UKANDA WA FARAJA: KANDA TATU AMBAZO UNATAKIWA KUPITIA BAADA YA KUUKIMBIA UKANDA WA FARAJA.

NENO LA LEO (OKTOBA 31, 2020): UKANDA WA FARAJA: KANDA TATU AMBAZO UNATAKIWA KUPITIA BAADA YA KUUKIMBIA UKANDA WA FARAJA.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambapo tunaendelea kuwa kwenye changamoto ya kufungwa kwa mitandao ya kijamii. Naamini kila mmoja wetu ameamka salama na yupo tayari kuendelea na majukumu yake ya siku ya leo. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache. 

Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza kuhusu ukanda wa faraja (comfort zone) na kanda tatu ambazo unatakiwa kuzipitia baada ya kuukimbia ukanda wa faraja. Kwa asili tumeumbwa katika hali ambayo miili yetu haitaki kuumia hivyo inaridhika inapokuwa kwenye mazingira salama au tulivu (comfort). Mwili wa binadamu unaogopa mabadiliko kiasi kwamba inapotokea mabadiliko ya namna yoyote ile mwili unakuwa katika hali ya mshutuko. Ni kutokana na sababu hiyo, watu wengi wanaridhika kuwa kwenye mazingira ambayo yamezoeleka (comfort zone) kuliko kujaribu mazingira mapya.

Athari ya kuridhika na mazingira yaliyozoeleka ni kukosa ubunifu ni uthubutu wa mawazo mapya katika ukuaji wa mhusika kwenye kipindi cha uhai wake. Watu wanaofanikiwa kimaisha ni lazima wawe tayari kuukimbia ukanda wa faraja kwa ukanda huo unawafanya wengi kubweteka na hali inayowazunguka. Katika mzunguko wa ukuaji mhusika ni lazima apitie kwenye ukanda wa faraja (comfort zone), ukanda wa hofu (fear zone), ukanda wa kujifunza (learning zone) na ukanda wa ukuaji (growth zone). Karibu tuangalie sifa za kila ukanda.

Pia Soma: JE NI MARA NGAPI UNAJILAZIMISHA KUTOKA KWENYE UKANDA WA FARAJA?

Ukanda wa hofu – Huu ni ukanda unaofuatia baada ya ukanda wa faraja. Katika ukanda wa faraja mhusika anaridhika na kila hali inayomzunguka hila katika ukanda huu mhusika anakuwa hajiamini kwenye kila hatua anayokusudia kuchukua katika maisha yake. Katika ukanda huu mhusika anajiona mnyonge dhidi ya mawazo ya wengine (mawazo ya wengine ni bora kuliko yake); kila mara anatafuta visingizio vya kujifariji kulingana na hali yake; na hofu inamzuia kuchukua hatua zinazolenga kutekeleza kwa vitendo mawazo aliyonayo katika kuboresha maisha yake.

Ukanda wa kujifunza – Huu ni ukanda muhimu kwa mwanadamu yeyote anayelenga kuishi maisha ya thamani. Katika ukanda huu hakuna changamoto ambayo inamzuia mhusika kusonga mbele kwa kuwa katika kila changamoto mhusika anatafuta suluhisho. Pia, katika ukanda huu mhusika anajifunza mbinu na maarifa mapya yanayomuwezesha kuongeza uzoefu dhidi ya mazingira yanayomzunguka. Hata hivyo, kwenye ukanda huu mhusika anaweza kujikuta ameingia kwenye ukanda mpya wa faraja hali ambayo itapelekea hasiweze kukua zaidi katika yale anayofanya.

Ukanda wa ukuaji – Huu ni ukanda ambao mhusika anaishi kusudi la maisha yake kwa ukamilifu. Kwa kuliishi kusudi la maisha yake mhusika anaishi ndoto alizonazo kuhusu maisha kwa kuhakikisha kila mara anaweka malengo mapya mara baada ya kutekeleza malengo ya awali. Ilifanikiwe katika ukanda huu ni lazima ujifunze kuishi kwa hali ya uchanya (positive oriented) kwenye kila hali iliyopo mbele yako. Makwazo, madhaifu na changamoto siyo sababu ya kukuzuia kusonga mbele.

Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kanda nne za ukuaji katika kuelekea kwenye mafanikio unayotamani. Watu wengi huwa wanajikuta wameishia kwenye ukanda wa faraja hali inayopelekea wasiweze kukua zaidi au kufanikisha ndoto walizonazo. Ikiwa unahitaji mafanikio ni lazima kila mara ukimbie ukanda wa faraja katika kila hatua unayopiga. Jiulize je hatua uliyonayo sasa siyo sehemu ya ukanda wa faraja? Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

 

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

KUMBE NDOA ULIYOIZOEA INAWEZA VUNJIKA NA MAISHA YAKAENDELEA.

NENO LA LEO (OKTOBA 30, 2020): KUMBE NDOA ULIYOIZOEA INAWEZA VUNJIKA NA MAISHA YAKAENDELEA.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni nyingine ambayo tumeamka salama na tukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kuendeleza pale ulipoishia jana. Ikiwa ni siku ya pili tangu tumetimiza haki yetu ya msingi ya kuchagua viongozi wa kutuvusha salama katika kipindi cha miaka mitano ijayo tunaendelea kusikilizia maumivu ya kuzimwa kwa mawasiliano ya mitandao ya kijamii. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza juu ya somo muhimu ambalo limetokana na hatua iliyochukuliwa na Serikali ya kuzima mitandao ya kijamii. Leo hii ni siku ya tatu tangu mitandao hii izimwe na maisha mengine yameendelea. Ukweli ni kwamba kizazi cha sasa ambacho kinamiliki simu janja kimeweka ushirika au kifunga ndoa na simu hizo. Kizazi hiki kinatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko inavyokuwa kwenye majukumu mengine ya siku. 

✍🏾 Kuzimwa kwa mitandao hii ya kijamii ni ufunuo kwa wale waliofunga ndoa na simu janja kuwa wanaweza kuishi bila kufuatilia yanayojiri kwenye mitandao ya kijamii. Natambua kuwa zoezi la kuzima mitandao ya kijamii kuna ambao litakuwa limewaathiri kwa asilimia kubwa hasa kwa wale wanaotumia mitandao hii kama jukwaa la kutangaza biashara zao.

✍🏾 Ukweli unabakia kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapoteza muda mwingi kufuatilia mambo yasiyo na tija. Katika kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii imezimwa unaweza kuamua kuanza maisha mapya ya kutokuendeshwa kwa rimoti na simu janja yako. 

✍🏾 Yanayojiri kwenye mitandao ya Facebook, WhatsApp au Instagram hayana tija sana ikilinganishwa na majukumu yako ya msingi ambayo umekuwa ukipiga dana dana (trade off) dhidi ya mitandao ya kijamii. Kipindi hiki ni muhimu kwako kupima ufanisi wa kutekeleza majukumu yako ya msingi ikilinganishwa na kipindi ambacho mitandao ya kijamii ilikuwa inaingilia utendaji kazi wako.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza maisha yanaweza kuendelea hata bila ya uwepo wa mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii imekuwa ni chanzo cha kupoteza muda na matokeo yake ni ufanisi mdogo katika kazi. Pia, mitandao hii imekuwa chanzo cha kuvunja mahusiano ya watu wengi, hivyo kuzimwa kwake kwa siku hizi ni fursa ya kutuonesha kuwa tunaweza kuiendesha mitandao hii badala ya mitandao hiyo kutuendesha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HAKUNA NAMNA NI LAZIMA UJITOFAUTISHE NA WENGINE

NENO LA LEO (OKTOBA 27, 2020): HAKUNA NAMNA NI LAZIMA UJITOFAUTISHE NA WENGINE.

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni wakati mwingine tena tumejaliwa kuwa hai kwa ajili ya kuendeleza yaliyo bora katika maisha yetu. Kila mmoja atumie siku hii kuendelea kuchochea kuni kwa ajili ya uendelevu wa mafanikio ya ndoto yake. Basi tuianze siku kwa kusema “hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani”.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kujitofautisha na kundi la watu ili upate kuwa tofauti kwenye kila sekta ya maisha yako. Watu wengi waliofanikiwa au wanaoendelea kufanikiwa ni wale ambao wanafanya vitu vya tofauti. Kundi kubwa la watu hawa linahusisha watu wenye sifa nyingi ambazo hazifanani na wanaowazunguka. Kupitia neno la tafakari ya leo nataka uanze kujitofautisha na wengine kwenye sehemu zifuatazo:- 

✍🏾 Sehemu #1: Fanya kazi nyakati ambazo wengine wamelala – Kadri wengine wanavyovuta shuka asubuhi na kuwahi kwenda kulala usiku wewe jitofautishe kwa kufanya kazi za ziada. Usiku chelewa kulala kwa kufanya kazi ambazo zina tija na asubuhi wahi kuamka kwa ajili ya maandalizi ya majukumu ya siku. Baada ya miaka kadhaa watakushangaa uliweza vipi kufikia mafanikio uliyonayo.

✍🏾 Sehemu #2: Jifunze wakati ambao wengine wanachati – Katika ulimwengu wa mafanikio unatakiwa kuwa kama nyoka katika hatua za ukuaji wake. Kadri nyoka anavyokua anaimarisha magamba yake mpaka inafikia hatua ambapo maganda hayo yanamzuia kuendelea kukua zaidi. Ili apate kukua zaidi ni lazima avue gamba na kuanzisha ukuaji upya. Katika ulimwengu wa mafanikio gamba linachukuliwa kama maarifa yanayokuzuia kusonga mbele. Ili ufanikiwe zaidi unatakiwa kuongeza maarifa kila mara.

✍🏾 Sehemu #3: Weka akiba wakati ambao wengine wanakula raha – Ni kupitia utaratibu wa kuweka akiba utaweza kuwa na uwezo kunufaika na fursa zinazojitokeza ghafla. Kadri utakavyofanikiwa kunasa fursa hizo ndivyo utaambiwa kuwa una bahati na kusahau kuwa bahati huwa inaenda kwa waliojiandaa. Pesa inaenda inakopendwa zaidi, hivyo jitofautishe na wengine kwa kuipenda pesa yako kupitia utaratibu wa kuweka akiba.

✍🏾 Sehamu #4: Ishi kana kwamba waone unavyoishi ni ndoto. Watu wengi waliofanikiwa huwa wanafanya vitu ambavyo awali vinaonekana kuwa ndoto kwenye macho ya watu wa kawaida. Ndiyo kwa wengine wataendelea kuona unafanya vitu visivyowezekana hila kwako wewe endelea kubadilisha ndoto na kuzoweka kwenye uhalisia wake.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kujitofautisha na kundi la watu wengine. Ikiwa unatamani kufika mbali hakuna namna zaidi ya kupiga hatua za ziada ikilinganishwa na kundi watu wanaokuzunguka. Anza sasa kuwa wa tofauti. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

[USHAURI] VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI KUANZISHA BIASHARA MPYA

NENO LA LEO (OKTOBA 23, 2020): [USHAURI] VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI KUANZISHA BIASHARA MPYA

πŸ‘‰πŸΎ Habari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya ambapo tunazawadiwa masaa 24 katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Wajibu tulionao ni kuendelea kutoa thamani dhidi ya jamii inayotunzunguka na viumbe vyote kwa ujumla. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza maeneo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara mpya. Linapokuja suala la kuanzisha biashara hasa kwa wajasilimali wadogo changamoto huwa ni nyingi. Kwa kutaja tu baadhi katika mazigira yetu huwa ni pamoja na: kukosekana kwa mtaji wa kuanzisha biashara husika, uhakika wa kushindana kwenye soko na uhakika wa wazo bora la biashara. Kupitia neno la tafakari ya leo nitakushirikisha sehemu za kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara yako ili uweze kukabiliana na changamoto hizi.

✍🏾 Tambua hamasa/shauku yako. Kuanzisha biashara ni sawa na kuanzisha familia kutokana na ukweli kwamba unahitaji kuwekeza muda, kufanya kazi kwa bidii pamoja na uwekezaji wa kifedha. Vyote hivi vinahitaji dhamira ya kweli kutoka ndani mwako hivyo kama hauna hamasa/shauku ya kutosha juu biashara husika itakuwa vigumu sana biashara nhiyo kukua. Kwa kifupi ni kwamba unahitaji una pendo wa hali ya juu kwenye biashara yako.

✍🏾 Tafsiri wazo lako kwenye mpango wa biashara. Mpango wako wa kibiashara unakuwa ni dira ya kukuongoza kwa ajili ya kufikia mafanikio unayohitaji. Mpango huu unapaswa kuonesha malengo ya baadae ikiwa ni pamoja na hatua utakazofuata kwa ajili ya kufikia malengo husika. Pia mpango huu kama umeandaliwa vyema unaweza kutumika kwa ajili ya kukuza mtaji kutoka kwa wafadhiri au taasisi za kifedha ikiwa ni pamoja kutumia mpango huu kwa ajili kusambaza bidhaa zako kwenye soko.

✍🏾 Fanya tafiti kuhusiana na wazo lako kama ni wazo sahihi sehemu unayotaka kuanzisha biashara. Kabla ya kuanzisha biashara hakikisha unafanya tafiti juu ya wazo lako la biashara ili uwe na taarifa sahihi zinazoendana na nyakati pamoja na sehemu husika. Taarifa hizi unaweza kuzipata kupitia semina za biashara, sehemu za masoko/biashara zinazozunguka eneo husika, maonyesho ya biashara, sehemu za viwandani au kwenye mitandao ya kijamii.

✍🏾 Tambua wapinzani wako wa karibu kwenye soko. Kwanza unahitaji kutambua kuwa washindani wako kibiashara sio maadui wako bali ni sehemu ya kujifunza mbinu zipi zimefanikiwa na zipi zimeshindwa kufanya kazi. Hii itakusaidia kuboresha mbinu zako kwa ajili ya kutoa huduma ambayo imeboreshwa ikilinganishwa na wapinzani wako. Taarifa za wapinzani wako unaweza kuzipata kupitia kwenye mitandao, semina za biashara, tafiti mbalimbali kuhusu bidhaa/huduma zinazotolewa na wapinzani wako.

✍🏾 Ainisha ni mitandao ipi ya kijamii ambayo unaweza kuitumia kutangaza biashara yako. Tambua umuhimu wa kutumia mindao ya kijamii kama vile facebook na twitter kwa ajili ya kupata taarifa sahihi kuhusu bidhaa/huduma unayokusudia kuitoa. Mitandao ya kijamii ni sehemu isiyo rasmi kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuboresha bidhaa/huduma unayokusudia kuitoa kulingana na wazo lako la biashara. Pia unaweza kutumia mitandao ya kijamii kufahamu mahitaji ya wateja katika soko linalokuzunguka.

✍🏾 Tafuta mwalimu/mshauri wako wa kibiashara. Mshauri wa biashara ni mtu muhimu kwa mtu anayeanzisha biashara kwa kuzingatia kuwa mshauri anakuwa tayari ana uzoefu wa kutosha katika sekta ya biashara. Msahauri huyu anahitaji kumpa mwanga pamoja na mwongozo mjasiliamali anayeanza safari yake ili akabiliane na mawimbi ya kibiashara. Ushauri huu utakusaidia kuepukana na makosa ya kibiashara ambayo yanaweza kupelekea upoteze mtaji wako.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza maeneo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara mpya. Biashara nyingi zinakufa kwa kuwa zinapuuza maeneo hayo wakati wa uanzishwaji wake. Kuwa wa tofauti katika biashara yako kabla ya kuianzisha. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

HUU NDIYO UTATU UNAOTAFUNA BIASHARA YAKO

NENO LA LEO (OKTOBA 22, 2020): HUU NDIYO UTATU UNAOTAFUNA BIASHARA YAKO

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku ya kipekee ambayo tumepewa kibali cha kuendelea kutoa thamani kwa wanaotuzunguka na viumbe vyote kwa ujumla. Tuendelee kutumia uhai huu kwa faida kwa kuwa wote hatujui mwisho wetu ni lini na siku hizo za mwisho zitawadia kwa njia ipi. Basi tuianze siku kwa kusema "hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani."

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza makosa matatu ambayo yanafanywa na wafanyabiashara wengi. Tafiti zinaonesha kuwa biashara nyingi (80%) zinazoanzishwa huwa zinakufa ndani ya kipindi cha miaka mitano toka kuanzishwa kwake. Pia, biashara zinazostahimili kuvuka kipindi hiko cha miaka mitano huwa zinaendeshwa kwa hasara na zimedumaa. Je wewe ni miongoni mwa wale ambao biashara yako imedumaa au ilishindwa kupenya kipindi cha miaka mitano? Haya hapa makosa yanayogharimu biashara nyingi:-

✍🏾 Kosa #1: Kutokuwa na utaratibu wa kutunza kumbukumbu. Wamiliki wengi wa biashara huwa wanakosa takwimu muhimu za mzigo unaoingia, mzigo uliotoka, faida iliyotengenezwa na gharama za uendeshaji wa kila siku. Hili ni kosa ambalo linatafuna biashara nyingi kwa kuwa mmiliki anashindwa kujua kama biashara inatengeneza faida au hasara. Hali hii inapelekea kushindwa kutofautisha mauzo ghafi pamoja na mtaji.

✍🏾 Kosa #2: Kukosekana na usimamizi mzuri wa mtaji na faida inayotengenezwa. Biashara nyingi huwa zinaendeshwa pasipokuwa na msimamizi anayewajibika moja kwa moja. Leo dukani yupo, kesho yupo baba na keshokutwa yupo mtoto. Hili siyo kosa ikiwa wote wanafuata misingi maalumu ya uendeshaji wa biashara husika. Ukweli ni kwamba biashara nyingi zinakufa kwa kuwa katika ngazi ya familia unakuta anayeielea vyema biashara husika ni mtu mmoja. Matokeo yake pindi anapoingia mtu mwingine dukani anafanya makosa yanayogharimu ukuaji wa biashara.

✍🏾 Kosa #3: Kutokuwepo mpango wa ukuaji wa biashara husika. Hili ni kosa ambalo linapelekea biashara nyingi zidumae na mwisho wake zitoweke kabisa. Kupitia mpango wa ukuaji mmiliki wa biashara anakuwa na mtazamo wa biashara yake katika vipindi tofauti kwa nyakatza baadae. Pamoja na mambo mengine mpango huu unaainisha namna ya kutafuta masoko mapya, jinsi ya kukuza mtaji na jinsi ya kuwekeza faida inayotengenezwa. Biashara nyingi hazina mpango wa aina hii na matokeo yake zinaendelea kuwa vile siku nenda rudi.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza makosa matatu ambayo yanagharimu ukuaji wa biashara katika mazingira yetu. Yapo makosa mengi hila kwa kuanzia anza kurekebisha hayo kwenye biashara yako ili uone tofauti.  Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

HII NDIYO NJIA RAHISI YA KUPIMA UTAJIRI WAKO

NENO LA LEO (OKTOBA 21, 2020): HII NDIYO NJIA RAHISI YA KUPIMA UTAJIRI WAKO

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku mpya na ya kipekee katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Kipekee kabisa natarajia umeamka ukiwa na nguvu na hamasa ya kutosha kwa ajili ya kuendelea kuwa mtu wa thamani kwa jamii na viumbe wanaokuzunguka. Basi tuianze siku kwa kusema "hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani."

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza njia rahisi ya kugundua kama wewe ni tajiri, mtu wa kipato cha kati au masikini. Mara nyingi mtaani linapotamkwa neno utajiri wengi huwa wanakimbilia kwenye tafsiri ya umiliki wa pesa. 

✍🏾 Ukweli ni kwamba utajiri ni zaidi ya umiliki wa pesa kwa kuwa utajiri unapimwa kwa pesa taslimu, mali zisizohamishika, mali zinazohamishika, pesa zilizoko Benki au umiliki wa pesa kwenye masoko ya mitaji. Muunganiko wa vyote hivyo ndivyo vinaunda utajiri wa mtu.

✍🏾 Je ntawezaje kujua kuwa mimi ni tajiri? Mwanamafanikio Robert Kiyosaki huwa anasema utajiri wa mtu unapimwa na "idadi ya siku ambazo ataweza kuishi bila kufanya kazi huku akijitoaheleza kwenye mahitaji yake yote bila kuteteleka". Fikiria tukio la ghafla ambalo linakuacha kwenye mazingira ambayo hauwezi kufanya kazi. Katika mazingira hayo ambayo utakuwa haufanyi kazi ikiwa utaendelea kukidhi mahitaji yako ya msingi kwa kipindi cha muda wote utakaoishi basi wewe ni tajiri mkubwa.

✍🏾 Hata hivyo, katika jamii tuna idadi kubwa ya watu ambao ili waendelee kuishi ni lazima wafanye kazi. Huu ni ukweli husiopingika kwa kuwa ridhiki inapatikana kadri mtu anavyojibidisha kila siku. Ridhiki ya wengi ipo mikononi mwao kila siku.

✍🏾 Je nawezaje kuongeza siku za kuishi bila kufanya kazi? Ili uongeze siku ambazo unaweza kuishi pasipo kufanya kazi unalazimika kuweka mazingira ambayo pesa itakuwa inafanyia kazi hata katika kipindi ambacho umelala. Hapa unatakiwa kuweka nguvu kwenye umiliki wa mali zisizohamishika na zinazohamishika pamoja na umiliki wa pesa kwenye masoko ya mitaji.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza njia rahisi ya kugundua kama wewe ni tajiri, mtu wa pato la kati au masikini. Anza sasa kuongeza siku ambazo unaweza kuishi pasipo kufanya kazi.  Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

SIRI 6 AMBAZO MATAJIRI HAWATAKUAMBIA

NENO LA LEO (OKTOBA 20, 2020): SIRI 6 AMBAZO MATAJIRI HAWATAKUAMBIA.

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo tumejaliwa kuwa na pumzi ya bure katika siku za uhai wetu. Ni siku ambayo naendelea kukumbusha kuwa kila siku ambayo unabahatika kuishi ni msingi wa kujenga mlima wa mafanikio katika maisha yako. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza siri sita ambazo matajiri wengi wanazitumia kukuza utajiri wao. Mara ukipata nafasi ya kuongea na tajiri yeyote wengi huwa hawataki kuweka wazi jinsi walivyofanikiwa kuwa na tajiri au jinsi gani wanafanikisha kukuza utajiri wao. Wapo ambao watakukatisha tamaa kuwa kutengeneza utajiri siyo jambo jepesi na ni watu wachache ambao wamebalikiwa kuwa na kariba ya namna hiyo. Pia wapo ambao kwa haraka haraka watakuambia ni rahisi kuwa tajiri bila kukuambia kwa undani unatakiwa kufanya nini ili uwe tajiri. Karibu tujifunze siri 6 ambazo zinatumiwa na matajiri wengi:-

✍🏾 Siri #1: Mshahara pekee hauwezi kukufanya uwe tajiri. Wafanyakazi wengi ambao wanategemea mshahara pekee maisha yao ni kuishi mwezi kwa mwezi (mshahara kwa mshahara). Maana yake ni kwamba kiwango wanacholipwa kupitia mshahara ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kawaida katika maisha. Niliwahi kuandika kuwa wanaopanga viwango vya mshahara huwa wanaweka kiwango ambacho kitamfanya mhusika aendelee kufanya kazi ili apate mshahara. Kama umeajiriwa anza sasa kutafuta kipato cha ziada nje ya mshahara.

✍🏾 Siri #2: Mfumo wa bei ni miongoni mwa wezi wanaoiba utajiri wako. Ni wazi kwamba thamani ya pesa ya leo haiwezi kuwa sawa na kesho kulingana na mabadiliko ya mfumuko wa bei yanayotokea. Ili pesa iendelee kuwa na thamani dhidi ya mfumuko wa bei inatakiwa kuwekezwa sehemu ambapo inaongezeka thamani. Anza kuwekeza sasa.

✍🏾 Siri #3: Nunua vitu vinavyoongezeka thamani (assets) na epuka kununua vikorokoro (liabilities). Hii ni siri kubwa ambayo inatenganisha watu tajiri na watu masikini. Masikini mara nyingi wanajikita kununua vitu ambavyo thamani yake inapungua kwa kipindi cha muda wakidhania kuwa ni rasilimali (assets). Vitu hivyo vinaendelea kuwagharimu kila siku kutokana na gharama za matunzo au uendeshaji. Kinyume chake ni sahihi kwa watu tajiri kwenye kununua.

✍🏾 Siri #4: Epuka kuwa na matumizi yanayozidi pato lako.  Masikini mara nyingi wanajiingiza kwenye mikopo kutokana na kuwa na bajeti kubwa inayozidi pato wanaloingiza. Matokeo yake madeni yanaendelea kuwatafuna siku hadi siku. Ikiwa unahitaji kuwa tajiri ni lazima uhakikishe unatumia pungufu kuliko pato lako.

✍🏾 Siri #5: Mara zote jilipe kwanza! Huu ni muujiza mwingine katika ulimwengu wa kutengeneza utajiri. Siri hii inakutaka kuhakikisha kila shilingi inayoingia mikononi mwako utenge asilimia flani (10 - 15) kwa ajili ya kuwekezwa sehemu ambapo inaongezeka thamani.

✍🏾 Siri #6: Muujiza wa ongezeko la riba katika kipindi cha muda maalumu. Ikiwa umewekeza pesa yako sehemu ambayo kila mwaka inaongezeka kwa asilimia flani, baada ya mwaka wa kwanza pesa iliyowekezwa itaongengezeka kwa asilimia inayotolewa na taasisi husika kama ongezeko la riba. Katika mwaka wa pili pesa yako itaongezeka kuanzia kwenye thamani yake ya mwisho wa mwaka wa kwanza. Hali hiyo itaendelea mpaka mwisho wa kipindi cha uwekezaji.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza siri 6 ambazo zitakuza utajiri wako. Anza sasa kwa kuwa kesho huwa haina mwisho.  Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

JE NI MARA NGAPI UNAJILAZIMISHA KUTOKA KWENYE UKANDA WA FARAJA?

NENO LA LEO (OKTOBA 19, 2020): JE NI MARA NGAPI UNAJILAZIMISHA KUTOKA KWENYE UKANDA WA FARAJA?

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya katika juma jipya ambapo tunaalikwa kuendeleza yaliyo mema kwa kuwa hayo ndiyo yanayapa thamani maisha yetu. Ni asubuhi leo unakumbushwa kuendelea kupiga hatua kila siku zinazolenga kukufikisha kwenye ushindi unaotamani. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza umuhimu wa kuukimbia ukanda wa faraja (comfort zone). Kwa asili mwili wa binadamu unapenda raha kiasi ambacho hauko tayari kupokea mabadiliko ya haraka katika mazoea yaliyojengeka muda mrefu. Ni kutokana na hali hiyo watu wengi hawako tayari kuachana na mazingira waliyozoea au tabia zilizozoeleka na kuingia kwenye maisha mapya ambayo pengine hayana uhakika wa baadae.

✍🏾 Mwaka 1975 kijana Bill Gates akiwa na umri wa miaka 19 aliamua kuukimbia mfumo wa maisha uliozoeleka katika jamii. Sawa na ilivyo kwa vijana wengine Bill alilewa katika hali ambayo aliaminishwa kuwa ili ufanikiwe unatakiwa kwenda shule, usome kwa bidii, ufahulu masomo na mwisho wake upate kazi nzuri yenye malipo mazuri. Kijana Bill aliamua kubeba hatari ya kuukimbia mfumo kwa kuachana na masomo ya chuo kikuu katika Chuo cha Harvard.

✍🏾 Kijana Bill katika hali ya kushangaza akiwa hana mtaji wa rasilimali fedha ($0) akaona kuna maisha nje masomo ya chuo (ukanda wa faraja). Pamoja na kwamba kijana Bill hakuwa na mtaji wa fedha kuna vitu ambavyo alikuwa navyo katika ulimwengu wa ujasiliamali. Kubwa zaidi alikuwa na maarifa, taarifa sahihi na alijiamini kuwa anaweza. Kwa sifa hizo, kijana Bill aliungana na mwenzake Allen na kuanzisha kampuni ya Microsoft ambayo ilijikita kwenye kutengeneza "software" za kompyuta.

✍🏾 Kwa misingi ileile ya kuamini kuwa anaweza, leo hii (2020) tunapomzungumzia mzee Bill kampuni yake ina thamani ya USD trilioni moja. Tunaweza kuelezea mafanikio ya Bill Gates katika kila hali tunavyotaka, lakini pointi muhimu ya kukumbuka ni kwamba amefanikisha yote hayo kwa kuwa aliweza kuukimbia ukanda wa faraja katika muda na umri sahihi. 

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza umuhimu wa kuukimbia ukanda wa faraja katika umri na wakati sahihi. Kila mmoja wetu ana ukanda wake wa faraja ambao unamzuia kufikia mafanikio anayotamani. Jiulize ni ukanda upi wa faraja ambao umeendelea kukuzuia kufika kule unakotamani na kisha jivike bomu kwa kuukimbia ukanda huo.  Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

[HUSISHANGAE] HIVI NDIVYO UNAWEZA KUONGEZA MUDA WAKO!

NENO LA LEO (OKTOBA 17, 2020): [HUSISHANGAE] HIVI NDIVYO UNAWEZA KUONGEZA MUDA WAKO!

πŸ‘‰πŸΎHabari ya asubuhi rafiki yangu na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya na ya kipekee ambayo tunazawadiwa tena katika akaunti ya siku za maisha yetu. Ni siku ambayo tunaongozewa masaa 24 kwa ajili ya kuendelea kutoa thamani dhidi ya jamii inayotunzunguka na viumbe vyote kwa ujumla. Kumbuka wajibu wetu mkubwa katika maisha ya kila siku ni kuibadilisha Dunia hii kuwa mahala pazuri pa kuishi. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza namna ya kuongeza muda wetu katika kila siku tunayobahatika kuishi. Muda ni rasilimali ambayo watu wote tumepewa sawa kwa maana wote tuna masaa 24 katika siku na siku 7 kwa wiki. Pamoja na kwamba wote tumepewa rasilimali hii kwa vipimo sawa wapo watu ambao wanaona muda hautoshi na wengine wana muda wa kutosheleza kufanya yale ya muhimu katika maisha yao ya kila siku. Kiukweli ni kwamba muda haujawahi kutosha kwa watu wengi kwa kuwa mambo ni mengi kuliko muda wenyewe. Pamoja na kwamba muda ni mchache zipo mbinu ambazo unaweza kutumia ili kuhakikisha unapata muda wa kutosha kutekeleza majukumu muhimu katika siku. Karibu ujifunze mbinu hizo:-

✍🏾 Mbinu #1: Unaweza kuongeza muda kwa kuamua kupotezea au kusema hapana. Unaweza kuokoa muda wako kwa kupotezea au kusema hapana kwa baadhi ya vitu ambavyo havina tija katika maisha yako. Hapa unahitaji kuwa jasiri wa kukataa kuwa kila sio linalokuja kwenye fikra zako au mbele yako lazima lifanyiwe kazi au siyo kila anayekuja utimize haja zake. Mfano, unaweza kuachana na tabia ya mabishano, kufanya kazi za wengine ambazo sio lazima ufanye wewe, kuangalia vipindi vya TV ambavyo havina tija, kupoteza muda kwenye mitandao, epuka vikao visivyo na tija, na epuka kazi za kujitolea ambazo zimepitiliza. Tabia hizi zinapoteza muda ambao ungeutumia kwa ajili ya kuwa karibu na familia yako au kufanya mambo mengine ambayo ni muhimu.

✍🏾 Mbinu #2: Wekeza muda wako kupitia maamuzi yako ya fedha. Maamuzi ya fedha unayofanya kwa sasa yana mchango mkubwa wa kuamua hatima ya kipato chako na muda wako kwa siku zijazo. Kabla ya kufanya matumizi yoyote tambua kuwa thamani ya pesa hiyo kwa kesho ni kubwa endapo imewekezwa sehemu sahihi kuliko ikitumiwa sasa. Kutokana na msingi huu unatakiwa kufahamu kuwa kila shilingi unayoitumia kwa sasa ina athari kubwa kwenye nafasi yako ya kifedha kwa miaka ijayo. Hapa unaweza ukajitathimini kwenye matumizi yako ya fedha ambayo siyo ya lazima kama ununuzi wa vocha, magazeti, uvutaji wa sigara, ulevi au matumizi ambayo hayapo kwenye bajeti yako. MUDA UNA THAMANI ZAIDI YA PESA KUTOKANA NA UKWELI KUWA MUDA UKITUMIWA VIZURI UNATENGENEZA PESA AMBAZO ZITAENDELEA KUJITENGENEZA ZENYEWE.

✍🏾 Mbinu #3: Unaweza kuongeza mudwa wako kwa kugatua madaraka/kazi AMBAZO ZIPO JUU YA UWEZO WAKO AU SIYO ZA KIWANGO CHAKO. Fanya tathimini ya majukumu ya kazi zako za kila siku na kisha jiulize kama kuna ulazima wa kazi zote kufanywa na wewe. Chagua kazi ambazo unaona unaweza kumfundisha mtu wa chini yako azitekeleze kwa niaba yako. Kwa kufanya hivyo utakuwa umeokoa muda ambao utautumia kufanya mambo mengine. Pia, sehemu nyingine ya kugatua madaraka ni kwa majukumu ambayo yapo nje ya uwezao wako. Mafanikio yanahusisha kujenga timu ya watu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano, hivyo, ili ufanikiwe ni lazima uwe tayari kuamini kuwa kazi yako inaweza kufanywa na mtu yeyote kwa viwango unavyohitaji.

✍🏾 Mbinu #4: Unaweza kuongeza muda wako kwa kuairisha baadhi ya majukumu pale inapobidi. Watu waliofanikiwa wanafahamu kama endapo kuna ulazima wa kazi husika kukamilishwa kwa sasa au kusubirishwa kwa baadae kwa kutegemea umuhimu wake kwa wakati husika. Kwa ujumla kila kazi au maamuzi unayofanya ni lazima kwanza usome alama za nyakati. Kama alama za nyakati haziruhusu kazi/maamuzi husika kufanyika kwa wakati huo hakuna haja ya kulazimisha kufanya maamuzi hayo na badala yake ni vyema ukasubiria kwa baadae.

✍🏾 Mbinu #5: Ongeza muda wako kwa kutuliza akili katika mambo yaliyo ya muhimu au yenye tija. Zipo nyakati ambazo utatakiwa kufanya kazi mara mbili zaidi ya ulivyozoea kwa ajili ya kuhakikisha unakamilisha majukumu yaliyopo mbele yako. Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa rasilimali zote unazielekeza kwenye jukumu husika kwa kadri zinavyotakiwa mpaka pale ambapo utaona kuwa umefanikisha kukamilisha jukumu hilo. Hapa unahitaji kuongeza muda wako kwa kuhakikisha unafanyia kazi ambayo ni ya kipaumbele kwa wakati husika na si vinginevyo. Hakikisha haurusu mwingiliano wa vitu vingine ambavyo vinaweza kukupoteza kwenye kipaumbele chako. Pia, katika zoezi la kuongeza muda ni lazima uhakikishe vipaumbele vyako vina muunganiko wa matukio kiasi kwamba kukamilika kwa kipaumbele kimoja kunapelekea kuanza kwa kipaumbele kingine. Pia, kipaumbele kimoja kisaidie kuongeza muda kwa ajili ya kipaumbele kinchofuatia.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza mbinu tano ambazo tunaweza kuzitumia kuongeza muda wetu. Ni mbinu ambazo kila mmoja anaweza kuzitumia kwa kuwa ni rahisi kutumiwa katika majukumu yetu ya kila siku. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia maarifa kwenye elimu ya pesa kupitia usomaji wa vitabu. Chagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka kwa kubofya kiunganisha hapo chini. Kila nakala ya uchambuzi wa kitabu inapatikana kwa gharama ya Tshs. 3,999. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.

BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Kujiunga Kundi la WhatsApp la FIKRA ZA KITAJIRI ili upate mafundisho haya kila siku, bofya link hii: https://chat.whatsapp.com/JACBxr9kX7K0qt58cQTrrw

Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com