MATOKEO YATAKUELEZEA ZAIDI KULIKO MIPANGO ULIYONAYO

NENO LA LEO (SEPTEMBA 14, 2020): MATOKEO YATAKUELEZEA ZAIDI KULIKO MIPANGO ULIYONAYO.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni asubuhi mpya katika juma jipya ambapo tunaianza wiki ya tatu katika mwezi Septemba. Ni siku ya kipekee ambapo tunaweza kusikia kwa mbali sauti za ndege wa kila aina ambazo zinadhihirisha ukuu wake Muumba. Kama ilivyo kwa ndege na sisi tunaalikwa kwa ajili ya kuendelea kumtukuza Muumba wetu kupitia kazi za mikono na akili yetu. Basi kila mmoja wetu aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza muhimu wa kuifanya mipango yetu kuwa siri ili kila inapokamilishwa matokeo yaongee kwa niaba yetu. Bahati mbaya tunaishi katika Ulimwengu ambao kila mtu anatamani kuonesha kile anachofanya hata kama kipo hatua za awali. Bahati mbaya zaidi ni pale ambapo matukio ya Ulimwengu wa sasa ni feki (the world of fake events).

✍🏾 Katika Ulimwengu huu wenye matukio ya uongo tunashuhudia watu waki "post" picha kwenye mitandao ya kijamii zenye kuonesha kuwa wamepiga hatua katika yale wanayofanya. Bahati mbaya sana picha nyingi zinazowekwa ni zile zinazoonesha upande wa mafanikio pekee na kuficha upande wa vikwazo au sehemu ambazo mhusika ameshindwa kufanikiwa. 

✍🏾 Ni katika Ulimwengu wa sasa ambapo tunashuhudia watu wapo radhi kupiga cha uongo na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii ili kuwahadaa watu waliopo kuwa mhusika amepiga hatua kimafanikio. Ni katika Ulimwengu wa sasa watu wamegeuza mitandao ya kijamii kuwa sehemu ya kuhifadhia kumbukumbu zao hasa zinazoonesha picha zenye matukio mazuri pekee.

✍🏾 Yote hayo yanafanyika kwa kuwa watu wengi wanataka jamii ifahamu wanafanya nini. Wengi wanaitahiji jamii ijue kuwa wapo na wanajihusisha mambo muhimu ya kimaendeleo. Wengi wamefikia hatua ya kuongelea mipango yao hata kama hawajaulizwa. Ukweli ni kwamba watu wanafanya hivyo kama kujipatia heshima kwa jamii inayowazunguka kuwa wanapambana kimaisha kwa ajili ya kufikia mafanikio wanayotamani.

✍🏾 Hata hivyo, watu wengi wanatumia nguvu kubwa kuelezea mipango yao ya maisha kwa kuwa jamii haina muda wa kusikiliza mipango waliyonayo. Jamii hiyo hiyo ndo inakatiza mipango mingi ya hao wanaotumia nguvu kuelezea mipango yao kwa kuwa ndani ya jamii kuna watu wa kila aina. Wapo ambao wanajifanya kujua kila kitu faida na hasara zake wakati hawajawahi kufanya. Wapo ambao  mara zote wanawaza matokeo hasi kiasi ambacho kila utalowaambia unakusudia kufanya watakuambia hilo haliwezekani. Hiyo ndiyo jamii ambayo unapambana kuelezea mipango yako.

✍🏾 Kumbe, kuendelea kupambana kuelezea mipango yako kwa kila mtu ni kupoteza muda. Unatakiwa kuifanya mipango yako siri na kuhakikisha unaishi vitendo vya kuiweka mipango hiyo kwenye uhalisia wako. Kadri utakavyoishi vitendo ndivyo utapata matokeo ambayo yatajitangaza yenyewe. Ni rahisi jamii kuelewa uhalisia wako kupitia matokeo kuliko kupitia mipango uliyonayo.

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa mipango tuliyonayo kwenye kila sekta ya maisha yetu inatakiwa kuwa siri. Jamii inataka kuona matokeo ndipo ikuelewe zaidi kuliko unavyopambana kuelezea mipango yako. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika biashara yako itastawi. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(