NENO LA LEO (SEPTEMBA 19, 2020): HIVI NDIVYO UNAWEZA KULITAMBUA KUSUDI LA MAISHA YAKO.
Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine ambayo tuna kila sababu ya kumshukuru Muumba kutokana na kibali cha uhai ambacho tumezawadiwa. Wajibu wetu ni kutumia kibali hiki kwa ajili ya kuendeleza bidii ya kubadilisha maisha yetu roho, kiafya, kiuchumi na kijamii. Basi kila mmoja wetu aianze siku kwa kusema hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema siku hii kwa ajili ya kuongeza thamani ya maisha yangu hapa Duniani.
JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.
👉🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza maana halisi ya kusudi la maisha na jinsi unavyoweza kuishi maisha ambayo umeumbiwa kuyaishi hapa Duniani. Mara nyingi nimekuwa nikiulizwa maswali na baadhi ya wasomaji wa Makala zangu ambayo yanalenga kujua maana ya kusudi la maisha na namna ambavyo mtu anaweza kuishi kusudi la maisha yake. Karibu tujifunze wote ili kupitia neno la tafakari ya leo tupate ufunuo wa kuishi kusudi halisi ya maisha yetu.
✍🏾 Je kusudi la maisha ni nini? Kusudi la maisha yako ni lile lengo pana la maisha yako ambalo ni: “imara, linajumuisha kila sekta ya maisha yako na unapaswa kulikamilisha katika kipindi cha uhai wako si tu kwa ajili ya faida yako bali kwa ajili ya jamii nzima”. Somo la kujifunza hapa ni kuwa kusudi la maisha ni (a) lengo kubwa ambalo ni msingi wa maisha yako yote (b) imara na halitakiwi kubadilika mara kwa mara (c) ni ufunguo wa kuujua ukweli wa uliumbwa kukamilisha nini hapa Duniani (d) linajikita kwenye kukamilisha kitu katika maisha yako si tu kwa faida yako bali kwa ajili ya wengine.
✍🏾 Je kusudi la maisha yangu nitalipata wapi? Unaweza kupata kusudi la maisha yako sehemu yoyote ile. Kusudi la maisha yako linaweza kuwa kwenye jamii inayokuzunguka, marafiki, ndugu, familia, imani (kanisani au msikitini), jamii na hata kwa watu walio mbali na upeo wako. Mfano katika ngazi ya familia kusudi la maisha yako linaweza kuhusisha msaada kwa wanafamilia wote ili wapate kufikia ndoto zao au kuwasaidia wale wasiojiweza katika jamii inayokuzunguka. Vivyo hivyo, kwa ngazi ya familia kusudi la maisha yako linaweza kuwa baba/mama bora. Hivyo hauna sababu ya kuumiza kichwa sana kufikiria ni wapi utapata kusudi la maisha yako badala yake anzia hapo ulipo.
✍🏾 Je natakiwa kuanzia wapi katika kuliishi kusudi la maisha yangu? Katika kutafuta ukweli wa umeumbwa kwa ajili ya nini hapa Duniani unatakiwa kupata majibu ya maswali mawili (a) Je wewe ni mtu wa aina gani? na (b) Je dunia unayoishi ina asili gani?. Majibu ya maswali haya ndio yanayopima kiwango na ubora wa mahusiano yako dhidi ya familia, marafiki, waajiri au waajiriwa wetu au jamii nzima kwa ujumla. Swali la kwanza linalenga kukufanya ujitambue kwa nini hasa uliumbwa na kwa nini bado unaishi wakati swali la pili linalenga utambue uhusiano wako na mazingira yanayokuzunguka.
✍🏾 Je nitajuaje kuwa tayari naliishii kusudi la maisha yangu? Katika hatua za ukuaji wa mwanadamu inafikia hatua ya kilele cha mabadiliko/maendeleo na hapa ndipo mwanadamu anakuwa kwenye hatua ambayo jitihada zake zimechanua matunda katika kila sekta ya maisha yake. Matunda haya yanajumuisha ukuaji wa kiroho, upendo, uvumilivu, kijitambua kimwili, uwezo wa kuchanganua mambo na uwezo wa mawasiliano dhidi ya wanaomzunguka. Hapa ndipo mwanadamu analiishi kusudi la maisha yake kwa viwango vilivyokusudiwa toka enzi za kuumbwa kwake. Ni katika kipindi ambacho mhusika pamoja na jamii inayomzunguka wanafurahia matunda ya kusudi la maisha yake.
✍🏾 Je kuna athari gani za kutotambua kusudi la maisha yako? Mwanadamu anapokuwa hajajua kusudi la maisha yake anakuwa ni sawa na ombaomba ambaye siku zote anakalia boksi kuomba vicenti vya hela kumbe ndani ya hilo boksi kuna kila kitu cha thamani. Kila mmoja ndani yake ana mbegu za kufanya mambo makubwa huku akiongozwa na roho lakini kutokana na kwamba watu wengi hawatambui kusudi la maisha yao wanaishia kufanya vitu vya kawaida kwa ajili ya kuridhisha tamaa za mwili. Mwandishi anatushirikisha kuwa kama haujatambua kusudi la maisha yako kwa maana ya kufikia kilele cha ukuaji wa kiroho wewe ni ombaomba ambaye unahitaji kujitambua kuwa haupaswi kuwa ombaomba kwani ndani mwako kuna kila kitu cha thamani.
✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuhusu kusudi la maisha na jinsi ya kuliishi kusudi la maisha yako. Fanyia kazi mafundisho haya ili maisha yako yawe na thamani kwako na jamii inayokuzunguka. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.
PS: Neno la tafakari ya leo limeandaliwa kutoka kwenye uchambuzi wa Kitabu cha “The Power of Now” kutoka kwa mwandishi Eckhart Tolle na uchambuzi wa kitabu cha “Noble Purpose” ambacho kimeandikwa na mwandishi William Damon. Hakikisha unajifunza zaidi kuhusiana na kusudi la maisha yako kwa kulipia Tshs. 4,999/= ili ujipatie nakala za vitabu hivi vyote. Wahi mapema hii ni OFA ya leo.
👐🏾 Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.
BORN TO WIN ~ DREAM BIG
Mwalimu Augustine Mathias
Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410
Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com
Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com
onclick='window.open(