⏩Hongera kwa jumapili iliyo bora. Ni matumaini yangu kuwa siku imemalizika salama. Waswahili wanasema "kimya kingi kina mshindo wake".
⏩Ni kweli kuwa toka tarehe 20 mwezi Aprili, 2020 hadi sasa nimepitia mawimbi ya maumivu ya mwili kutokana na ajali mbaya ambayo Mungu aliniepushia.
Kujiunga kundi letu la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI, TAFADHALI BOFYA HAPA
⏩Pamoja maumivu hayo ilifikia sehemu nikawa kwenye tafakari nzito ya kujiuliza ikiwa ningekufa katika ajali ile ningeacha alama gani katika mioyo ya watu wanaofuatilia masomo yangu na familia yangu kwa ujumla.
⏩Katika tafakari hiyo nikapata wazo la kuandika kitabu na ndipo nikaona nina deni la kuelimisha kuhusu jinsi gani kila mmoja wetu anaweza kuishi MAISHA YENYE THAMANI yaani maisha yanayoacha alama chanya katika Ulimwengu tunaoishi.
⏩Hata hivyo, pamoja na maamuzi hayo changamoto ilibakia ni kwa jinsi gani nitaweza kuandika kitabu hicho katika kipindi ambacho napitia maumivu makali kiasi ambacho siwezi kukaa muda mrefu. Pia, ni kipindi ambacho Kompyuta yangu mpakato ilikuwa na hitilafu.
⏩Yote hayo yakaonekana kama kikwazo cha kunizuia kukamilisha azma yangu ya kuandika kitabu ambacho ni msingi wa kuelimisha jamii hasa wafuatiliaji wa masomo yangu ili wapate kuishi maisha yenye kuacha alama baada ya ukomo wa maisha ya haya.
⏩Ili kuondokana na changamoto hiyo ilinibidi nitafute kwenye mitandao jinsi gani naweza kuandika kitabu kupitia simu yangu ya mkononi.
⏩Majibu niliyopata yamewezesha leo hii niwe mwenye furaha kwa kufanikisha kuandika kitabu changu cha kwanza. Huwezi amini lakini huo ndiyo ukweli, nimefanikiwa kuandika kitabu chenye zaidi ya kurasa 150 kupitia simu yangu ya mkononi.
⏩MAISHA YENYE THAMANI ni kitabu kinachotoa ufafanuzi wa kina kuhusu nyakati za maisha, mahitaji na hatua za ukuaji wa mwanadamu tangu kuzaliwa hadi kufa.
⏩Katika kitabu hiki nimeelezea namna mwanadamu anavyoweza kujitambua na kuishi maisha yenye manufaa, furaha na amani.
⏩Nimeelezea kwa kina namna ambavyo nadharia mbalimbali za maendeleo na ukuaji wa mwanadamu zinavyoathiri utu wa mwanadamu ambao ni msingi mkuu wa maadili katika jamii.
⏩Pia, katika kitabu hiki nimeainisha misingi ya imani na mapokeo ya dini mbalimbali jinsi inavyojibu swali kuu la msingi wa kitabu hiki, yaani majibu kuhusu “chanzo na maana ya maisha hapa duniani.”
⏩Aidha, nimechambua changamoto zinazokabili dunia ya sasa na kuonyesha jinsi gani kila mmoja wetu anaweza kushiriki katika utatuzi wa changamoto hizo.
⏩Kama hiyo haitoshi, nimeelezea baadhi ya Sheria za Asili (Universal Laws) ambazo ni msingi wa ufanisi katika maisha.
⏩Hakika maudhui ya kitabu hiki, mtu akifanikiwa kuyafahamu na kujua namna ya kuyaishi, inamuiya rahisi kuishi maisha yenye thamani kubwa sana kwa kizazi chake na kuacha alama kwa vizazi vijavyo.
⏩Hakika hiki ni kitabu muhimu sana kwa wazazi na walezi wa familia, Vijana, viongozi wa taasisi na ngazi zote katika kujiongezea uwezo na ufahamu wa maisha.
Kitabu hiki kwa sasa kinapatikana kwa mfumo wa Nakala tete (soft copy) kwa bei ya zawadi ya Tshs. 10,000/= badala ya Tshs. 20,000/=
Kupata kitabu hiki, lipia kupitia Mpesa kwenye namba +255 (0) 763 745 451 au Airtel Money namba +255 (0) 786 881 155 au Halopesa namba +255 (0) 629 078 410 zote majina ni AUGUSTINE MATHIAS MUGENYI.