FAHAMU WATU AMBAO UNATAKIWA KUWAKIMBIA.


NENO LA LEO (SEPTEMBA 15, 2020): FAHAMU WATU AMBAO UNATAKIWA KUWAKIMBIA.

Habari ya asubuhi rafiki yangu mpendwa na mwanafamilia ya FIKRA ZA KITAJIRI. Ni siku nyingine tena katika siku za uhai wetu hapa Duniani. Wote tunaalikwa kuitumia siku hii kwa ajili ya kufanya yale yanayoleta thamani kwetu na jamii inayotuzunguka. Kubwa zaidi ni kuendelea kutambua kuwa maisha yetu ni kwa ajili ya ukamilisho wa kusudi maalum hapa Duniani. Basi kila mmoja wetu aseme hii ndiyo siku bora aliyoifanya Bwana, nitafurahi, nitamshukuru na kuitumia vyema ili nipate yaliyo bora katika maisha.

JIUNGE NA KUNDI LA WHATSAPP LA FIKRA ZA KITAJIRI KWA  KUBONYEZA HAPA NA KUJIUNGA BURE. Jiunge sasa nafasi ni chache.

✍🏾 Karibu katika neno la tafakari ya leo ambapo tutajifunza aina ya watu ambao unatakiwa kujiweka mbali nao ili ufanikishe mipango yako. Tumeona katika utangulizi wa somo hili kuwa maisha yetu ni kwa ajili ya ukamilisho wa kusudi maalumu hapa Duniani. Na kusudi hilo linahusisha kujitoa kwa ajili ya watu wengine au viumbe wengine. Na katika kujitoa huko ndivyo na mhusika anafanikisha ndoto alizonazo kuhusu maisha.

✍🏾 Kutokana na ukweli kwamba mwanadamu ni kiumbe anayeishi katika makundi ya kijamii, hakuna namna kiumbe huyu ataweza kuliishi kusudi la maisha yake bila kujikuta anazungukwa na watu. Maisha ni kutegemeana, hivyo ili kufanikisha ndoto ulizonazo kuna makundi ya watu ambayo yatakuwa na msaada mkubwa kwako. Hata hivyo katika safari yako kuwa makini na watu hawa:-

✍🏾 Kundi #1: Wale ambao mara zote hawakuambii ukweli. Watu wa aina hii ni wengi katika jamii. Mara zote watakuambia uongo ili waendelee kuwa karibu na wewe. Pengine uongo huo huwa unahusisha kuficha mapungufu yako ili mradi waendelee kunufaika na mahusiano yenu. Kama unahitaji mabadiliko halisi katika maisha aina ya watu hao unatakiwa kukaa nao mbali.

✍🏾 Kundi #2: Ambao wanalenga kukutumia. Kwenye jamii huwa kuna watu wanaopendelea uhusiano wa upande mmoja kunufaika (symbiotic relationship). Kundi hili la watu litafanya kila linalowezekana ili mradi liendelee kujinufaisha kutoka kwako. Hawa nao unatakiwa kuwakimbia tena bila kuaga.

✍🏾 Kundi #3: Wanaopambana kukuangusha. Kundi hili huwa linahusisha watu ambao wanajifanya marafiki lakini ndani mwao ni wapinzani wako wakubwa. Hawa wanaweza kukuangamiza kimya kimya bila ufahamu wako na katika kipindi hicho ukawa unaendelea kuwashirikisha mipango yako.

✍🏾 Kundi #4: Ambao hawakuheshimu. Kundi hili linahusisha watu ambao hata ufanye nini ambalo jema kwao utaendelea kuonekana si lolote. Watu hawa ukiendelea kuwa karibu nao utakatishwa tamaa ya kuendelea kufanikisha ndoto ulizonazo. 

✍🏾 Mwisho, kupitia neno la tafakari ya leo tumejifunza kuwa kuna watu ambao ili ufanikiwe kimaisha huna budi kuwakimbia. Mara nyingi watu hao huwa ni watu wa karibu na sisi hivyo unatakiwa kufanya maamuzi magumu ya kuwakimbia. Fanyia kazi mafundisho haya na hakika biashara yako itastawi. Kumbuka, mbegu ikidodoka ardhini ni lazima iote na kuzaa matunda, nami naiombea mbegu hii niliyodondosha kupitia neno la tafakari ya leo ipate kuzaa matunda mengi katika Maisha yako.

PS: Unaweza kujipatia nakala ya uchambuzi wa Vitabu ambavyo vitakufanya upige hatua kwenye kila sekta ya maisha yako kwa gharama ndogo kabisa. Lipia sasa vitabu viwili ili upate na kimoja cha OFA. Kuchagua nakala za uchambuzi wa vitabu unavyotaka bofya kiunganisha hapo chini na kuchagua kitabu.

πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ 

BOFYA HAPA KUPATA ORODHA YA UCHAMBUZI WA VITABU

πŸ‘πŸΎ Nakutakia kila la kheri kwenye siku hii ya leo. Kumbuka husikose kutoa mrejesho wa kile ambacho unajifunza kutokana na uwepo wako kwenye kundi hili.


BORN TO WIN ~ DREAM BIG

Mwalimu Augustine Mathias

Mawasiliano: 0763 745 451/0786 881 155/0629 078 410

Barua pepe: fikrazakitajiri@gmail.com

Tovuti: fikrazakitajiri.blogspot.com

onclick='window.open(