaamsha hisia za upendo kati yenu. Ikumbukwe kuwa picha ni kumbukizi ambayo itaendelea kuamsha hisia kati yenu hata nyakati zijazo. Hii ni pamoja na kutumia teknolojia kujipenda bila masharti.

JIFUNZE KUONA WEMA/UZURI KATIKA KILA JAMBO. Hii ni tabia ambayo itakuwezesha kuukimbia ubaya katika kila unalofanya maana katika kila tukio badala ya kuona ubaya utajifunza kutafuta upande wa pili wa tukio husika. Kwenye matukio ya ubaya unatakiwa kujiuliza je katika tukio la namna hii ni lipi jema ambalo naweza kujifunza? Angalia karibu yako, angalia ndani mwako, angalia wanaokuzunguka, angalia vitu vinavyokuzunguka – katika kila kinachokuzunguka jifunze kutazama wema au uzuri wake. Hakika kwa tabia hii utavuta mengi mazuri badala ya mabaya.

ONESHA USO WA TABASAMU. Uso wako na uoneshe tabasamu kwa kila mtu iwe mnafahamiana au mgeni. Nimekuwa nikifundisha kuwa mafanikio ya kila aina yanatokana na watu. Ikiwa utajifunza mbinu rahisi za kuvuta watu kwako itakuwa rahisi sana kufanikisha ajenda zako muhimu katika maisha. Kuonesha tabasamu kila mara ni moja ya mbinu ya kuvuta watu wengi kwako. Mtu mgeni mara nyingi atavutiwa kuanzisha maongezi na mtu mwenye tabasamu usoni na mcheshi ikilinganishwa na mtu ambaye muda wote amekaza uso.

WAINUE WATU WENGINE. Brikiwa, furahi na kujivunia kadri unavyowainua watu unaojumuika nao. Toa pongezi hata kwa kazi ndogo ambazo watu wa karibu yako pale wanapofanikisha kazi. Toa pongezi pale inapotakiwa kulingana na ufanisi wa kazi. Wafurahishe watu wanaokuzunguka au ambao mnashirikiana katika majukumu ya kazi.

AJALI AFYA YAKO. Afya ni kila kitu katika kufanikisha kila hitaji la maisha yako. Ilinde afya yako kupitia mawazo, fikra na vitendo. Jiweke mbali na hofu zisizo na maana na ikiwezekana kuwa tayari kuonekana kama mtu hasiyejali ikiwa watu wanaokuzunguka wanataka kukupandikizia hofu ndani ya nafsi yako. Fanya mazoezi ya viungo. Soma maarifa mbalimbali kwa ajili ya kulinda afya ya ubongo wako. Kula na kunywa kwa kuzingatia vyakula/vinjwaji vinavyohitajika katika kujenga na kulinda mwili.

TENGA MUDA KWA AJILI YAKO. Huu ni muda maalum kwa ajili ya nafsi yako. Katika muda hakikisha unapata muunganiko halisi wa roho na mwili. Ikiwa ni sara tumia muda huu kwa ajili ya kuomba. Ikiwa ni tajuhudi, tumia muda huu kwa ajili ya kufanya tajuhudi. Ikiwa ni fikra huru, tumia muda huu kuvuta fikra. Muda wa peke yako ni wa muhimu kwa ajili ya afya ya akili na mwili wako – hakikisha unakuwa na muda wa peke yako kwa ajili ya tafakari na tathimini.

SOMA: FAHAMU NJIA ZA KUEPUKA MAJUTO KATIKA MAISHA YAKO YA KILA SIKU

IPENDE NAFSI YAKO. Epuka tabia ambazo zinaharibu mwili na roho yako. Mwili wako na uwe hekalu la roho mtakatifu. Jipende ili kila mmoja anayekuzunguka atamani kujua siri ya mafanikio yako. Jikosoe na ukubali kukosolewa pale unapokuwa umekosea. Jicheke mwenyewe na kujihurumia pale unapokesea.

JIFUNZE KWA KADRI UWEZAVYO. Hakika ikiwa haujifunzi ni wazi kuwa umekufa japo bado unaishi. Kila siku ukurasa unafunguliwa kwa ajili ya kujifunza maarifa mapya katika maisha yetu. Jifunze kupitia makosa yako, makosa ya wengine na kupitia wanaokuzunguka.

KUJIUNGA NA PROGRAMU MAALUM YA "JILIPE KWANZA": SOMA MAKALA HII KWA KUBONYEZA MAANDISHI HAYA YENYE RANGI   

Mwisho, katika neno la tafakari ya leo nimekushirikisha tabia 10 ambazo ukifanikiwa kuziishi kamwe hautakaa ujutie. Maisha ni furaha na furaha inapatikana kupitia kuishi tabia za kawaida katika maisha ya kila siku. Kumbuka, mbegu ikidondoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS:  Ongeza maarifa yako kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

onclick='window.open(